Bibie hiyo ni taarifa tu ilitolewa lakini ukweli ni kwamba nafasi ya rais haikuwa hivyo. hapakuwepo na ugombeaji wa nafasi hiyo ndani ya Chadema isipokuwa uchaguzi wa mtu mmoja tu kama walivyofanya CUF na Lipumba aloweka nia. hapakuwepo na kiako cha aina yeyote kujadili majina ya wagombea kwa sababu fomu hazikutoka hiyo ndio ukweli kama nasema uongo nambie majina ya watu walochukua fomu na kurudisha kabla ya tarehe 30 na 25. Chadema walikuwa wakisubiri tu mfadhili wao Supreme Leader japo mlitupiga pande humu tuamini Lowassa ni wa ACT..
Sasa unataka tukubali unachoandika wewe bila ushahidi wowote kuwa ndio ukweli? Mpaka hapo umeona uongo wako, ukweli ni kuwa nafasi ya uchukuaji wa form ya urais ulitangazwa, sasa kama watu walijitokeza wakanyimwa form au walitangaza kinafiki kinafiki hilo ni swala lingine ambalo linahitaji ushaidi.Mpaka hapo hoja ya
@Jokakuu inasimama kuwa Dr. Slaa hakuchukua fomu.
Na kama unakumbuka unajua kwamba walisema mgombea Urais atatangazwa week moja baada ya uchaguzi wa CCM, lakini walipoahihisha nao wakaahirisha hadi baada ya CCM kumtangaza. sasa basi kama kuna ukweli wowote basi tuone Lipumba akigombea na Lowassa au nayo imefanyika nyuma ya pazia?.. Chadema sasa hivi wamejaa WANAFIKI watupu walikataa kuwa Lowassa hakukutana na viongoziwa Chadema na wala hatapokelewa. Mbowe aliwahi kusema over his dead body, sasa imekuwaje?.. .
Mbowe/Chadema si Msaafu au Biblia kuwa watakachosema hakibadiliki, hawa ni banadamu kama mimi na wewe wanabadilika kutokana na mazingira na hali halisi. Na kosa si kusogeza mbele utangazaji wa mgombea urais bali kosa kama wasingetangaza mgombea urais. Sasa kama unatangaza mgombea urais leo au mwezi ujao hiyo si hoja, hoja ni je umemtangaza mgombea urais???
Samahani kuhusu mwaka alohama Dr.Slaa lakini ukweli ni kwamba mtandao huu umekuwepo toka Enzi ya Mwiyi sema tu Mwalimu Nyerere alishindwa kuwadhibiti na ndio maana ukisikiliza hotuba yake ya NEC kmwaka huo 1995 utajua nili maanisha nini. Mimi binadamu nakosema sana katika maandishi yangu na hujichanganya vile vile lakini lengo langu ni kuonyesha kwamba hawa watu hawana nia njema kabisa na nchi hii..
Sasa kama wewe unakosea kiubinadamu jambo ambalo sina tatizo lao, je Mbowe/Dr.Slaa hawaruhusiwi kukosea kiubinadamu?