KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Nashangaa hukumwona mtani wako maarufu, ambaye habari yako hii kwa mara ya kwanza kakosa neno la kukwambia, kabaki akicheka tuu! Ikiwa alama kwamba hili limechoma penyewe hasa panapouma.Mungu wabariki Wazungu
Hata kama ni bure lazima mlipie kodi hahahaha hiyo ni biashara ya Mbowe hahaha
Tuliwaeleza tokea zamani, siasa sio mikutano pekee; kuna njia mbalimbali za kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Tuweke matumaini wananchi wataanza kusikia mliyo nayo ya kuwaambia, na hasa kuhusu huu uchaguzi wa Oktoba.
Litakuwa kosa kubwa sana kwa wananchi kumpa Magufuli ngwe nyingine kwa kura nyingi zaidi na wabunge wengi zaidi.
Hiyo kwake itakuwa ni ishara kwamba akaze uzi zaidi kunyima haki za yeyote asiyekubaliana naye.
Na hakika atakuwa na haki hiyo kama wananchi watamchagua kwa asilimia sitini na kumpa wabunge zaidi ya asilimia hamsini.