CHADEMA wamshangaa Komu kusubiri posho za ubunge, wajiandaa kumtosa

CHADEMA wamshangaa Komu kusubiri posho za ubunge, wajiandaa kumtosa

Wakimpiga chini anaweza ning'inia kwenye ubunge wa mahakama mpaka aitie mkononi posho yake"chezea mangi wewe"

Sent using Jamii Forums mobile app
Mku hapo umepatia kile "Mangi" anachoweza kukifanya. Hakuna Mangi anaekaa mbali na pesa!!!! Na wakimtosa wakati wanajua uchaguzi ni kesho kutwa itakuwa aibu just because yeye ataenda Mahakamani kama wabunge wengi wanavyofanyaga.Its much more prudent management team Chadema wapuuzie tu.
 
Hapo ndiyo nakuona una ubishi wa kipumbavu, Zitto alifukuzwa akakimbilia mahakamani ndiyo maana nikakuambia alikuwa Mbunge wa Mahakama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mbwiga Zitto angefukuzwa ubunge wake ungekoma automatically kama wa Sophia Simba.

Zitto alijiuzulu ubunge na itabaki hivyo katika cv yake...... kama hutaki kanywe debe zima la mbege kwa hasira.

Nyie Bavicha tangu aondoke Shonza mnafeli sana!
 
Hapana.

Watakuwa wamejivunjia heshima kumwacha mtu kama huyo kwa sababu yoyote ile. Ni lazima wasimame kwenye 'principles' waziaminiazo kama chama.
Mku hivi unajua "Prudence" works much better than "Principles"? However, silence is also an answer.
 
Mku hivi unajua "Prudence" works much better than "Principles"? However, silence is also an answer.
I am bound to disagree on both aspects: 'prudence' versus 'principle'; and "silence" being an answer based on philosophical argument.
 
cutelove, Viongozi wa CHADEMA badala ya kulaumu viongozi wanaokihama chama, na wengi wao mliwaamini, ni wakati mwafaka wa kutafuta mchawi ndani ya chama.
Hakuna mchawi chadema chama kiko imara sana na huyo gugu ametambua ndo maana kahama.
 
Wamsimfukuze wataingia mtegoni mwake,komu anatafuta sababu ya kufukuzwa
 
cutelove, Viongozi wa CHADEMA badala ya kulaumu viongozi wanaokihama chama, na wengi wao mliwaamini, ni wakati mwafaka wa kutafuta mchawi ndani ya chama.
Ndani ya chama hawana mchawi bali mlozi tu. Mlozi wao weshamtambua kuwa ni ccm. Inawaloga na fweza tu
 
Chadema inaweza kufanya mambo mawili.
1.kumuacha aendelee na ubunge wake ndani ya chadema huku akizuiwa kushiriki vikao vyote vinavyo ihusu kuijenga chadema, kutompa ruhusa kufanya mikutano na wananchi wa jimbo lake kwa nembo ya chadema . Njia hii ni kuhakikisha anakosa ushirikiano toka kwenye chama moja kwa moja na kwa wananchi kwa kunyimwa ridhaa nachama kuonana na wananchi wake

2. Kufukuzwa uanachama, jaribio la hapo juu likifeli ama likionesha halina mafanikio yaliyokusudiwa njia ya mwisho kumfukuza uanachama.

DUMU KUBWA
 
DUMU,
1.Atafanya mikutano na wananchi kwa ticket ya ubunge wake.

2. Komu kaitega chadema mtego mgumu sana naamini mwisho mzuri baina yao itakuwa ni salama kwa pande zote mbili yeye na chadema.
 
Kwa kauli alioitoa maamuzi magumu yakitolewa na CHADEMA sawa wala asilalamike, bora angekaa kimya tu wakati moyoni anajua anawaza nini
 
Nimeona ndugu Antony Komu ameachana na Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na malengo yake ni kuhamia NCCR MAGEUZI baada ya kumaliza kipindi chake cha ubunge baada ya bunge kuvunjwa , je chadema mnasuburia nini kwa nini msimfukuze ili akose uhalali (regitimacy) ya kuwepo bungeni ili na kiinua mgongo kipeperuke?

Mfano mkiitisha kikao cha wabunge wanaotokana na Chama chenu je atahudhuria au hatahudhuria?

Je mchango wake katika Chama bado upo?
 
Hamsomeki. Wakisema wanaondoka baada ya muda wao mnakuja na nyuzi hizi wakiondoka kabla wamenunuliwa...dah...
 
Hata kama watataka kumfukuza hawatafanya hivyo mpaka wapate ruzuku ya miezi iliyobaki
Ufipa maisha magumu sana
 
It takes two to tango!

Kama wakimfukuza ili akose kiinua mgongo, na CHADEMA pia itakosa sehemu ya ruzuku kwa sababu wabunge wake watapungua!

Mbowe ''anavyopenda pesa'' sioni kama ataweza kujipiga risasi mguuni!
 
Umuofia kwenu wakuu.

Nimekuwa na wakati mgumu sana kufikiria uamuzi wa bwana huyu, kutangangaza hadharani kuwa atakihama chama kinachompa dhamana pindi tu muda wake wa kuwa Mbunge utakapoisha.

Nikawaza inawezekana vipi, kwa sasa aendelee kuwa mwanachama kwa misingi ipi, labda wakongwe mnisaidie hii imekaaje kama ni kisheria au utaratibu kulingana na muda uliobaki.

Ninachofahamu mimi, bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa hana sifa ya kuwa mbunge, na hivyo kumfukuza uanachama ni kumfutia ubunge wake.

Siamini kama hajacalculate hili, anazo sababu au kinga kiasi cha kuwa amajeridhisha haitakula kwake, ameamua kushiba kisha kwa jeuri anamtambia baba yake mlishi.

CHADEMA mnajua cha kufanya kwa uzito wa fedheha hii, labda kama kuna hasara chama kitaingia kwa kufukuzwa kwake, napendekeza afutiliwe mbali ili mboga na ugali vyote vimwagike.

Kama mbwai na iwe mbwai bwashee.
 
Ncha Kali,
Hakuna kitu kibaya duniani kama kukataa ukweli hata kama unakukabili. Siyo siri kuwa CHADEMA kuna matatizo makubwa na hii imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi sasa.

Kukataa ukweli huo haukusahihishi mapungufu ndani ya chama hicho na mwishowe chama chetu kitukufu kitabakia ni chama cha matukio na kesi zisizokuwa na miguu.
 
Hakuna kitu kibaya duniani kama kukataa ukweli hata kama unakukabili.
Siyo siri kuwa CDM kuna matatizo makubwa na hii imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi sasa. Kukataa ukweli huo haukusahihishi mapungufu ndani ya chama hicho na mwishowe chama chetu kitukufu kitabakia ni chama cha matukio na kesi zisizokuwa na miguu.

Jielekeze kwenye mada bwashee, jenga hoja acha kuongea mafumbo hapa... una maana gani..?
 
Kumfukuza ni kumpa Kiki isiyo ya lazima kiasi ccm wataona wamefanikiwa kuwaumiza Chadema.

Dawa ni kumwacha aendelee kujiahangaikia.
 
Back
Top Bottom