Wasipo mzuia Rais kuhutubia Bunge, itakuwa haina maana wabunge hao kususia huku nje wanaisikiliza hiyo hotuba na pia dunia yote kwa ujumla.
Isitoshe, kutokufanya hivyo itakuwa sawa na maamuzi yao ya kususia Bunge la Bajeti, ambayo imedhihirika hayakuwasaidia kufikia lengo lao na badala yake limewaweka njia panda katika ulingo wa siasa.
Hivyo basi, vitendo vyao vya kususasusa, wakiwa Waheshimiwa wawakilishi wa wananchi, nawaza kwa sauti tu, ingekuwaje kama wafuatao nao wakiamua kususia majukumu yao na kujifungia kwa siku 14, ili kujihakikishia hawana maambukizi ya korona:
√ Polisi;
√ Madereva wa vyombo vya usafiri (Mabus, Meli, Treni, Daladala);
√ Watumishi wa afya, ambao ndio wako karibu sana na wagonjwa;
√ Wafanya biashara, hasa wa vyakula;
√ Na kadhalika.
Kama lengo ni kusikika kimataifa, njia sahihi ni kupambana, uso kwa uso, na wanae amini anawakandamiza kufikia malengo yao. Wamzuie Rais kulihutubia Bunge.