GE2025 CHADEMA yalaani askari magereza kumsukuma mwenyekiti Tundu Lissu

GE2025 CHADEMA yalaani askari magereza kumsukuma mwenyekiti Tundu Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
1753944583009.png
​
TAARIFA KWA UMMA​
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapaza sauti kwa hasira na huzuni kubwa kulaani vikali kitendo cha kinyama na kisicho cha kibinadamu kilichotekelezwa na askari wa magereza, ambaye alimshambulia kwa kumsukuma kwa nguvu na kumuangusha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Tundu Lissu, wakati akitoka katika viunga vya Mahakama ya Kisutu.

Tukio hili limetokea baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini kwa mara nyingine tena, ambayo sasa imepangwa kutajwa tena tarehe 13 Agosti 2025.

Hili si tukio la kawaida. Ni tukio la kikatili, la kushtua, na linalodhalilisha utu wa binadamu. Ni hatari zaidi kwa kuwa limefanywa na mtu ambaye, kisheria, anapaswa kuwa mlinzi wa sheria, haki, ulinzi, na usalama wa raia wakiwemo wale wanaokabiliwa na kesi mahakamani ambao bado wanastahili kuonekana kuwa hawana hatia hadi itakapothibitishwa vinginevyo na vyombo vya sheria.

Ni muhimu kuwakumbusha Watanzania wote kwamba Mwenyekiti, Mheshimiwa Tundu Lissu, bado anaendelea kuishi na ulemavu wa kudumu uliotokana na kupigwa risasi 16 katika jaribio la mauaji la Septemba 7, 2017. Kwa msingi huo, aina yoyote ya ukatili dhidi yake si tu kwamba ni kinyume cha sheria, bali pia ni tishio la moja kwa moja kwa maisha yake.

Chadema inatoa wito mzito kwa Mahakama ya Tanzania, kama mhimili huru wa utoaji wa haki, kuhakikisha kuwa tukio hili linachunguzwa kwa kina, na hatua za haraka na wazi zinachukuliwa dhidi ya waliohusika, bila kujali wadhifa wao. Tukio la ukatili ndani ya maeneo ya Mahakama linaathiri taswira ya Mahakama kama kimbilio la haki, na linatishia uaminifu wa wananchi kwa mfumo wa utoaji haki nchini.

Imetolewa leo Almamisi, 31 Julai 2025
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

Pia soma: VIDEO: Askari Magereza wamsukuma Lissu kidogo aanguke Kizimbani wakati akiaga Mahakamani​
 
1753869023486.png

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani tukio la kusukumwa kwa mwenyekiti wake, Tundu Lissu na askari wa Magereza baada ya kesi ya uhaini inayomkabili kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu Dar es Salaam.

Video za tukio hilo zilizosambaa mitandaoni Agosti 13, 2025 zilimwonyesha Lissu akiwapungia mkono wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamehudhuria mahakamani hapo na ndipo askari Magereza waliokuwa wamemzunguka walimwondoa na kumsukuma.

Video: Askari Magereza wamsukuma Lissu kidogo aanguke Kizimbani wakati akiaga Mahakamani

Taarifa iliyotolewa leo Julai 31 na Mkurugenzi wa Mawasiiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia imesema kitendo hicho ni cha kinyama na kisicho cha kibinadamu kilichotekelezwa na askari wa Magereza, ambaye alimshambulia kwa kumsukuma kwa nguvu na kumuangusha.

“Hili si tukio la kawaida. Ni tukio la kikatili, la kushtua, na linalodhalilisha utu wa binadamu. Ni hatari zaidi kwa kuwa limefanywa na mtu ambaye, kisheria, anapaswa kuwa mlinzi wa sheria, haki, ulinzi, na usalama wa raia wakiwemo wale wanaokabiliwa na kesi mahakamani ambao bado wanastahili kuonekana kuwa hawana hatia hadi itakapothibitishwa vinginevyo na vyombo vya sharia.

“Ni muhimu kuwakumbusha Watanzania wote kwamba Mwenyekiti, Mheshimiwa Tundu Lissu, bado anaendelea kuishi na ulemavu wa kudumu uliotokana na kupigwa risasi 16 katika jaribio la mauaji la Septemba 7, 2017. Kwa msingi huo, aina yoyote ya ukatili dhidi yake si tu kwamba ni kinyume cha sheria, bali pia ni tishio la moja kwa moja kwa maisha yake,” imesema taarifa hiyo.

Chama hicho kimeitaka Mahakama ya Tanzania kulichunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua waliohusika.

7a489c5a-11b7-4ae8-87cd-c25ffc22b145.jpg
 
View attachment 3425524

View attachment 3425536
Hao askari magerereza wanaovaa matambara nyusoni ni Wazanzibari wameletwa kwa kazi maalum ya kumuangamiza Lissu, Samia ni mwanamke katili sana.
 
Yule mkulima aliyemalizana na mkuu wa mkoa na kumtupa kituo Cha polisi sikuhizi watu wa hivyo hawapo?
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Au siyo!!..umetema sumu mwenyewe hapo,umepata nafuu
Nafuu itapatikana siku ubao ukigeuka sasa hivi mnajiona mko salama sana, hata Polepole enzi zake naye alijiona yuko salama leo hii anaishi kama digidigi, yana mwisho haya .
 
Hivi ni vitisho kutoka kwa walamba asali yaani ni waroho kwelikweli,wapo tayari kufanya chochote ili wasibugudhiwe.Inaonekana kila tukio ni maelekezo.
 
Back
Top Bottom