CHADEMA tuwe makini, huku kuhama Chama kila wilaya kunakoendelea nadhani kuna mkono wa CCM

Very well said, wengine tulipigia kura Chadema na kuamini kwenye sera zake kwenye chaguzi zilizopita, ila kwa sasa kila anayekosoa au kuonyesha kwamba kuna mambo hayako sawa basi anaitwa kijani, inakwaza kwa kweli.

Nafikiri kukosa willingness ya kusikiliza constructive criticism, itacost chama sana. Na kama hii ipo mpaka ngazi za juu, basi kusiwe na mshtuko kwanini baadhi ya wanachama wanajiengua.
Ushauri upi? Wa kukubali ujinga wa CCM.
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Kama Lissu na Heche hawajahama chama no problem just take a drink and enjoy yourself!
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Wenye tamaa ya pesa wao waame tu ila chadema ni mbele Kwa mbele no reform no election 💯
 
Very well said, wengine tulipigia kura Chadema na kuamini kwenye sera zake kwenye chaguzi zilizopita, ila kwa sasa kila anayekosoa au kuonyesha kwamba kuna mambo hayako sawa basi anaitwa kijani, inakwaza kwa kweli.

Nafikiri kukosa willingness ya kusikiliza constructive criticism, itacost chama sana. Na kama hii ipo mpaka ngazi za juu, basi kusiwe na mshtuko kwanini baadhi ya wanachama wanajiengua.
Watanzania wanaweza kuwa wajinga ila mjinga naye anamacho na maskio.
 
Lissu anaingiaje kwenye mada hii.

Kila linalotokea kwenu CCM.... hii ni moja ya sign ya cowardness. Lini mtakubali na nyie mnafanya makosa ya kimkakati ndiyo maana mmekosa mvuto na wanachama wanawahama!!
Wanajua kwa thati adui wao siyo CCM Wala G55 ni kutapatapa tu.Adui wa CHADEMA CHAKAVU ni matusi,kejeli,dhihaka l,udikteta,hoja kinzani
 
Yaani Kila ukishindwa jambo lawama kwa CCM. ...

Ushindwe uchaguzi lawama kwa CCM.
Ushindwe kulea wanachama wako lawama kwa CCM.

Mnafanya CCM ionekane ni dude kuuuuubwa na kua nili taasisi kikubwa ambalo kwa utaalamu wa inteligensia linaizidi taasisi ya FBI na CIA kwa pamoja.

Mnafanya CCM ionekane Kama jini, zimwi flan ambalo hata mapadre na wachungaji wanaowasaidia hawawezi kuliombea likateteleka hata robo.
 
Yaani Kila ukishindwa jambo lawama kwa CCM. ...

Ushindwe uchaguzi lawama kwa CCM.
Ushindwe kulea wanachama wako lawama kwa CCM.

Mnafanya CCM ionekane ni dude kuibwa la taasisi ambayo inaizidi taasisi ya FBI na CIA kwa pamoja.

Mnafanya CCM ionekane Kama jini, zimwi flan ambalo hata mapadre na wachungaji wanaowasaidia hawawezi kuliombea likateteleka hata robo.
Dalili ya kuzidiwa kisisas hiyo.
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Wengi hamumuelewi mtoa mada.

Mtoa mada ana ill intent kwenye bandiko lake. Amejaribu kutengeneza taswira kuwa tatizo sio Wanachama wanaohama Bali tatizo ni Viongozi wapya wa CHADEMA. Mtoa mada ni miongoni mwa Anti-Lissu na Anti-Heche. Msomeni mabandiko yake yote hapa muone kama ana dhamiri njema na Uongozi wa Sasa wa CHADEMA.

Tukirejea kwenye mada, kwanza si kweli wanaohama ni kwa sababu ya Uongozi wa Sasa, Bali ni resentment waliyonayo Kwa aliyekuwa Kiongozi wanayemuunga mkono kuangushwa katika Uchaguzi. Wengine ni kinyongo Cha kuondolewa Ofisini for the likes of Salum Mwalimu, Kigaila au Mrema. Lakini wanasahau kila Uongozi wa Taasisi yoyote unapoingia so many times utafanya mabadiliko Kwa baadhi ya Watendaji ambao walikuwa kwenye Uongozi uliopita na pengine hawaku deliver. Busara ilikuwa Kwa Kigaila na Mrema kukubali wame serve Chama vya kutosha na Sasa ni muda wa wengine kukihudumia Chama, vinginevyo wanaonekana ni opportunists, wasaka vyeo na wasio na dhamiri ya dhati ya kuleta mabadiliko Kwa Watanzania.

Human nature inafeel sympathy na yeyote anayeonewa. Kwa sasa CHADEMA ya Lissu inaonewa sana na Serikali Kwa hiyo Hawa jamaa Kwa sasa kutoka na kupigania vyeo badala ya maslahi mapana ya Wananchi inawapotezea credibility kubwa sana mbele ya Jamii. Nina uhakika Jamii will always stick with CHADEMA rather than these golddiggers.
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Chakufanya ni kuangalia historia ya kila mmoja anyeondoka ili mfanye tathmini kwa kuzingatia yafuatayo:-
a) Ni mwenzetu tangu lini?
b) Kwanini ameondoka?
c) Je, ni mamluki?
d) Kama ni mamluki kwanini hatukujua mapema? Mfano. Kama ni mamluki inamaana Mrema, Mwalimu, Kigaila, Grace Kihwelu walikuwa mamluki kipindi chote tukiwa nao. Je, Hawa waliopo akina Lissu, Heche, Mnyika na Amani Golugwa sio mamluki au tunasubiri waondoke ndio tuwaite mamluki?
e) Je, kama viongozi wenu wa Chadema na wanachama ni rahisi kurubuniwa, kama chama mko salama?

Mkiyatafakari hata kwa makini chama chenu kitasimama, ila msimuamini kabisa John Heche!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
CHADEMA nadhani kuna sehemu akili hazijawakaa sawa. Kila kitu kwenu lawama CCM. Lini mtajitathmini?

Nyie Miungu watu hamwezi kufanya makosa chamani!! Duh
Kataa ila yote yanayotokea kwa chadema ni matokeo ya ccm, wananchi na viongozi wa chadema kutekwa wahusika wa kwanza ni ccm, viongozi kuhama ni ccm ndio wapangaji wa hayo. Unafikiri huko ccm hakuna watu wanaosema hayo maovu wanayoyafanya.
 
ukirejea kwenye mada, kwanza si kweli wanaohama ni kwa sababu ya Uongozi wa Sasa, Bali ni resentment waliyonayo Kwa aliyekuwa Kiongozi wanayemuunga mkono kuangushwa katika Uchaguzi.
Uongozi ullopo umeshindwa kuunganisha makundi na wameingia kwenye kufanya kosa kubwa la kutokutafuta suluhisho kwa malalamiko ya viongozi wa zamani ikiwa ni pamoja na utenganifu unaotokana na kurushiana maneno. LIssu alipaswa kuleta upatanisho kwanza ndani ya chama.. Hivyo baadhi ya viongozi ndani ya chama wanamuona kama dikteta na wanaona hakuna nafasi ya kusikilizwa na hivyo kuamua kutimua mbio. Tatizo ni uongozi mpya.
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Kabla ya kuwanyooshea vidole CCM, CDM inapaswa kujitafakari yenyewe na kushughulikia malalamiko ya wanaohama. Kuna waliojiunga CDM 1992 halafu leo wanahama! Wengine wanakaribia kulia.

Mimi ningewashauri wajitenge hadharani na vijana wanaotukana kwa kujifanya kuwa wao ni Team Lissu. Wazuie hizi fukuza fukuza zinazofanywa katika matawi. Hii itaweza kufanya wengine wenye mpango wa kuhama wasite. Haupati uzoefu darasani au kwa kununua. Hawa wanaondoka wana uzoefu mkubwa ambao hao vijana watu wa diaspora itabidi wapitie learning curve

Amandla...
 
Uongozi ullopo umeshindwa kuunganisha makundi na wameingia kwenye kufanya kosa kubwa la kutokutafuta suluhisho kwa malalamiko ya viongozi wa zamani ikiwa ni pamoja na utenganifu unaotokana na kurushiana maneno. LIssu alipaswa kuleta upatanisho kwanza ndani ya chama.. Hivyo baadhi ya viongozi ndani ya chama wanamuona kama dikteta na wanaona hakuna nafasi ya kusikilizwa na hivyo kuamua kutimua mbio. Tatizo ni uongozi mpya.
Tafakari kama kweli Viongozi wa zamani Wana dhamiri njema. Imagine mtu kama John Mrema alianza kuushambulia Uongozi ukiwa na siku Moja tuu. So unatarajia hao kina Lissu wafanye reconciliation saa ngapi wakati hata hawajakabidhiwa Ofisi wanashambuliwa. Kwanza hiyo peke yake ni disrespect kubwa sana Kwa Viongozi. John Mrema Kwa matendo yake alistahili kugukuzwa mara moja. Yaani utende makosa ya kinidhamu Kwa kuchokoza watu halafu hapohapo unawataka wawasamehe. Kwa nn John Mrema and co. Kabla ya kutoa kibanzi kwenye macho ya Lissu &Heche wasingetoa maboriti Yao ya uchokozi?

Hebu tujifunze CCM kama hizi insubordination zinavumilika. CCM hawana hata muda wa kumvumilia mtovu wa nidhamu ila mnamtaka Lissu awavumilie wanaoleta utovu.
 
Na CDM mmewaiga kwa kufanya mtu kuwa G55 kuwa kama kosa la jinai.

Amandla..
Ni kosa ndiyo Kwa sababu hiyo ni kwenda kinyume Cha Maamuzi halali ya Chama. Kamati Kuu ya Chama ilishaamua hakuna mabadiliko basi hakuna kushiriki Uchaguzi. Inakuwaje wewe uliyeshiriki kwenye Kamati Kuu ukakubaliana na maazimio ya Chama, ukatoka nje na kiyatangaza na kuyawekea mkazo , miezi kadhaa baadaye baada ya kuondolewa Ofisini unayapinga maamuzi yaleyale uliyoyashiriki?

Wewe Fundi Mchundo ni mkongwe hapa JF, maana hata hiyo signature Amandla ilitumiwa sana na Chama baada ya zile vurugu walizopitia CHADEMA around 2011 na 12, so ulikuwepo enzi zile tukim dissect Zitto Kwa kwenda Kinyume Cha Maamuzi ya Chama, ulikuwepo tukimponda Dr Slaa Kwa kujitoa CHADEMA akipinga maamuzi halali ya Chama. Leo unawezaje kuwa na audacity ya kuwatetea wakosefu walewale wa type ya Zitto, Kitila, Slaa? Unless upo biased na Uongozi uliopita na una mtazamo hasi na Viongozi wapya but not to the Party Principles.
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
ni lini chadema ilikua makini gentleman zaidi ya viongozi wake waaandamizi kitaifa kuropoka ropoka tu bila mpangilio?

Nadhani hayo yanayotokea ni matokeo ya athari za uropokaji, na hakuna haja ya kusingizia mamluki sijui kutoka wapi hali ya kua wanaojiengua ni wanachadema wanaojulikana na wanaojiengua mchana kweupe.

hata hivyo,
n Lini vibaka na matepeli wa kisiasa kama heche au lisu wakawa makini gentleman?🐒
 
Ni kosa ndiyo Kwa sababu hiyo ni kwenda kinyume Cha Maamuzi halali ya Chama. Kamati Kuu ya Chama ilishaamua hakuna mabadiliko basi hakuna kushiriki Uchaguzi. Inakuwaje wewe uliyeshiriki kwenye Kamati Kuu ukakubaliana na maazimio ya Chama, ukatoka nje na kiyatangaza na kuyawekea mkazo , miezi kadhaa baadaye baada ya kuondolewa Ofisini unayapinga maamuzi yaleyale uliyoyashiriki?

Wewe Fundi Mchundo ni mkongwe hapa JF, maana hata hiyo signature Amandla ilitumiwa sana na Chama baada ya zile vurugu walizopitia CHADEMA around 2011 na 12, so ulikuwepo enzi zile tukim dissect Zitto Kwa kwenda Kinyume Cha Maamuzi ya Chama, ulikuwepo tukimponda Dr Slaa Kwa kujitoa CHADEMA akipinga maamuzi halali ya Chama. Leo unawezaje kuwa na audacity ya kuwatetea wakosefu walewale wa type ya Zitto, Kitila, Slaa? Unless upo biased na Uongozi uliopita na una mtazamo hasi na Viongozi wapya but not to the Party Principles.
Amandla Awethu/Ngawethu ni battle cry ya ANC na sio ya Chadema. Hizo unazoita Principles zingetumika, Lissu asingekuwa leo Mwenyekiti maana alipinga waziwazi uamuzi halali wa chama chake kuingia katika maridhiano. Chama ambacho hakiruhusu mawazo mbadala ni ama kiwe cha dikteta au ki sinyae kwa kukosa mbinu mpya. Waliongoza jitihada za kuwaondoa Zitto na Kitila ni hao hao unaowatetea leo. Mimi toka mwanzo nilipinga maana niliona ina set precedence mbaya. Na kweli ikawa hivyo.

Shida yangu na Slaa ilikuwa ni yeye kutoa tuhuma nzito bila uthibitisho wowote dhidi ya chama chake.

Tatizo kubwa la Chadema ni kuwa wameanza kuamini wimbo walizokuwa wanajiimbia. Kuwa wao wamekamilika na wanaweza kuitoa CCM madarakani bila kushirikiana na chama kingine. Wamefikia hatua ya kuwaona watu ambao wamekifikisha chama kilipo wanatukanwa matusi ya nguoni na watu ambao walikuwa hata hawajaziliwa wakati chama kina undwa.

Chadema kimekuwa kama CCM mpya iliyojivika kanzu ya upinzani. Hawa wakiingia madarakani hawatakuwa tofauti na CCM. Wazo hilo ndilo linalotutisha wengine. Chawa wa CDM hana tofauti ya yule wa CCM.

Amandla...
NGAWETU...
 
Back
Top Bottom