CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Wapo watu waliojiweka mkao wa kula 2020, kumbuka hata Mzee Lowassa alidandia jahazi na kumpiga kikumbo Dr. Slaa lakini mwisho wa siku haikuwa vile alitaka iwe.
Hebu jibu hili swali Kada Mwenzangu "wangeshiriki unadhani nani angenufaika??"
 

Msipate shida, Tiss wapo na nyie wapambe mpo, anzisheni chama mnachotaka kama mnaona hivi vyama vibaraka vilivyopo havina mvuto. Lakini wananchi tunajitambua hatuko tayari tena kushiriki siasa na chaguzi za kishenzi.
 
Hebu jibu hili swali Kada Mwenzangu "wangeshiriki unadhani nani angenufaika??"
Mkuu, ungepeda niseme wananchi, lakini nashindwa kutumia hilo neno. Maana kama wanufaika wangekuwa ni wananchi, wasingetumia uwamuzi ambao sio wa kidemokrasia wa kususa uchaguzi.

Wanufaika wapo na wanajijua, kitendo hichi cha kujitoa kinapunguza nguvu kwa yeyote alitetegema madiwani au wenyeviti wa mitaa na vijiji kujenga hoja kwa wanachama au hata wananchi kwa ujumla ili kuvuka 2020.
 
Mwananchi wa kawaida ni lazima atoe ushirikiano kwa serikali ya mtaa kwa sababu vinginevyo anaweza kujikwamisha katika kutimiza mambo yake muhimu.

Mabwanyenye ndio aghalabu kutumia Huduma za serikali ya mtaa kwani wenyewe wana consultants na mawakala katika kila jambo hata jumuiya hawasali lakini Kanisani wanakaa viti vya mbele kabisa.

Inawezekana kukawa na uonezi kweli katika maeneo fulani ya uchaguzi lakini kule uswahilini kutotoa ushirikiano kwa serikali yako ya mtaa ni jambo ambalo haliwezekani.

Tusidanganyane

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii inanikumbusha hata 2015 walikataa matokeo na kutokumtambua JPM, matokeo yake wakajikuta hata shughuli zao za kawaida za bungeni na nje ya Bunge zinakwama. Kwenye siasa za vyama vingi huwezi kuikwepa serikali, ni lazima utashirikana nayo utake usitake.
 
Msipate shida, Tiss wapo na nyie wapambe mpo, anzisheni chama mnachotaka kama mnaona hivi vyama vibaraka vilivyopo havina mvuto. Lakini wananchi tunajitambua hatuko tayari tena kushiriki siasa na chaguzi za kishenzi.
Mnalaumu mtu asie na hatia, siku postmortem ikifanywa mtakuja kuona ukweli uko wapi.
 
Kiukweli mi sijapendezwa na Hali ya mambo ilivyo , wangewaacha Tu wapinzani na sio kuwanyanyasa kias hiki, Mbowe amefanya maamuzi Bora Sana kuwah kutokea, JPM namkubali Ila Kwa hili totaly wrong
 

Ukombozi wa nini unazungumzia wewe???!!!
 
Ni maamuzi sahihi 💯
Mmewatendea haki Wananchi
Huu ndio Upinzani
Safari ya Kuipigania Demokrasia ndio imeanza kama viongozi wa upinzani ndio mnakuwa imara zaidi.
Tutafika ng'ambo ile yenye matumaini
 
Mbowe ni mwanaCCM damudamu alipandikizwa kufanya mission ya kuipandisha na kuiua CHADEMA amefanikiwa maana Chadema itaenda Makumbusho kama CuF, NCCR MAGEUZI
 
Mbowe ni mwanaCCM damudamu alipandikizwa kufanya mission ya kuipandisha na kuiua CHADEMA amefanikiwa maana Chadema itaenda Makumbusho kama CuF, NCCR MAGEUZI
Kafunge viatu vya watawala wezi huna lolote la maana.Mrema na Cheyo jee wamevinyanyua vyama vyao?
 
Kwani hata ikifa wewe nini kinakuwasha?kama mmebaki peke yenu machozi ya nini!au mtakosa buku 7 za bando?

Naona baada ya majahili wa CCM kuharibu na kuutia najisi uchaguzi wa serikali za mitaa, wanafanya juhudi za ziada za kutakatisha uovu wao!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…