Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Tukubali tu kwamba kwa hali ilivyo sasa lolote linaweza kuzungumzwa kwa lengo la kutuliza/kuondoa athari/hasara itayatokana na kauli za Dk. SLAA jana....Mengi yatazungumzwa lakini ukweli wanaujua Slaa, Mbowe, Gwajima na Tundu Lissu
Nguruvi, ukisoma vizuri kuna kitu ambacho hakijasemwa vizuri. Mazungumzo na Lowassa hayakuanza baada ya jina lake kukatwa. Gwajima alifanya kile alichotakiw akufanya na mhusika mkuu. Walijua kizuizi kikubwa kwa Lowassa kuja CDM ni Slaa, kwanza sababu ya nafasi yake (alikuwa tayari ni mgombea wao) na pili sababu ya msimamo wake ulio tofauti sana na Lowassa. Si unaona wakati mwingine hata ndani ya familia kuna mambo fulani mzazi anajua ili lifanyike lazima mzazi mwenzie ndio atoe "Ok". Hivyo, mtoto ataambiwa nenda kwa "babaako" au "mamaako" si kwamba yule mzazi mwngine hajaimbishwa bado!
Kuna watu walishaimbishwa kwa muda na ulipofika wakati akatumwa mshenga... "nenda kwa Slaa"... the rest is history.
Mzazi anayeulizwa anaweza kusema "Mamaako anajua" halafu mtoto anasema "ntaenda kumuuomba ila ukikubali najua hatakataa..." kumbe dili lilishachongwa muda!! Angalia simulizi hili kwa karibu utaona mchezo huu...
Hili jukwaa la great thinkers nalo mmeligeuza jukwaa la kampeni na propaganda.
Swala la Slaa kumkaribisha Lowassa Chadema sio big deal.
Tatizo ni kumsimamisha agombee urais.
Hata kule CCM walipomkata Lowassa hawakumfuta uanachama na hata angegombea ubunge wasingemkata kama ilivyo 1995 ambapo alionekana ana upungufu wa kimaadili kwa nafasi ya urais lakini akapitishwa kugombea ubunge.
Kwahiyo sioni tatizo Slaa kumkaribisha Lowassa kama mwanachama wa kawaida kuongeza nguvu kwenye timu ya kampeni.
Kama vyama vimekubali kuungana ingawa vinatofautiana itikadi, hakuna tatizo kumkaribisha mtu mmoja. Tatizo ni mtu huyo mmoja mgeni anapopewa nafasi ya kuamua hatma ya chama.
Alinda , kumbe ni kuanzia May wapo katika maongezi. Naunganisha na ile kauli ya 'amekatwa Dodoma, tunafanyaje'
Maswali yako yanahitaji majibu kwakweli. Na majibu yapo katika ''maongezi'' kati ya May-July
@Ngwamapalala kuna hoja hapo, unaweza kutusaidia?
Pili, Alinda aliuliza haya
Je, Dr alimkaribisha Lowassa kama nani? Mgombea,mwanachama, au mtu atakayesaidia kampeni?
Mwalimu akaulizahivi Gwajima alipompigia simu Dr Slaa na kumwambia, Dodoma wamemkatatufanyeje ? Ina maana gan?
Kuna alihojia kuwa nani hasa alimwalika Lowassa kati ya pande mbili?
Sidhani kama hili ni swali sahihi; kama nijibu nadhani alilitoa mwenyewe na linaeleweka. Lakini kwamba "alimkaribisha" inadhania mambo mengi sana.
Rejea majibu yake jinsi gani Lowassa aliomba kuingia lakini pia usisahau kuwa ushahidi mkubwa uliopo ni kuwa tayari Lowassa alishaanza dili ya kutaka kuingia CDM mapema sana kabla ya kukatwa CCM na mtu mhusika mkubwa hakuwa Slaa katika hili. Kimsingi hata kile kinachoitwa "kupitishwa" kwa Slaa kugombea ilikuwa ni geresha tu kwani kuna waliokuwa wanajua mapema dili wanalotaka kuchezewa lichezwe vipi. Slaa alikuwa ni chaguo lao la pili; chaguo lao la kwanza tunalijua sasa.
Nadhani hapa watu pia wanamiss ukweli mwingine; kama CDM walimpitisha Slaa mapema hivyo awe mgombea wao ni kwanini? Waliamini kuwa anawafaa kweli kweli au walifanya kama hadaa? Siyo kwamba walimpitisha kwa sababu waliamini anaweza kuwakilisha maslahi ya chama na harakati zao kwenye Uchaguzi Mkuu? Sasa watu wale wale ndani ya miezi michache wanabadili 360 halafu walitaka Slaa asimame na kusema ndio tu? Ukweli wangemkubalia pale pale aliporesign on principle.
Alinda;
Pesa na madaraka yanafanya watu wasalitiane. Nimemsikiliza Dr vizuri. Na kwa maoni yangu binafsi, watu wamezidiana. Hili sio swala la kumleta Lowassa ndani ya CDM. Kuna watu wamefaidika na siku zinavyokwenda tutakuja kuyasikia zaidi.
Nguruvi, ukisoma vizuri kuna kitu ambacho hakijasemwa vizuri. Mazungumzo na Lowassa hayakuanza baada ya jina lake kukatwa. Gwajima alifanya kile alichotakiw akufanya na mhusika mkuu. Walijua kizuizi kikubwa kwa Lowassa kuja CDM ni Slaa, kwanza sababu ya nafasi yake (alikuwa tayari ni mgombea wao) na pili sababu ya msimamo wake ulio tofauti sana na Lowassa. Si unaona wakati mwingine hata ndani ya familia kuna mambo fulani mzazi anajua ili lifanyike lazima mzazi mwenzie ndio atoe "Ok". Hivyo, mtoto ataambiwa nenda kwa "babaako" au "mamaako" si kwamba yule mzazi mwngine hajaimbishwa bado!
Kuna watu walishaimbishwa kwa muda na ulipofika wakati akatumwa mshenga... "nenda kwa Slaa"... the rest is history.
Mzazi anayeulizwa anaweza kusema "Mamaako anajua" halafu mtoto anasema "ntaenda kumuuomba ila ukikubali najua hatakataa..." kumbe dili lilishachongwa muda!! Angalia simulizi hili kwa karibu utaona mchezo huu...
'UZA UWAPE MASIKINI UNIFUATE' Ushahidi wa Richmond EL anaujua 100%, angeusema. Ndio u-asset wake kwa CDM, laa ni upuuzi.
Alomleta Lowassa Chadema siwezi kumjua zaidi ya mhusika mwenyewe isipokuwa nasema hawezi kuwa Dr.Slaa kwa maelezo ya Tundu Lissu kwa sababu katika maelezo yake uongo umejitenga wazi kabisa..
1. Mimi nilipokuwa Bongo mwezi November na December mwaka jana nilipata habari hizo sikutaka kuzizungumza hapa kijiweni kwa sababu zilikuwa tuhuma tu. Miezi ilivyopita nikasikia habari mpya kuwa ataenda ACT sio Chadema na ndiye mfadhili wa safari zao.. Nikayaacha kama yalivyo nikisubiri UKWELI ni upi.
2. Hapa hapa JF ilikuwepo mjadala kuhusu Lowassa kuhamia Chadema toka mwaka 2011 kama hatachaguliwa CCM tukazipuuza kwahiyo haikuwa habari mpya. Lissu anaposema kwamba ni Dr.Slaa aliyemleta Lowassa ni uongo kwa sababu nyingi tu za msingi na nimezisema hapo nyuma. a) Haiwezekani mtu alochaguliwa kugombea Urais na kamati kuu ama baraza kuu ajichukulie maamuzi binafsi ya kumtafuta mtu mwingine nje ya chama aje kugombea badala yake hali yeye kisha pitishwa! - Haiwezekani.. Hata wewe leo hii ukichaguliwa kuwa mbunge wa Ilala na umepitishwa huwezi tena kufanya maajabu aloyasema Tundu Lissu na zaidi ya hapo Dr.Slaa na Lowassa ni Mbwa na Chatu! Ningekubali tu kama Tundu Lissu angesema Dr.Slaa amechukia baada ya Kamati ya Chadema kumchagua, lakini ujio wa Lowassa tulimwambia akae pembeni Lowassa atasimama badala yake..
3. Muda aloutaja Tundu Lissu kwamba Dr.Slaa ndio alituma ujumbe, wakati huo Lowassa alikuwa bado hajatoswa CCM, Lowassa alikuwa tumaini la wajumbe wengi wa CCM kuliko mgombea mwingine yeyote na hata yeye mwenyewe alijua atashinda na hakuna wa kumzuia, leo iweje akubali mazungumzo ya kuhamia Chadema hata kabla ya uchaguzi wa ndani wa CCM? Kisha kwa sisi tunaomjua Lowassa huyu mtu ana guts za ajabu, anajiamini kupita kiasi na kwamba anachokifikiria ni lazima kipatikane kwa nguvu zozote zile. Kutoswa CCM ilikuwa pigo kubwa sana ambalo hakulitegemea kabisa. Lowassa alikataa ushauri wa wapambe wake ndani ya CCM kuweka Plan B ikiwa ataenguliwa. Na ndivyo alivyoingia UKAWA akaweka masharti kaa atajiunga Chadema awe mgombea na pasipo ushindani. hili ndio mimi nadhani lilowaondoa Dr.Slaa na Lipuymba UKAWA..
Ni hayo tu... siwezi kwenda taratibu mahala ambapo mnataka kunibana katika jambo ambalo hata nyie wenyewe hamjui nani alomleta Lowassa isipokuwa kwa kuwasoma waongo, wafitini wenye kuwa na kila sababu kila jambo bana wanapolifanya. Uongozi wa kamati kuu Chadema wamekuwa na maamuzi mabaya sana na haya yote yanatokana roho mbaya za vaadhi ya viongozi wenyewe.
Ukiangalia tu historia yake ya kutoa vibaasha sidhani kama anawapa viongozi kwa sababu ya kura moja zao, bali anajuwa wanamakundi ya wafuasi wenye uwezo wa kumpa kura nyingi tu. Kwenye ethics wanasema uwezi defy nature ya kitu viumbe vinatabia ya kurudia mambo yaleyale given the challenge or circumstances."Churchill: "Madam, would you sleep with me for five million pounds?" Socialite: "My goodness, Mr. Churchill... Well, I suppose... we would have to discuss terms, of course... "
Churchill: "Would you sleep with me for five pounds?"
Socialite: "Mr. Churchill, what kind of woman do you think I am?!"
Churchill: "Madam, we've already established that. Now we are haggling about the price"
Sikumbuki quote hasa aliyosema Dr. Slaa, lakini alimuita Lowassa Shetani or something to that nature na akihusisha na Upadiri na Ukristo wake.
Wakristo tuna kauli tunasema (tena kinafiki wakati tunajiandaa kupokea Sakramenti, lakini tuna mambo kibao kichwani na moyoni kutokana na uanadamu wetu) Namkataa Shetani na mambo yake yote na kazi zake zote....
Dr. Slaa kama alikubali kumkaribisha Lowassa hata kwenda kuongea na Mwenyekiti na wenzake, ina maana alikuwa anamkaribisha Shetani (si amemuita shetani?)
Je leo Dr. Slaa anapoafikiana na Mwakyembe na Sitta kwenye kauli zao dhidi ya Lowassa, ina maana hata Lowassa angekiri vipi au kusema Richmond (let say ni ya Rostum, Brigaia wa Oman au Kikwete), bado yeye asingeamini wala kusamehe ungamo la Lowassa?
Kwa maoni yangu binafsi, ni heri kauli ya Dr. Slaa ingesema nimejiuzulu siasa, sikubaliana na wenzangu kwa maamuzi ya kumfanya Lowassa kuwa mgombea pamoja na kuwa nilishiriki kumkaribisha. Ngefuata Lipumba way na kusema nafsi ilimsuta na angemalizia kuwaomba watu waheshimu maisha yake ya nyumbani na kuacha kumsimanaga yeye na mpenzi wake.
Jibu la swali kamba Dr alimkaribisha Lowassa kama naninadhani linapatikana kutoka kwa maelezo ya Slaa mwenyewe kasema "kiongozi ambaye anaenda kuwa raisi wa nchil azima awe na wafuasi nyuma yake" akaendelea kusema… "anakuja peke yake au anawafuasi wa kutosha nyuma yake? Na wafuasi hao wa aina gani?"@Ng'wamapalala kuna hoja hapo,unaweza kutusaidia?
Pili, Alindaaliuliza haya
Je, Dr alimkaribisha Lowassa kama nani? Mgombea,mwanachama, au mtuatakayesaidia kampeni?
Mwalimuakaulizahivi ' Gwajima alipompigia simu Dr Slaa na kumwambia, Dodomawamemkatatufanyeje ? Ina maana gan?
Kuna alihojia kuwa nani hasa alimwalika Lowassa kati ya pande mbili?
''Amekatwa Dodoma tunafanye? Nikambiwa subiri niwasiliane na mwenyekiti''na ukichukua maelezo ya Lissu yanaleta mantiki ya hii kauli "jamaa kakatwe" maana kama ingekuwa gafla kwa vyovyote vile Dr. Slaa angemuuliza Gwajima "ni jamaa gani unayemzungumzia? au na unaniambia ili nifanyeje? (yaani walao tungesikia kauli inayoonshea mshangao au upya wa jambo hili)