CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Hah hah hah! Nafurahi sana ninapoona CCM wanaogopa hadi bendera. Hah hah. Safi sana Mkurugenzi. Unatupatia kick Kali!
hiyo ya kuogopa bendera ni kali sana. ni hatua moja mbele baada ya CCM kuogopa uchaguzi hadi kupora uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji
 
Bendera za upinzani zikipepea zina madhara yapi kwa serikali iliyopo madarakani?
 
Hata hiyo jamani bendera la Chadema linamvuto sana hata rangi za mavazi au sare zake inapendeza sana
 
Chama gani chenye maamuzi juu ya vyombo vya dola? Nilichosema sijabahatisha kwani huo uhayawani ulifanyika kote nchini kwenye chaguzi za marudio.
Mhh...... Sawa ndugu..... Japo mi sijashuhudia kitu kama hicho huku kwetu....
 
waambie waje waondoe na hizi huku
1576668512443.png
 
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

Bendera hizo ziliwekwa katika barabara hiyo takribani wiki mbili zilizopita ulipoanza uchaguzi wa mabaraza ya chama hicho. Mkutano mkuu wa chama hicho kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti utafanyika kesho Jumatano Desemba 18, 2019.

Katika barua hiyo ya leo Jumanne Desemba 17, 2019 kwenda kwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji ambayo Mwananchi imeona, mkurugenzi huyo amesema manispaa ya Ubungo ndio inayoihudumia barabara hiyo inashangazwa kuona bendera za chama hicho zikiwa kwenye bustani.

Dominic amesema bendera zimewekwa kama matangazo kinyume na utaratibu wa kibali.

"Kwa barua hii nakutaarifu kuwa unatakiwa uondoe bendera hizo ndani ya muda wa saa mbili baada ya kupokea barua hii. Agizo hii lisipotekelezeka bendera hizo zitaondolewa kwa utaratibu mwingine," inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Meya wa Ubungo ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Boniface Jacob alipoulizwa kuhusu agizo hilo la mkurugenzi amesema, “bendera hizo haziondolewi kwa sababu Chadema tuna haki ya kutumia maeneo ya wazi ya umma kama vyama vingine vya siasa kwa mujibu wa sheria.”


Chanzo: Mwananchi
===


MWENDELEZO
Polisi wamefika eneo la Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar unapofanyika Mkutano wa CHADEMA na kuagiza bendera za chama hicho zilizowekwa kushushwa

Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alikiandikia barua chama hicho kikuu cha Upinzani Nchini kutaka kishushe bendera hizo

KAMA NI UCHAFU ONDOENI NA UCHAFU HUU HAPA ZINAKESHA HUU MWAKA WA 3 ZIKO HAPA NA MNAZIPITA KILA SIKU JE HAZIWASUMBUIII... ILA ZILEEE ZA CHAMA KUBWA NDO SHIDA.. HAMLALI NA HAMTOPATA USINGIZI.
1576668546131.png
 
Tumekuwa tukishuhudia wakati wa vikao vya CCM bendera zikitundikwa hata "vyooni" mbona hatujawahi ona maagizo ya aina hiyo ya kuzishusha bendera zao kwa masaa mawili?

Tunaomba pia utujulishe je uwepo wa Chadema siyo halali kwa mujibu wa msajili wa vyama vya kisiasa nchini?

Lakini mnachoshau nyinyi CCM ni kuwa hakuna chenye mwanzo hapa duniani kikakosa kuwa na mwisho!
Sheria za miji matangazo yanayolipiwa ni ya kwenye hifadhi za barabara. na Chadema kama hawana pesa ya kulipia wangeenda kutundika bendera vyooni kukwepa sheria.
 
Chadema muonee huruma mkurugenzi ana familia shusheni hizo bendera mwe
 
They don't care as this is their new winning approach.
Mm ni mshabiki wa hii awamu ya tano japo sio mdau wa chama chochote kile...... Mambo mengi yafanywayo na serikali nakubaliana nayo lakini kuna mengine hasa haya ya siasa za vyama siyaungi mkono.... Sema ndo politics zenyewe...... Ukizifikiria sana zinaumiza kichwa.....
 
Ushahidi kama huu ulitolewa mahakamani majaji wa rufaa wakaukataa, hivyo hata ukauweka leo, kesho sidhani kama unasaidia. Lakini ni vema kuuweka. Tatizo kubwa ni mahakama zetu (judiciary) na majaji wa UPE akina.... and Co. Ltd!
Mkuu 'Retired', nafahamu mahakama ya CCM iliukataa huo ushahidi.

Kumbuka.mtafuta haki hachoki na wala hakati tamaa.

Kuna mahakama moja tu Tanzania ambayo haihojiwi.

Mimi naizungumzia mahakama hiyo hiyo. Ndio mahakama inayohitaji ushahidi wenu ulio wazi ili itoe hukumu yake isiyohojiwa.

Ni makosa na uzembe kuamini kwamba mahakama hiyo inauona ushahidi, kwa hiyo haihitaji nyinyi muuwasilishe mbele yake. Hii ndio kazi inayowashinda sana hadi sasa. Ndio ni kazi ngumu, lakini ni kazi inayowezekana.

Nawaomba sana, shughulisheni vichwa vyenu ni jinsi gani mtakavyoweza kuufikisha ushahidi wenu huko ili hukumu itolewe.

Hii ndio kazi kubwa ninayoiandika hapa kila siku ninayowasihi muifanye kwa bidii zote bila kuchoka.
 
Mm ni mshabiki wa hii awamu ya tano japo sio mdau wa chama chochote kile...... Mambo mengi yafanywayo na serikali nakubaliana nayo lakini kuna mengine hasa haya ya siasa za vyama siyaungi mkono.... Sema ndo politics zenyewe...... Ukizifikiria sana zinaumiza kichwa.....
Hapa, hizi sio 'politics' kwa aina yoyote ile. Huu ni uonevu, na siasa sio kuoneana kwa kutumia vyombo vinavyotakiwa kusimamia haki kwa yeyote bila kujali 'politics' anayoiamini.
Kwa hiyo, mkuu 'ROBERTO', unatumia kisingizio cha 'politics' kufumbia macho unachosema hukitaki.

Just be honest with yourself.
 
Kesho Mkutano Mkuu , tumealika mabeberu wote .
Kazi kwenu itakuwa kwenda kuwatoa ujinga waTanzania wanaoaminishwa kwamba tuna vita na 'mabeberu'. Maana yake ni kwamba, kuonekana ukiwa karibu na 'beberu' wakati huu ni kujiongezea kazi ya kutoa ujinga kwa sehemu kubwa ya raia wanaoamishwa ujinga huo.
 
Back
Top Bottom