Pamoja na mapungufu yao ya hapa na pale hiki chama kiko vizuri kwenye ishu za kidijitali. Wanaenda vizuri na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia. Ninawapongeza na kuwasihi waendelee hivyohivyo labda itawasaidia kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2030.
Hizi pongezi zangu zimetokana na mkutano wao uliofanyika jana huko Arusha mjini maeneo ya soko kuu. Pamoja na uhaba wa wahudhuriaji kwenye mkutano wao ila CHADEMA hawakukaa kinyonge na kutimia akili kubwa sana kupitia teknolojia ya ARTIFICIAL INTELLIGENCE kuhariri picha kabla ya kuzichapisha mitandaoni zikionyesha watu wakiwa wamejaa mkutanoni kupitiliza. Hakika hii ni akili kubwa kisiasa.
Ingawa watu wengi mtandaoni wameonekana kuchukizwa na kilichofanyika kwasababu ni kujidanganya ila mimi ninawapongeza CHADEMA kwa matumizi ya teknolojia. Angalau kwa sasa watabakiwa na aibu ya kura chache kwenye sanduku la kura ila kwenye post za mtandaoni AI itawanusuru.