CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

..Dr.Slaa ha kuchukua fomu.

..inasemekana cc ya cdm ilimpendekeza.

..sasa cc ya cdm imempendekeza Lowassa badala ya Dr.Slaa.

..pia inaelekea nccr na cuf wamemkubali Lowassa kuliko ambavyo cdm wamemkubali.

..halafu kuna zile tetesi kwamba cuf hawamtaki Dr.Slaa. Huenda ni ukweli. Labda tujiulize fomu aliyochukua Prof. Lipumba imepotelea wapi? Je, Prof wakati anachukua fomu hakujua kwamba anayepaswa kugombea kupitisha ukawa ni Dr.Slaa?

..inawezekana Lowassa anawaunganisha Ukawa kuliko ambavyo Dr.Slaa angewaunganisha.

. Mkandara, Susuviri, Nguruvi3, Mag3, King Suleiman
..

Jokakuu:

lol naona umejikita kwenye tetesi. Nadhani wapinzani nao wameanza kuwa pragmatic. Nikiangalia kura za maoni za wabunge, mikutano ya CDM ina wapiga kura 200, wakati CCM wana 1000. Namba hazidanganyi. Wapinzani wanaweza kuwa very vocal and committed, but if the fail to overcome numerical advantage during the election, they will go back where they started. Kama Lowassa anatibua namba ya wapiga kura wa CCM, inawezekana wapinzani hawakutaka maumivu.
 
..inabidi tujikite kwenye tetesi maana mambo yenyewe yanaendeshwa kama enzi za Soviet Union.

..umezungumzia suala zuri sana kuhusu kama cdm wana numerical advantage over ccm.

..hoja yako ingekuwa na majibu kama idadi ya wanachama wa cdm nchi nzima ingekuwa inajulikana.

..cdm wamekuwa ktk harakati za kuwaelimisha wananchi kuhusu ufisadi na mabilioni yanayotafunwa kwa miaka karibu 10 sasa.

..Je kwa kampeni na harakati hizo wameweza kuandikisha wanachama kiasi gani?
.
 
Mkandara,

..Dr alitakiwa awe na fomu yake tayari.

..nini kilikuwa kinampa kigugumizi asichukue fomu?

..sasa hata haieleweki kama alikuwa anataka kugombea au alikuwa anasubiri aombwe na chama chake.

..je, tatizo ni kwamba hamtaki Lowassa? Au, tatizo ni kwamba amedhulumiwa nafasi hiyo?

..Je, Mbowe angeleta mtu asiye na tuhuma bado kungekuwa na sintofahamu tuliyonayo sasa hivi?

Cc Nguruvi3, Zakumi
 
Last edited by a moderator:
..inabidi tujikite kwenye tetesi maana mambo yenyewe yanaendeshwa kama enzi za Soviet Union.

..umezungumzia suala zuri sana kuhusu kama cdm wana numerical advantage over ccm.

..hoja yako ingekuwa na majibu kama idadi ya wanachama wa cdm nchi nzima ingekuwa inajulikana.

..cdm wamekuwa ktk harakati za kuwaelimisha wananchi kuhusu ufisadi na mabilioni yanayotafunwa kwa miaka karibu 10 sasa.

..Je kwa kampeni na harakati hizo wameweza kuandikisha wanachama kiasi gani?
.
Endapo hawana idadi, kuna la kujiuliza. Je, zile opereshenizilikuwa ‘bonanza'?

Baada ya 2010 tuliwaambia wapinzani katika uzi mmoja wa Mzee Mwanakijiji kuwa haitoshikukusanya watu, lazima kuwe na ufuatailiaji na ikiwezekana daftari la kura lawapinzani.
Tunategemea maswali kama haya yawe na majibu

Pili, Zakumi ana hoja muhimu. Ukiangalia kwa survey tu,watu wanaofuatilia chaguzi za awali hapa JF, update za CCM zinawasomaji wengi.

Hata ukweli unaonyesha hivyo, kwamba kura za maoni zipo katika ''1000s'' wakati Wapinzani ni katika ''100s''
 
Mkuu maneno haya sio kweli, Ofisi ya Chadema ilifungwa baada tu ya Lowassa kuchukua fomu na hakuruhusiwa mtu mwingine yeyote kuchukua fomu ya Urais, hivyo kupendekezwa kwa Dr.Slaa wakati uchukuaji fomu bado haujatangazwa rasmi haina maana yoyote. Chadema wametuonyesha mfumo mbovu kuliko hata ule wa CCM kuengua watu na kamati ya maadili jambo ambalo mimi naona CCM wameboresha mfumo wao zaidi ili kupata viongozi wenye sifa, zamani hapakuwa na sifa isipokuwa mwenye umaarufu na uwezo wa ku deal na matatizo!
.
Mkuu unapoongea vitu lazima uwe na uhakika navyo, tafadhali sana

Uwe na uhakika na unachosema na si kutumbukiza hisia zako.Please
 
..suala lingine linalonitatiza ni AGENDA za cdm wwanapokwenda kwa wananchi mikoani.

..majuzi nilibahatika kuangalia video za mikutano ya salum mwalimu, upendo penezya,na tundu lissu.

..i came out disappointed kwamba viongozi hao walishindwa ku-connect na wananchi waliokuwepo ktk mkutano.

..sidhani kama wananchi huko vijijini wanaguswa na hoja za ufisadi. Kama hoja hiyo ingekuwa na mashiko kwelikweli basi leo hii ccm ingekuwa imeshaanguka.

..kingine nilichokiona ni wananchi wana-connect na mzungumzaji pale anapojenga hoja kuhusu masuala au kero zilizopo ktk eneo husika.

..kwa mfano ilipozungumzwa hoja ya wachimbaji wadogo wadogo pamoja na haki zao wananchi waliitikia vizuri kuliko wakati mzungumzaji alipokuwa akimwaga ma-data ya mabilioni ya ufisadi.

..kwa hiyo mimi nadhani cdm watakuwa na nafasi nzuri zaidi kama watakuwa na a good mix ya hoja za ufisadi na hoja zinazohusu kero za kila siku za wananchi huko vijijini.

Cc Zakumi, Molemo, Mkandara, Mag3, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Hii inatokana na sababu kwamba hata wabunge wetu wanatafuta umaarufu wa Kitaifa badala ya kutumikia Majimbo yao. Na hii inatokana na mfumo uliopo ambao mbunge anaishi Dar wakati anawakilisha Kishapu. Hajui matatizo ya wananchi wake jimboni hadi uchaguzi mkuu kazi kutafuta umaarufu kesho awe waziri. Maswala ya Ufisadi yanatakiwa katika mdahalo wa wagombea Urais ambapo mgombea analitazama maswala mazima ya Kitaifa.

Leo hii upande wa twitter tumezungumzia sana swala la Dira ya Kitaifa ambapo maswala muhimu ya UMaskini, Ujinga na Maradhi yamekuwa sio kipaumbele tena kwa wabunge wetu hivyo wanaposimama majukwaani huwa hawana sera.

Kilichonifurahisha zaidi ni KARMA, yaani Chadema ilokuwa wakimcheka Zitto na kumwita Supreme Leader leo wao ndio wao wanaongozwa na Supreme Leader wa ukweli. Na hawawezi kuwa na nafasi nzuri hata kidogo wakigusia Ufisadi watajimaliza kisiasa kwa sababu mafisadi wote sasa hivi Chadema ndio kimbilio lao. Na huwezi kuwa Fisadi na Greed ukakumbuka matatizo ya wananchi, vitu havi havishabihiani..Hizo ahadi za Lowassa kuwafanya watu wote matajiri ati anauchukia Umaskini wakati kuna ndugu zake mwenye hadi leo ni maskini..

- Atawadanganya wangapi?
 
Mkuu unapoongea vitu lazima uwe na uhakika navyo, tafadhali sana

Uwe na uhakika na unachosema na si kutumbukiza hisia zako.Please
Ebu wewe tupe Uhakika ulikuwa vipi kama kuna mgombea aloruhusiwa kuchukua fomu ya Urais Chadema? mimi nasema kwa sababu najua hilo limetokea na limepangwa nje kabisa ya taratibu za chama kwa miaka yote. Je, unajua kwamba hata Dr.Slaa amepinga kumpa mtu huyu nafasi hiyo pasipo masharti ama kufuata utaratibu wa kikatiba?

Huu ni mpango mpya baada ya maridhiano ya viongozi wa Chadema na Lowassa. Kwa hiyo ni bora wewe nisahihishe kuliko kuhoji Uhakika wangu wakati wewe mwenyewe huna uhakika. Leo unaye Supreme Leader unaanza kubabaika eeeh!
 
Mkuu maneno haya sio kweli, Ofisi ya Chadema ilifungwa baada tu ya Lowassa kuchukua fomu na hakuruhusiwa mtu mwingine yeyote kuchukua fomu ya Urais, hivyo kupendekezwa kwa Dr.Slaa wakati uchukuaji fomu bado haujatangazwa rasmi haina maana yoyote. Chadema wametuonyesha mfumo mbovu kuliko hata ule wa CCM kuengua watu na kamati ya maadili jambo ambalo mimi naona CCM wameboresha mfumo wao zaidi ili kupata viongozi wenye sifa, zamani hapakuwa na sifa isipokuwa mwenye umaarufu na uwezo wa ku deal na matatizo!.

Pamoja na kukubaliana na wewe katika baadhi ya hoja hasa swala la Lowassa na urais Chadema/Ukawa lakini naomba nikujulishe kuwa ulichoandika hapa ni uongo na fitina zilizoptiiliza (samahani kwa maneno hayo). Swala la kugombea Ubunge, Udiwani na urais vilitangawa na kulikuwa na thread humu ndani ninashindwa kuamini kuwa hilo tangazo hukuliona.
Tangazo lao ili hapa.

CHADEMA yafungua milango: Ratiba ya kuchukua fomu, vikao vya mchujo na uteuzi wa wagombea - wavuti

URAIS
Kuhusu urais, Mbowe alisema kuchukua na kurejesha fomu kutafanyika kati ya Julai 20 na 25, mwaka huu na Agosti 3 na 4, mwaka huu vikao vya Baraza Kuu la Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CHADEMA vitakutana.

Alisema wanachama watakaochukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania urais mwaka huu, watapelekwa kwenye mchujo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kupatikana mgombea mmoja atakayesimama kwa niaba ya vyama vinavyounda Ukawa.

Vyama vinavyounda UKAWA ni CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD).

Na baada ya hiyo tarehe kuwa zimepita kulikuwa hakuna mgombea hata mmoja wa Chadema aliyechukua form ya urais ndio wakaongeza muda.. udhibitisho ni huu:

http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...-moto/-/1597296/2807628/-/70tt1d/-/index.html

Mimi naomba tuutazame ukweli nao ni kwamba Dr.Slaa alihama CCM kwa sababu ya kundi hili hili la Mtandao mwaka 2005. hawa walichagua watu wao na kuwasimamisha hivyo yeyote ambaye hakuwa nao walimtosa kwa sababu walikuja kuchuma na wamechuma kweli kweli. Na ikumbukwe pia kwamba kama mwaka 2005 jina la JK lingeenguliwa kundi hili lingekuja CHadema na hivyo utawala mzima wa JK na ubovu wake ungekuwa wa Chadema sio CCM. na hii ndio hali halisi.i

Kuweka kumbukumba sawa Dr. Slaa alihama mwaka 1995 wakati wa Mh.Mkapa. Sina uhakika kama kundi la wanamtando unalolisema kama lilikuwepo. Pia kumbuka uliwahi kusema kwa:

"""Mnajua nyie mna tatizo sana kwa sababu mnaipenda sana Chadema mkashindwa kutazama ukweli. Ebu turudi nyuma kidogo tuachane na chama ila tuzungumze WATU.. Ebu tumchukue Dr.Slaa, huyu mwaka 1995 alijiandikisha kugombea Ubunge Karatu kwa tiketi ya CCM akashindwa na mwenzake ndani ya CCM, akahamia CDM kabla ya uchaguzi na kujiandikisha upya kama mgombea wa CDM jimbo hilo hilo la Karatu"" by Mkandara 9.May.2015.
 
Ebu wewe tupe Uhakika ulikuwa vipi kama kuna mgombea aloruhusiwa kuchukua fomu ya Urais Chadema? mimi nasema kwa sababu najua hilo limetokea na limepangwa nje kabisa ya taratibu za chama kwa miaka yote. Je, unajua kwamba hata Dr.Slaa amepinga kumpa mtu huyu nafasi hiyo pasipo masharti ama kufuata utaratibu wa kikatiba?

Huu ni mpango mpya baada ya maridhiano ya viongozi wa Chadema na Lowassa. Kwa hiyo ni bora wewe nisahihishe kuliko kuhoji Uhakika wangu wakati wewe mwenyewe huna uhakika. Leo unaye Supreme Leader unaanza kubabaika eeeh!
Nani amefunga ofisi, lini na sababu zipi , kwa amri ya nani? Tunachotaka ni habari zenye uhakika

Mag3 kamwambia mtu hapo juu, bilioni 10 ni umbea na hapa simahali pake.
Huyo aliyeleta bilioni 10 naye alikuwa anajua kama wewe

Tunasema hivi kwasababu hatutaki mijadala ya majungu jungu tu ya kusikia

cc Molemo
 
Last edited by a moderator:
[/QUOTE]Bibie hiyo ni taarifa tu ilitolewa lakini ukweli ni kwamba nafasi ya rais haikuwa hivyo. hapakuwepo na ugombeaji wa nafasi hiyo ndani ya Chadema isipokuwa uchaguzi wa mtu mmoja tu kama walivyofanya CUF na Lipumba aloweka nia. hapakuwepo na kikao cha aina yeyote kujadili majina ya wagombea Urais kwa sababu fomu hazikutoka huu ndio ukweli kama nasema uongo nambie majina ya watu walochukua fomu za urais na kurudisha kabla ya tarehe 20 na 25. Chadema walikuwa wakisubiri tu mfadhili wao Supreme Leader japo mlitupiga pande humu tuamini Lowassa ni wa ACT..

Na kama unakumbuka unajua kwamba walisema mgombea Urais atatangazwa week moja baada ya uchaguzi wa CCM, lakini walipoahihisha nao wakaahirisha hadi baada ya CCM kumtangaza. sasa basi kama kuna ukweli wowote basi tuone Lipumba akigombea na Lowassa au nayo imefanyika nyuma ya pazia?.. Chadema sasa hivi wamejaa WANAFIKI watupu walikataa kuwa Lowassa hakukutana na viongozi wa Chadema na wala hatapokelewa. Mbowe aliwahi kusema over his dead body, sasa imekuwaje?..

Samahani kuhusu mwaka alohama Dr.Slaa lakini ukweli ni kwamba mtandao huu umekuwepo toka Enzi ya Mwinyi sema tu Mwalimu Nyerere alishindwa kuwadhibiti na ndio maana ukisikiliza hotuba yake ya NEC mwaka huo 1995 utajua nili maanisha nini. Mimi binadamu nakosema sana katika maandishi yangu na hujichanganya vile vile lakini lengo langu ni kuonyesha kwamba hawa watu hawa hawana nia njema kabisa na nchi hii, Alomrudisha madarakani Lowassa nani kama sio Mwinyi?
 
[/QUOTE] Ahsante Alinda

Mkuu Mkandara , Alinda kaja na hoja hizo. Ni wakati utuambie kama uliyosema bado unasimama nayo na kwasababu zipi

Kumbuka madai yako ni mazito ima kwa uongozi au wanachama.Kuyaacha tu kama yalivyo ni fitna.
Tuondoe fitna kwa wewe kutueleza ukweli
au kufuta

Nani amefunga ofisi, lini na sababu zipi , kwa amri ya nani? Tunachotaka ni habari zenye uhakika

Mag3 kamwambia mtu hapo juu, bilioni 10 ni umbea na hapa simahali pake.
Huyo aliyeleta bilioni 10 naye alikuwa anajua kama wewe

Tunasema hivi kwasababu hatutaki mijadala ya majungu jungu tu ya kusikia

cc Molemo
Mkuu hiki ni kiswahili cha Mjini tu kufunga Ofisi haina maana nyingine zaidi ya kwamba fomu zilikuwa hazitoki yaani meza ya kutoa fomu za Urais haikuwepo!
 
Mkuu hiki ni kiswahili cha Mjini tu kufunga Ofisi haina maana nyingine zaidi ya kwamba fomu zilikuwa hazitoki yaani meza ya kutoa fomu za Urais haikuwepo!
Kwani fomu zinatolewa chini ya madaraka ya nani? Mwenyekiti,Katibu, au nani?
 
Kwani fomu zinatolewa chini ya madaraka ya nani? Mwenyekiti,Katibu, au nani?
Wee sio ndio unaujua ukweli, unaniuliza miye ili iweje? Nasema fomu za Urais hazikutoka Dr.Slaa aliweka nia lakini hakuchukua fomu wala hakupewa hata kaa angetaka!.. Lowassa ni Supreme Leader hataki kushindana na mtu yeyote ni moja ya mashatri yake yeye. hamtaki anaondoa Mabillioni yake..

Mkuu Mbowe mshikaji,, siwezi simama hapa kusema ovyo pasipo sababu wala kuchukia hatua alizochukua na siwezi kumbadilisha. Yeye kawambieni mtakuja kumwelewa baadaye sasa nyie subirini kumwelewa..
 
Bibie hiyo ni taarifa tu ilitolewa lakini ukweli ni kwamba nafasi ya rais haikuwa hivyo. hapakuwepo na ugombeaji wa nafasi hiyo ndani ya Chadema isipokuwa uchaguzi wa mtu mmoja tu kama walivyofanya CUF na Lipumba aloweka nia. hapakuwepo na kiako cha aina yeyote kujadili majina ya wagombea kwa sababu fomu hazikutoka hiyo ndio ukweli kama nasema uongo nambie majina ya watu walochukua fomu na kurudisha kabla ya tarehe 30 na 25. Chadema walikuwa wakisubiri tu mfadhili wao Supreme Leader japo mlitupiga pande humu tuamini Lowassa ni wa ACT..

Sasa unataka tukubali unachoandika wewe bila ushahidi wowote kuwa ndio ukweli? Mpaka hapo umeona uongo wako, ukweli ni kuwa nafasi ya uchukuaji wa form ya urais ulitangazwa, sasa kama watu walijitokeza wakanyimwa form au walitangaza kinafiki kinafiki hilo ni swala lingine ambalo linahitaji ushaidi.Mpaka hapo hoja ya @Jokakuu inasimama kuwa Dr. Slaa hakuchukua fomu.

Na kama unakumbuka unajua kwamba walisema mgombea Urais atatangazwa week moja baada ya uchaguzi wa CCM, lakini walipoahihisha nao wakaahirisha hadi baada ya CCM kumtangaza. sasa basi kama kuna ukweli wowote basi tuone Lipumba akigombea na Lowassa au nayo imefanyika nyuma ya pazia?.. Chadema sasa hivi wamejaa WANAFIKI watupu walikataa kuwa Lowassa hakukutana na viongoziwa Chadema na wala hatapokelewa. Mbowe aliwahi kusema over his dead body, sasa imekuwaje?.. .

Mbowe/Chadema si Msaafu au Biblia kuwa watakachosema hakibadiliki, hawa ni banadamu kama mimi na wewe wanabadilika kutokana na mazingira na hali halisi. Na kosa si kusogeza mbele utangazaji wa mgombea urais bali kosa kama wasingetangaza mgombea urais. Sasa kama unatangaza mgombea urais leo au mwezi ujao hiyo si hoja, hoja ni je umemtangaza mgombea urais???

Samahani kuhusu mwaka alohama Dr.Slaa lakini ukweli ni kwamba mtandao huu umekuwepo toka Enzi ya Mwiyi sema tu Mwalimu Nyerere alishindwa kuwadhibiti na ndio maana ukisikiliza hotuba yake ya NEC kmwaka huo 1995 utajua nili maanisha nini. Mimi binadamu nakosema sana katika maandishi yangu na hujichanganya vile vile lakini lengo langu ni kuonyesha kwamba hawa watu hawana nia njema kabisa na nchi hii..

Sasa kama wewe unakosea kiubinadamu jambo ambalo sina tatizo lao, je Mbowe/Dr.Slaa hawaruhusiwi kukosea kiubinadamu?
 
Wee sio ndio unaujua ukweli, unaniuliza miye ili iweje? Nasema fomu za Urais hazikutoka Dr.Slaa aliweka nia lakini hakuchukua fomu wala hakupewa hata kaa angetaka!.. Lowassa ni Supreme Leader hataki kushindana na mtu yeyote ni moja ya mashatri yake yeye. hamtaki anaondoa Mabillioni yake..

Mkuu Mbowe mshikaji,, siwezi simama hapa kusema ovyo pasipo sababu wala kuchukia hatua alizochukua na siwezi kumbadilisha. Yeye kawambieni mtakuja kumwelewa baadaye sasa nyie subirini kumwelewa..
Mkuu Mkandara, umeshindwa kuthibitisha madai yako kuwa ofisiza CDM zilifungwa.
Sijatoa madai kuhusu fomu , wagombea au chochote.

Madai hayoumeanzisha wewe, tumekutaka uthibitishe! Umeshindwa hata unababaka baika tu

Kama ni lugha ya mtaani ungeandika hivi ‘ofisi zilifungwa' hizo alama zina maana kiuandishi

Umeshindwa kujibu hoja za Alinda kuhusu ukweli.

Alinda ameweka ushahidi,wewe unasema ni maneno tu. Huna ushahidi dhidi ya ule alioweka

Mkandara, hapa si mahali pa fitna na majungu. Tafadhali sana usituondoe katika mjadala mzito kutuelekezakatika fitna

Hoja yako imefungwa, hakuna ofisi ya CDM iliyofungwa. Ni fitna na uongo wa Mkandara kama hulka yake.
 
Sasa unataka tukubali unachoandika wewe bila ushahidi wowote kuwa ndio ukweli? Mpaka hapo umeona uongo wako, ukweli ni kuwa nafasi ya uchukuaji wa form ya urais ulitangazwa, sasa kama watu walijitokeza wakanyimwa form au walitangaza kinafiki kinafiki hilo ni swala lingine ambalo linahitaji ushaidi.Mpaka hapo hoja ya jokaa Kuu inasimama kuwa Dr. Slaa hakuchukua fomu.
Sikusema haikutangazwa siku ya kuchukua fomu, nilichosema ni kwamba Fomu hazikutolewa sasa kama wewe unao ushahidi fomu ziliztoka na watu wakachukua uweke hapa ndio utasema mimi muongo.

Mbowe/Chadema si Msaafu au Biblia kuwa watakachosema hakibadiliki, hawa ni banadamu kama mimi na wewe wanabadilika kutokana na mazingira na hali halisi. Na kosa si kusogeza mbele utangazaji wa mgombea urais bali kosa kama wasingetangaza mgombea urais. Sasa kama unatangaza mgombea urais leo au mwezi ujao hiyo si hoja, hoja ni je umemtangaza mgombea urais???
Swala tunazungumzia hapa sio kutangaza jina la mgombea bali utaratibu wa kuchukua fomu haukutokea kwa Dr.Slaa kama alivyosema JokaKuu ya kwamba Dr.Slaa aliombwa achukue fomu na hakufanya hivyo, ukweli ni kwamba hakupewa wala hakuruhusiwa iliandaliwa kutazamia matokeo ya CCM kwanza, kama Lowassa atamwagwa au laa - Walikusudia..

Sasa kama wewe unakosea kiubinadamu jambo ambalo sina tatizo lao, je Mbowe/Dr.Slaa hawaruhusiwi kukosea kiubinadamu?
Bibie mimi nakosea katika maandishi yangu badala ya kuandika mwaka 2005 wakati nilimaanisha mwaka 1995, haina maana inaondoa hoja ama maana ya kile nilichokusudia kusema. Hili swala la kumtangaza Lowassa kama mgombea mmoja pasipo kushindanishwa tena kwa matakwa yake na masharti yake sio la makosa, ila ni mpango maalum wenye nia na lengo la kuhakikisha Lowassa anapita bila kupingwa..
 
Mkuu ikiwa fomu hazikutolewa ulitaka mimi nithibitishe vipi?.. Labda wewe unayejua zaidi nambie, au nipe mfano ikiwa wewe ungejua ofisi haikutoa fomu za mgombea urais utathibitisha vipi? mathlan..wakati mwingine mnabisha tu ili mradi kubisha mtu utathibitisha vipi kuwa fomu hazikutolewa!..kama ningesema zilitolewa, ningekuonyesha fomu hii hapa sasa hazikutolewa nikuonyeshe nini..
 
Sikusema haikutangazwa siku ya kuchukua fomu, nilichosema ni kwamba Fomu hazikutolewa sasa kama wewe unao ushahidi fomu ziliztoka na watu wakachukua uweke hapa ndio utasema mimi muongo.

Swala tunazungumzia hapa sio kutangaza jina la mgombea bali utaratibu wa kuchukua fomu haukutokea kwa Dr.Slaa kama alivyosema JokaKuu ya kwamba Dr.Slaa aliombwa achukue fomu na hakufanya hivyo, ukweli ni kwamba hakupewa wala hakuruhusiwa iliandaliwa kutazamia matokeo ya CCM kwanza, kama Lowassa atamwagwa au laa - Walikusudia..

Bibie mimi nakosea katika maandishi yangu badala ya kuandika mwaka 2005 wakati nilimaanisha mwaka 1995, haina maana inaondoa hoja ama maana ya kile nilichokusudia kusema. Hili swala la kumtangaza Lowassa kama mgombea mmoja pasipo kushindanishwa tena kwa matakwa yake na masharti yake sio la makosa, ila ni mpango maalum wenye nia na lengo la kuhakikisha Lowassa anapita bila kupingwa..

Hivi umesoma ulichokiandika au unataka kubishana na bibie Alinda? Hizo fomu zitatokaje kama hakuna mtu aliyekwenda kuziomba/kuzichukua? Tangazo lilitolewa, hakuna mtu ambaye alikwenda kuchukua fomu, sasa wewe unataka nikuonyeshe watu waliokwenda kuchukua fomu?????????? kweli?

Unataka Dr. Slaa aombwe na nani kuchukua fomu? Na Dr. Slaa ana cheo gani ndani ya Chadema? Au unachotaka kutwambia kuwa Mbowe alimficha Dr. Slaa fomu? (kama ni hivyo hizi ndizo fitina nilizosema?

Nilichokwambia kama wewe unakosea, kama binadamu je na wengine wasikosee?
 
Back
Top Bottom