SI KWELI CHADEMA wametumia Picha ya AI kuongeza idadi ya wafuasi kwenye mkutano wao Arusha?

SI KWELI CHADEMA wametumia Picha ya AI kuongeza idadi ya wafuasi kwenye mkutano wao Arusha?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1778315166655.png
 
Tunachokijua
Mei 08, 2026 viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema walifanya mkutano wa hadhara katika eneo la Soko Kuu Arusha.

Madai

Kumekuwapo na picha mbili zinazosambazwa mtandaoni zikionesha hali ya wafuasi wa chama hicho waliohudhuria katika mkutano huo, moja ikionesha idadi ndogo ya watu huku nyingine ikionesha idadi kubwa zaidi jambo lililoibua utata kuhusu uhalisa wa picha hizo.

Uhalisia

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa picha inayoonesha idadi ndogo ya watu imehaririwa kwa Akili Unde kutoka kwenye picha halisi ambayo inaonesha idadi kubwa zaidi. Aidha marejeo ya picha za video yanaonesha idadi ya watu sawa kama inavyoonekana katika picha yenye watu wengi.

Hata hivyo picha yenye watu wachache imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambayo ni ya kawaida kwa picha zinazohaririwa au kutengenezwa kwa AI, mfano kukosewa kwa maandishi katika bendera ya CHADEMA, changamoto katika sura na viungo vya watu ikiwemo kuzidi kwa idadi ya mikono kwa baadhi ya watu.

Sanjari na hayo nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde zinabainisha uhalisia wa Picha hizi.​

screenshot-2026-05-09-112421-png.3586033

screenshot-2026-05-09-113408-png.3586034
Pamoja na mapungufu yao ya hapa na pale hiki chama kiko vizuri kwenye ishu za kidijitali. Wanaenda vizuri na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia. Ninawapongeza na kuwasihi waendelee hivyohivyo labda itawasaidia kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2030.

Hizi pongezi zangu zimetokana na mkutano wao uliofanyika jana huko Arusha mjini maeneo ya soko kuu. Pamoja na uhaba wa wahudhuriaji kwenye mkutano wao ila CHADEMA hawakukaa kinyonge na kutimia akili kubwa sana kupitia teknolojia ya ARTIFICIAL INTELLIGENCE kuhariri picha kabla ya kuzichapisha mitandaoni zikionyesha watu wakiwa wamejaa mkutanoni kupitiliza. Hakika hii ni akili kubwa kisiasa.

Ingawa watu wengi mtandaoni wameonekana kuchukizwa na kilichofanyika kwasababu ni kujidanganya ila mimi ninawapongeza CHADEMA kwa matumizi ya teknolojia. Angalau kwa sasa watabakiwa na aibu ya kura chache kwenye sanduku la kura ila kwenye post za mtandaoni AI itawanusuru.
 
Mimi Jana nilikuwepo Arusha hakukuwa na watu kabisa kwenye mkutano wa Lema na ukiangalia kwenye social media picha ni tofauti na uhalisia eti chadema mnafanya hivo kwa faida gani?

Acheni usela usela nyie matapeli wa kisiasa.
 
Kwa hiyo mods huu uzi hapa chini ungefungwa

 
Dunia ya sasa unafanya upuuzi kama huu kweli?
Mimi pia nimeshangaa na kubaki kujiuliza, Pengine hili jambo ukilifanya upande ule ambao yuko yeye watakusifu sanaa na kuna kitu unaweza pata..
Maana siamini kwa utashi wake anaweza kuwa na akili za wivu za kuchezea AI kisa Chadema tu..
 
Na kwani idadi ya watu ikiwa kubwa au ndogo huyo akili finyu inamhusu nini kma yy yupo upande b si atulie shida nn nn kwani ..anyway m bad sina chama
 
Back
Top Bottom