CHADEMA wamshangaa Komu kusubiri posho za ubunge, wajiandaa kumtosa

CHADEMA wamshangaa Komu kusubiri posho za ubunge, wajiandaa kumtosa

Huu mtego ni ngumu sana kueleweka kwa watu waliozoea siasa za matusi na kufuata mkumbo

Hivi mmeshawahi kujiuliza, kwanini wananchi wa maeneo mengi walikua wanachagua diwani chadema, mbunge chadema ila raisi ccm?

Jibu ni moja, mumei-attach chadema na ukanda+ukabila

Hili kosa walilifanya Cuf pia, wao waliki-attach chama chao na dini, wote tunajua Cuf ilipoishia

NB:Ushauli, hili jambo msilichukulie kama propaganda za CCM, jichunguzeni vinginevyo mtaendelea kutoaminiwa na wananchi wa maeneo mengine, nina uhakika haya yangefanywa na kubenea au mtu yeyote asiye na damu ya kulee angetimuliwa siku hiyo hiyo.
 
Huyu Komu hana maarifa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilishangaa sana jana akiwa anasema kasoma UDSM nakumbuka mazungumzo yake na Kubenea kwenye simu wakati fulani wakimponda Mbowe halafu anasema haaminiki ndani ya chama. Hivi angeaminikaje baada ya dhamira yake ya mapinduzi?
Bado akaja kusikika tena kwenye mtandao wakiwa wana panga kumpindua mtu ACT wazalendo. Ndio maana nasema Komu ni malaya wa siasa hajawahi kuwa mpinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kufikiria kama tuna waheshimiwa wapumbavu kiasi hiki
Hapana huyu siyo mpumbavu, yuko wazi. Tatizo letu sisi tunapenda unafiki pamoja na kudanganywa. Watu wanaosema ukweli waziwazi hatuwapendi.

Huyu amewapa option nzuri CHADEMA kwa sababu pia wana haki ya kumfukuza, kablay ya muda wa Ubunge wake kuisha. Mngependa akae kimya halafu aje ashtukize baada ya Ubunge wake kuisha?

Hiyo ndiyo ingekuwa nzuri zaidi kuliko alivyofanya sasa? Tatizo letu watu tunapenda unafiki ikiwa ni pamoja na kudanganywa danganywa
 
Nani alimwambia atoe siri mapema, angetulia kwanza apige posho zake ndio asepe
 
..amesema bunge litakapovunjwa ndiyo atakuwa haitaki cdm.

..binafsi sioni sababu ya cdm kugombana naye. wasubiri bunge liishe waagane kwa furaha na bashasha

Mawazo yako sawia na yangu, asifukuzwe wala asigeuzwe mada. Bado miezi miwili bunge kuvunjwa, akifukuzwa ni kumpa promo tu.
 
Mie binafsi nafikiri wakati huu kabla ya uchaguzi vyama vya upinzani na hasa vile vinavyopigwa mawe mengi na CCM, vingeangalia upya katiba zao, namna zinavyotoa mwanya kwa wanachama waliobebwa na chama kisha anakuja kukisaliti chama katika wakati ambao chama kinamhitaji!

Nashauri ikibidi viongezwe vifungu kwenye katiba za vyama vinavyomtaka kiongozi yoyote aliyechaguliwa kupitia chama akiamua kukihama chama kabala mhula haujaisha au kufukuzwa na chama kwa sababu zozote zile, basi awajibike pia kukirudishia chama mishahara na posho zote alizokwisha lipwa kwa kipindi chote wakati akiwa mbunge wa chama hicho,

akilipe pia chama gharama za mishahara na posho zote angezostahili kuzipata kwa kipindi chote cha ubunge wake kwa miaka yote iliyobakia kufikia mhula wa miaka mitano! Kungekuwa na mikataba ya namna hii ingesaidia kupunguza athari za wasaliti!
 
Back
Top Bottom