Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tunamuunga mkono Maalim Seif kwa Urais Zanzibar. Lissu hataendelea na kampeni, atapangiwa majukumu mengine

Vyama vilivyokataa Lissu aendelee na kampeni navyo vimeambiwa vinapokea maagizo ina maana CCM wana nguvu
 
Mbowe ni Mtanzania...siyo kibaraka wa mabeberu Kama Lissu...anatanguliza Tanzania Kwanza...Lissu anamtanguliza Amsterdam na mabeberu wengine...
Mbowe ni Mzalendo, hayuko tayari kuona damu za watanzania zinamwagika sababu ya kulazimisha kuingia Ikulu. Historia ya Tanzania itamkumbuka daima. Sio wale jamaa na Lisu wao wanaotamba kuingiza nchi kwenye machafuko wabebe madini na rasilimali za Tanzania.
Queen Esther
 
Unafikiri hawajui matendo yenu??? Unafikiri hawajui kuwa mnaua ili kutengeneza balance badae??? Unafikiri hawajui kuwa kila kesi inayotokea saivi mnawapa Chadema ili kubalance tuhuma???!

Subirini tu😂😂😂😂✌
Umeweka upuuzi hapa....hivi kiwango chako Cha elimu kikoje?! It is no wonder unashabikia mauaji...yaani CCM hii iue watu eti ili kubalance mauaji..what a stupid comment?! Yaani mmeishiwa hoja...yaani mmekaa kusubiria mabeberu eti wachukue hatua...ndiyo maana nyie wenyewe mnachoma ofisi za chama chenu ionekane kuwa ni CCM au serikali..very stupid indeed...yaani mmewaua wale vijana kikatili Sana...na damu yao itawaandama kokote muendako...Kama kweli wewe ni jasiri jitambulishe hapa ufahamike ...
 
Hivi unadhani anachosema huyo jamaa hakifahamiki na hizo ngazi za juu? Hizo ngazi za juu wanajua sana na wao ni sehemu ya hayo maagizo ili wapate hela.


Sidhani mkuu ila naamini kuna baadhi ya watendaji wana 'take advantage ' kupitia mpango wa kukomesha uvuvi haramu
 
*CHADEMA PUMZI IMEKATA*

Baada ya akusikiliza kwa makini hituba ya Mbowe yangu ni haya yafuatayo:-

1. Mhe. Mbowe unaposema chama chenye ushindani na CCM ni Chadema peke yake huoni unadhalilisha vyama vingine vya upinzani?. Hata Chadema ilianza mdogo mdogo leo ipo hapo ilipofikia. MBONA UNAUA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI?

2. Mhe. Mbowe unaposema kura za vyama vitatu tu kati ya vyama karibu 17 ndio vimepinga kusimamishwa kwa Lissu huoni hiyo ni DEMOKRASIA??? Mbona unaikosoa tena!

3. Mhe. Mbowe! Kwanini mmeamua kuungana baada ya kuona maji yapo shingoni? Mhe. Membe alisisitiza sana muungane mkamgomea! Leo uchaguzi umebaki siku 24 na mmeambiwa maandalizi yamekwisha ndio mnaungana?! Huko ni kutafuta nongwaaaa baada ya kuona mmeshindwa!! Waliokiunga CCM mkono walifanya hivyo kabla kipenga hakijapulizwa. Sasa kipenga kimepulizwa imebaki kama robo kazi iishe mnataka kuungana!! Mwogopeni Mungu wajameni!!

4. Hatujaona mahali mnakemea wana CCM wanaouliwa na kujeruhiwa na wafuasi wenu. Mkt wa CCM Taifa Dr. Magufuli aliwatangazia wanachama wake kisasi ni cha Mungu!! Akaonya wasilipize kisasi!! Huo ni uungwana wa hali ya juu.

5. Ratiba za kampeni kila chama kilipeleka chenyewe kwenye Tume. Leo unalalamikia ratiba uliyotengeneza mwenyewe!! Mambo ya ajabu kabisa na ni kuleta vurugu kwenye nchi!! Mlipoanza mashindano mlikutanishwa wote na mkasaini, leo unasema huyu atolewe! DEMOKRASIA gani hiyo! Hivyo vyama navyo vina fursa na vitakua kama Chadema. Kumbuka kulikuwa na chama chenye nguvu kabla ya Chadema na hawakusema Chadema inaunga mkono CCM.

6. Kila chama kiliwasilisha Tume majina ya watakaopiga kampeni. CCM iliwasilisha majina na Waziri Mkuu ni Mjumbe wa Kamati kuu na jina lilipendekezwa na anapiga kampeni. Sasa nini kinakusumbua?? Mbona Chadema mmetengeneza orodha yenu na hakuna anayewauliza?

Mwisho niseme tu! Tayari mmeona uwezekano wa kushinda ni sawa na ngamia kuingia kwenye tundu la sindano mmeanza kutoka kwenye hoja mpo kwenye viroja! Mnahubiri kusimamia sheria leo mnataka Tume ipindishe sheria. Mlimuacha Lisu aropoke badala ya kunadi sera sasa jahazi linazama!! Bora mngemsikiliza mzee wangu Mhe. Membe!! JITAFAKARINI!! WATANZANIA HAWATAKI VURUGU!!! SANDUKU LA KURA LIACHWE LITAAMUA!!! DEMOKRASIA IACHWE ICHUKUE MKONDO WAKE!!!!
 
Safi sana waheshimiwa kwa kukwepa huu mtego, tusiruhusu TUME kupata kisingizio cha kufanya hujuma zaidi kwa mgombea wetu. Mwenyezi Mungu atatenda muujiza na hujuma zao hazitsaidia. Kule kwao maji yapo shingoni, Mheshimiwa TAL kaza buti, wale wameshalegea, WATAACHIA mapemaa!
 
Heee! Hii JF ya Mzalendo wa kweli Max Demelo!! Heeee!! kweli!! Ngoja tuone!! Mbona Magufuli anatukanwa humu sana tuu na watu hawafungiwi? Ngoja tukodoe macho!!
 
..wakati bado haujafika.

..wananchi wakichoshwa, cdm, act,ccm,... wote watawekwa pembeni.

..tatizo ni kwamba ccm hawaioni HATARI hiyo.
Demokrasia imekwama sio tu kwa chama tawala bali na vile vyama viranja vya upinzani.
Tukisubiri kuletewa demokrasia na hawa wachezaji butu tutachelewa kuchukuwa kombe.
Turudi kwanza kwenye drawing board ya demokrasia na katiba.
Tukimaliza hilo ndio tufanye Uchaguzi mkuu.
Vyama vya siasa kwa sasa sio muarobaini wa uchaguzi huru na haki ni maigizo tu.
CCM nayo ni kubwa mno kujisafisha na hilo ni tatizo kubwa kwani yeye kageuka kama bidhaa za Azam yupo kila pahala.
Mchango wa mgombea binafsi ni muhimu kwa kuwaengua vyama maslahi.
HIzo nyege za wapinzani kujitundika kwenye uchaguzi mkuu kila miaka mitano huku wakijua wanaabulia patupu, bila tume huru ni fedheha kwa umma wa Tanzania.
 
Tuambie mgombea wenu kwanini kila siku anaongea uongo na hamumkemei? Atoe ushahidi Wakurugenzi kuitwa Ikulu! Mbona hiyo hoja haijibiwi?
 
Alivyotepeta kwa tume ndo atakavyotepeta baada ya uchaguzi,la muhimu ni kutii sheria bila shuruti.
Lissu akiambiwa awehanasikia na anaelewa hawezi kushindana na dola.
 
Kuiitii hii amri batili na ya kifedhuli ya NEC CCM ni ujinga na ni sawa na kukubali mapigo yajayo
 
"Jifanye mjinga siku ipite," "funika kombe mwanaharamu apite"ni uamuzi wa hekima na mwiba mkali kwa ccm.
Mda huu chadema wautumie kuujulisha Ulimwengu wote taasisi zote za haki za binadamu na pia wasake ujuzi Malawi Zambia kenya congo Ghana Gambia wajue mbinu walizotumia kuondoa shetani Nchi mwao wazitumie kuondoa ushetani wa CCM
 
Bila mabeberu kuchukua hatua hii nchi itafika hatua kama Iddi Amini alivyokuwa Uganda. Ni bora mabebeberu wachukue hatua sasa maana tumechoka watu kuuawawa na kuteswa kwenye nchi yao
 
Haki haipatikani bali kwa ncha ya upanga.
Mkurugenziccm wa Tumeccm na polepole huwa hawatambui kuna maisha baada ya uchaguzi hawajui kuwa endapo malaika atazuia mbinu zao za hovyo hatimae chadema kuingia ikulu watakuwa na vya kujibu baadae, hawajitafakari kabla ya kutenda ushetani wao
 
Wakati mwingine ukishupaza shingo sana huwa linavunjika

NEC na kamati yao ile wanatafuta sababu ya kutoa adhabu kali zaidi na CHADEMA watafanya makosa makubwa kuingia huko mkenge. Ndio maana imebidi busara itawale zaidi na jazba ikae kando
Chadema mmekamatika, ninyi hamnaga busara kama mnajua mko sahihi. Mgombea anasema lake, mwenye chama anasema lake upuuzi mtupu. Hamjajipanga kushinda, na mjiandae kujiunga na wenzenu TLP.
 
Ni uamuzi wa busara sana. Walichokua wanakitafuta mabwana wale hawajakipata na hawatakipata
 
Wametangaza kushirikiana.

Namuona mahera na lafudhi yake akikandamiza maneno kupinga urafiki wa chadema na ACT-WAZALENDO na akihekelea urafiki wa UDP, TLP na CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…