hiyo ya kuogopa bendera ni kali sana. ni hatua moja mbele baada ya CCM kuogopa uchaguzi hadi kupora uchaguzi wa wenyeviti wa vijijiHah hah hah! Nafurahi sana ninapoona CCM wanaogopa hadi bendera. Hah hah. Safi sana Mkurugenzi. Unatupatia kick Kali!
Mhh...... Sawa ndugu..... Japo mi sijashuhudia kitu kama hicho huku kwetu....Chama gani chenye maamuzi juu ya vyombo vya dola? Nilichosema sijabahatisha kwani huo uhayawani ulifanyika kote nchini kwenye chaguzi za marudio.
Mhh...... Sawa ndugu..... Japo mi sijashuhudia kitu kama hicho huku kwetu....
If it was so....... Hawakufanya fair kabisaSina shaka na kitu ninachokisema.
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.
Bendera hizo ziliwekwa katika barabara hiyo takribani wiki mbili zilizopita ulipoanza uchaguzi wa mabaraza ya chama hicho. Mkutano mkuu wa chama hicho kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti utafanyika kesho Jumatano Desemba 18, 2019.
Katika barua hiyo ya leo Jumanne Desemba 17, 2019 kwenda kwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji ambayo Mwananchi imeona, mkurugenzi huyo amesema manispaa ya Ubungo ndio inayoihudumia barabara hiyo inashangazwa kuona bendera za chama hicho zikiwa kwenye bustani.
Dominic amesema bendera zimewekwa kama matangazo kinyume na utaratibu wa kibali.
"Kwa barua hii nakutaarifu kuwa unatakiwa uondoe bendera hizo ndani ya muda wa saa mbili baada ya kupokea barua hii. Agizo hii lisipotekelezeka bendera hizo zitaondolewa kwa utaratibu mwingine," inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Meya wa Ubungo ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Boniface Jacob alipoulizwa kuhusu agizo hilo la mkurugenzi amesema, “bendera hizo haziondolewi kwa sababu Chadema tuna haki ya kutumia maeneo ya wazi ya umma kama vyama vingine vya siasa kwa mujibu wa sheria.”
Chanzo: Mwananchi
===
MWENDELEZO
Polisi wamefika eneo la Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar unapofanyika Mkutano wa CHADEMA na kuagiza bendera za chama hicho zilizowekwa kushushwa
Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alikiandikia barua chama hicho kikuu cha Upinzani Nchini kutaka kishushe bendera hizo
Sheria za miji matangazo yanayolipiwa ni ya kwenye hifadhi za barabara. na Chadema kama hawana pesa ya kulipia wangeenda kutundika bendera vyooni kukwepa sheria.Tumekuwa tukishuhudia wakati wa vikao vya CCM bendera zikitundikwa hata "vyooni" mbona hatujawahi ona maagizo ya aina hiyo ya kuzishusha bendera zao kwa masaa mawili?
Tunaomba pia utujulishe je uwepo wa Chadema siyo halali kwa mujibu wa msajili wa vyama vya kisiasa nchini?
Lakini mnachoshau nyinyi CCM ni kuwa hakuna chenye mwanzo hapa duniani kikakosa kuwa na mwisho!
Mrejesho hizo bendera zingalipo badoAtafutwa kazi kama CAG
Elimu zenyewe ndo hizi za Newton's law ambazo mwenyekiti wa kavazi la Mwl Nyerere anaipiga madongo?Nchi hii ina wajinga wengi sana ingawa wameenda shule
If it was so....... Hawakufanya fair kabisa
Zina umuhimu gani wa kupachikwa?
Mm ni mshabiki wa hii awamu ya tano japo sio mdau wa chama chochote kile...... Mambo mengi yafanywayo na serikali nakubaliana nayo lakini kuna mengine hasa haya ya siasa za vyama siyaungi mkono.... Sema ndo politics zenyewe...... Ukizifikiria sana zinaumiza kichwa.....They don't care as this is their new winning approach.
Mkuu 'Retired', nafahamu mahakama ya CCM iliukataa huo ushahidi.Ushahidi kama huu ulitolewa mahakamani majaji wa rufaa wakaukataa, hivyo hata ukauweka leo, kesho sidhani kama unasaidia. Lakini ni vema kuuweka. Tatizo kubwa ni mahakama zetu (judiciary) na majaji wa UPE akina.... and Co. Ltd!
Hapa, hizi sio 'politics' kwa aina yoyote ile. Huu ni uonevu, na siasa sio kuoneana kwa kutumia vyombo vinavyotakiwa kusimamia haki kwa yeyote bila kujali 'politics' anayoiamini.Mm ni mshabiki wa hii awamu ya tano japo sio mdau wa chama chochote kile...... Mambo mengi yafanywayo na serikali nakubaliana nayo lakini kuna mengine hasa haya ya siasa za vyama siyaungi mkono.... Sema ndo politics zenyewe...... Ukizifikiria sana zinaumiza kichwa.....
Kazi kwenu itakuwa kwenda kuwatoa ujinga waTanzania wanaoaminishwa kwamba tuna vita na 'mabeberu'. Maana yake ni kwamba, kuonekana ukiwa karibu na 'beberu' wakati huu ni kujiongezea kazi ya kutoa ujinga kwa sehemu kubwa ya raia wanaoamishwa ujinga huo.Kesho Mkutano Mkuu , tumealika mabeberu wote .