CHADEMA tuwe makini, huku kuhama Chama kila wilaya kunakoendelea nadhani kuna mkono wa CCM

CHADEMA tuwe makini, huku kuhama Chama kila wilaya kunakoendelea nadhani kuna mkono wa CCM

Wanao sababisha hayo yote ni UBAGUZI unaofanywa na Lissu na Heche dhidi ya wafuasi wa Mhe. MBOWE sasa ngoja Mwamba awashikishe adabu.
na pia dua zao ni kuwa ikiwezekana Lissu aishie hukohuko jela asitoke.
 
Cdm haipiganii kuwa chama kikuu cha upinzani boss.
Vyama vyote vinasema kuwa vinapiganiq kuchukua dola, hata ACT-WAZALENDO wanasema hivyo. Lakini ki ukweli katika mazingira ya sasa kinachopiganiwa ni kuwa chama kikuu cha upinzani.
Kama siasa za miaka mitano kuwa nje ya uchaguzi ni mingi, tusingeona ACT wakiporwa uchaguzi hapo Znz, maana CUF haikushiriki uchaguzi wa kihuni wa marudio 2016.
Haswa. Na kutokana na experience yao ndio maana hawataki kusikia neno kususia uchaguzi. Walipoteza mengi wakiwa nje ya serikali. Tofauti na CDM, ACT-WAZALENDO wana base committed Zanzibar ambayo hata iwe vipi watakipigia kura chama cha Maalim. Ndio maana CCM inabidi ifanye juhudi za ziada ili itangazwe kuwa mshindi.
Kama hivyo vyama vingine ni mapandikizi ya ccm, wale mnaosema cdm kina ubinfasi hawataki kuungana vyama vya upinzani mnamaanisha nini?
Sijasema vyama vingine vyote ni mapandikizi. Naamini ACT-WAZALENDO sio pandikizi na ni mpinzani wa kweli wa CCM. CDM itakuwa katika nafasi nzuri zaidi kama itaweza kuunganisha nguvu na ACT-WAZALENDO lakini hilo linakuwa ngumu baada ya kila kukicha kuwaita CCM B. NCCR Mageuzi na CUF bado wanaamini kuwa Ukawa ulikifaidia zaidi CDM kuliko wengine. Na wao wametukanwa sana. Katika mazungumzo karibu yote ya kisiasa CDM imekuwa ikidai ipewe upendeleo tofauti na vyama vingine.

Kwa maoni yangu upinzani uliogawanyikq utakuwa na kazi ngumu sana kuitoa CCM madarakani.

Amandla...
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Usiogope kipindi ambacho ,chadema ingekufa ilikua kile kipindi cha mwendazake , kipindi cha kuunga juhudi ,chadema ni Dude kubwa ,kwa sasa wanaokiunga chama ichi mkono ni mara milioni 5 ya wanaohama, hacha magugu yajitenge na Ngano, hili ni jambo zuri sana
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
Chadema ina wananchi...
Kuwa na moyo mkuu,hii ni Agenda ya Mungu!
 
CHADEMA nadhani kuna sehemu akili hazijawakaa sawa. Kila kitu kwenu lawama CCM. Lini mtajitathmini?

Nyie Miungu watu hamwezi kufanya makosa chamani!! Duh
Na ww uchawa umekuzidi makosa gani yamefanywa na uongozi wa juu zaid ya kusimamia kauli mbiu iliyopitishwa na kamati kuu
 
Wengi hamumuelewi mtoa mada.

Mtoa mada ana ill intent kwenye bandiko lake. Amejaribu kutengeneza taswira kuwa tatizo sio Wanachama wanaohama Bali tatizo ni Viongozi wapya wa CHADEMA. Mtoa mada ni miongoni mwa Anti-Lissu na Anti-Heche. Msomeni mabandiko yake yote hapa muone kama ana dhamiri njema na Uongozi wa Sasa wa CHADEMA.

Tukirejea kwenye mada, kwanza si kweli wanaohama ni kwa sababu ya Uongozi wa Sasa, Bali ni resentment waliyonayo Kwa aliyekuwa Kiongozi wanayemuunga mkono kuangushwa katika Uchaguzi. Wengine ni kinyongo Cha kuondolewa Ofisini for the likes of Salum Mwalimu, Kigaila au Mrema. Lakini wanasahau kila Uongozi wa Taasisi yoyote unapoingia so many times utafanya mabadiliko Kwa baadhi ya Watendaji ambao walikuwa kwenye Uongozi uliopita na pengine hawaku deliver. Busara ilikuwa Kwa Kigaila na Mrema kukubali wame serve Chama vya kutosha na Sasa ni muda wa wengine kukihudumia Chama, vinginevyo wanaonekana ni opportunists, wasaka vyeo na wasio na dhamiri ya dhati ya kuleta mabadiliko Kwa Watanzania.

Human nature inafeel sympathy na yeyote anayeonewa. Kwa sasa CHADEMA ya Lissu inaonewa sana na Serikali Kwa hiyo Hawa jamaa Kwa sasa kutoka na kupigania vyeo badala ya maslahi mapana ya Wananchi inawapotezea credibility kubwa sana mbele ya Jamii. Nina uhakika Jamii will always stick with CHADEMA rather than these golddiggers.
Correct 💯
 
Hakuna nyakati ngumu kwa chama kupanga safu bora ya mashambulizi kama nyakati za mabadiliko ya uongozi wa juu wa chama .

Hii ondoka ondoka inayotokea sasa nimtaji muhimu sana kwa musktakabali bora wa kesho ya Chadema .

Natamani Chadema iendelee kutikiswa ili ifanikiwe kuondoa uchafu wote then ianze upya .

Msisahau kwasasa kasi ya uungwaji mkono na wanainji imeongezeka mara 80% zaidi

Top Cream ya chama iko nondo sana.
Hoja ya maana sana.

Ukweli ni kuwa baada ya CHADEMA kuwa upinzani wa nguvu muda mrefu sana, dola (CCM) imekuwa ikitumia mikakati kadhaa kukisambaratisha chama tokea ndani. Na njia kuu ni kutumia Hazina ya Taifa kurubuni makada wa CHADEMA wanaoonekana machachari sana. Mwenyekiti wa CCM anasimamia hela yote ya umma nchini na, anao uwezo wa kuitumia anavyotaka bila kuhojiwa na mtu yeyote. (Mushekli mkubwa wa katiba ya sasa). Hivyo, anaweza kutoa "bei" yoyote kumweka sawa yoyote wanayetaka awatii. Mbishi kupitiliza anashushiwa rungu la dola. Wapinzani wa kweli wanakutana na hali hiyo muda wote.

Katika muktadha huo lazima watakuwepo viongozi na makada kadhaa wa CHADEMA wanaoona FURSA kubwa kusaliti mwenendo wa Chama. Na bila shaka wanazidi kudhihirika kila wakati. Sasa ni dhahiri kuwa suala la Covid-19 lilikuwa na mkono wa viongozi wa CHADEMA (uliojificha). Na mengime mengi tu. Haya si ya kufumbia macho kwa chama chenye wapambanaji wanaokutana na adha za kutekwa, kutiwa vilema, kuuawa na kufilisiwa mara kwa mara.

Chama cha mapambano dhidi ya dola kandamizi lazima pia kipambane kikamilifu na wahujumu wa ndani wanaozidiwa tamaa na kugeuka wenzao bila kujali masahibu yanayowakuta. Utaendaje kwenye uchaguzi baada ya matukio ya 2019, 2020, na 2024 kwa mfumo uleule? Unataka kutikisa kiberiti?

ANC walivuma kwa ukatili wa kuvisha wasaliti matairi na kuwachoma moto kwa mambo ya aina hii. CHADEMA haiwezi kabisa kufika huko. LAKINI lazima wahujumu waachwe waondoke au waondolewe. Kama ni maelewano basi iwe na mtu mmoja mmoja atakayekiri kuwa serious na ajenda ya chama. Sio janja janja ya kutikisa kiberiti.
 
Gentleman,
hapo sio suala la impacts,
La muhimu zaidi ni kila moja kuheshimu uhuru na haki za kikatiba bila wengine kuwakasirikia.

ni muhimu kuheshimu hiyo ni muhimu zaidi 🐒

Sawa:

Screenshot_20250306-183123_1.jpg


Wahama chadema.
 
Vyama vyote vinasema kuwa vinapiganiq kuchukua dola, hata ACT-WAZALENDO wanasema hivyo. Lakini ki ukweli katika mazingira ya sasa kinachopiganiwa ni kuwa chama kikuu cha upinzani.

Haswa. Na kutokana na experience yao ndio maana hawataki kusikia neno kususia uchaguzi. Walipoteza mengi wakiwa nje ya serikali. Tofauti na CDM, ACT-WAZALENDO wana base committed Zanzibar ambayo hata iwe vipi watakipigia kura chama cha Maalim. Ndio maana CCM inabidi ifanye juhudi za ziada ili itangazwe kuwa mshindi.

Sijasema vyama vingine vyote ni mapandikizi. Naamini ACT-WAZALENDO sio pandikizi na ni mpinzani wa kweli wa CCM. CDM itakuwa katika nafasi nzuri zaidi kama itaweza kuunganisha nguvu na ACT-WAZALENDO lakini hilo linakuwa ngumu baada ya kila kukicha kuwaita CCM B. NCCR Mageuzi na CUF bado wanaamini kuwa Ukawa ulikifaidia zaidi CDM kuliko wengine. Na wao wametukanwa sana. Katika mazungumzo karibu yote ya kisiasa CDM imekuwa ikidai ipewe upendeleo tofauti na vyama vingine.
k
Kwa maoni yangu upinzani uliogawanyikq utakuwa na kazi ngumu sana kuitoa CCM madarakani.

Amandla...
ACT ya kweli iko Znz sio huku bara. Halafu huhitaji kura hata moja toka zanzibar kuwa rais wa nchi hii. NCCR na CUF na zilifaidika na umoja wa cdm na sio kinyume cha hapo. Kama vipi waungane hao NCCR na CUF sasa kimoja kiwe na wingi wa kura ili wawe vyama vikuu vya upinzani. Ama umesahau kuwa Magufuli pia aliwatapeli Lipumba na Mbatia uchaguzi wa 2020 atawapa viti ili wawe vyama vikuu vya upinzani, na hakuna walichopata? CCM haipo madarakani kwakuwa vyama vya upinzani havina umoja, bali tume hii ya uchaguzi, sheria na katiba ndio siri ya wao kukaa madarakani hadi leo. Cdm imeamua kujitoa muhanga wa hali hii. Iwe itakavyokuwa, msimamo wa sasa wa cdm wa kutosaini sheria za kihuni lazima utapelekea mageuzi makubwa kwenye katiba na sheria za uchaguzi, hata kama sio kwenye uchaguzi huu. Lakini cdm wangekubali kusaini sheria za kihuni uhuni ungeendelea kwa muda mrefu.
 
Hoja ya maana sana.

Ukweli ni kuwa baada ya CHADEMA kuwa upinzani wa nguvu muda mrefu sana, dola (CCM) imekuwa ikitumia mikakati kadhaa kukisambaratisha chama tokea ndani. Na njia kuu ni kutumia Hazina ya Taifa kurubuni makada wa CHADEMA wanaoonekana machachari sana. Mwenyekiti wa CCM anasimamia hela yote ya umma nchini na, anao uwezo wa kuitumia anavyotaka bila kuhojiwa na mtu yeyote. (Mushekli mkubwa wa katiba ya sasa). Hivyo, anaweza kutoa "bei" yoyote kumweka sawa yoyote wanayetaka awatii. Mbishi kupitiliza anashushiwa rungu la dola. Wapinzani wa kweli wanakutana na hali hiyo muda wote.

Katika muktadha huo lazima watakuwepo viongozi na makada kadhaa wa CHADEMA wanaoona FURSA kubwa kusaliti mwenendo wa Chama. Na bila shaka wanazidi kudhihirika kila wakati. Sasa ni dhahiri kuwa suala la Covid-19 lilikuwa na mkono wa viongozi wa CHADEMA (uliojificha). Na mengime mengi tu. Haya si ya kufumbia macho kwa chama chenye wapambanaji wanaokutana na adha za kutekwa, kutiwa vilema, kuuawa na kufilisiwa mara kwa mara.

Chama cha mapambano dhidi ya dola kandamizi lazima pia kipambane kikamilifu na wahujumu wa ndani wanaozidiwa tamaa na kugeuka wenzao bila kujali masahibu yanayowakuta. Utaendaje kwenye uchaguzi baada ya matukio ya 2019, 2020, na 2024 kwa mfumo uleule? Unataka kutikisa kiberiti?

ANC walivuma kwa ukatili wa kuvisha wasaliti matairi na kuwachoma moto kwa mambo ya aina hii. CHADEMA haiwezi kabisa kufika huko. LAKINI lazima wahujumu waachwe waondoke au waondolewe. Kama ni maelewano basi iwe na mtu mmoja mmoja atakayekiri kuwa serious na ajenda ya chama. Sio janja janja ya kutikisa kiberiti.
Maelezo mujarabu👏
 
Muda ni mwalimu mzuri. Mwakani sio mbali. Tutaona jinsi CDM ambayo haina uwakilishi Bungeni, haina ruzuku n.k. itakavyoweza kuendelea kujitoa mhanga. Humo humo ndani ya CDM ya sasa kuna wengi wanaoamini kuwa wakina G55 walifaidika sana na chama na sasa ni zamu yao ya kula. Commitment yao itathibitika pala ambapo chakula kitakuwa kimepungua sana. Na itajaribiwa zaidi kama Lissu ataanza safari za Ubelgiji na Lema za Canada.

Sisi wengine yetu ni macho.

Amandla...
 
Kila dakika chache nasoma habari za watu kuhama CHADEMA, hili jambo linafikirisha sana. Sidhani kama ni suala la ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA tu.

Yawezekana kuna mamluki wa CCM wamefanikiwa kupenya kwenye safu za juu za uongozi wa CHADEMA na wanafanya kwa makusudi makosa ya ubaguzi kwa lengo mahsusi la kuuwa Chama.

Tufikirie mapema jambo hili kabla ya kuja kushangaa ilikuwa vipi CHADEMA ikaharibiwa kirahisi hivyo.
CHADEMA haiwezi kufa, ni baraka ilioje kwa hao mamluki kuhama. Ni bahati ambayo CHADMEA siku moja wataamini ni muujiza wa Mungu umetenda yote haya
 
Imekataa kusaini kanuni za uchaguzi zenye upendeleo. Na hapo tume ikasema cdm hairuhusiwi kushiriki uchaguzi kwakuwa haijasaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Unataka ufafanuzi zaidi?
Ila CDM si tumekataa kusaini kwa sababu hatutaki kushiriki uchaguzi bila reform?

Sasa ukisema tumezuiwa wakati wenyewe kwa maamuzi ya chama hatukutaka kabisa kuwa sehemu ya uchaguzi bila mabadiliko nafikiri unakua unakosea.
 
Back
Top Bottom