CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Petro su unauona uonevu huu
huyo Petro, muulize anashangaa nini!! huyu mama mstaarabu sana. bahati yao chadema, Bashite alikuwa busy na nec. angeagiza Mbowe aende mwenyewe kituo chochote cha polisi na kuwaambia ameambiwa na rc. angepokelewa. Petro, kama kuna uonevu ukabaki tu kushangaa unakuwa upo upande wa anayeonea. ukisikia serikali ya awamu tamu ndio hii!! ccm mbele kwa mbele. kutetea serikali ya awamu hii ni kujitoa ufahamu.
 
Kazi kwenu itakuwa kwenda kuwatoa ujinga waTanzania wanaoaminishwa kwamba tuna vita na 'mabeberu'. Maana yake ni kwamba, kuonekana ukiwa karibu na 'beberu' wakati huu ni kujiongezea kazi ya kutoa ujinga kwa sehemu kubwa ya raia wanaoamishwa ujinga huo.
Je raia wanaopata msaada wa ARV kutoka kwa mabeberu watamuaminije Mtu aliyekula hela ya TETEMEKO ?
 
Kuna watu hawana akili kabisa, CHADEMA wanamkutano wao hapo, huo mkutano haudumu hata kwa wiki 2 wanachingaika nao ni nini, wakimaliza watafungu na kuondoka, na CHADEMA wameweka bendera kwenye uzio wa ukumbi wa mkutano sio i kama ni tatizo
Mbona mibendera ya CCM inapepea hadi chooni na vichochoroni? Ujinga mwingine jamani!
 
Je raia wanaopata msaada wa ARV kutoka kwa mabeberu watamuaminije Mtu aliyekula hela ya TETEMEKO ?
Erythro., amini usiamini, wengi wa hao wanaminishwa ARV "zinapatikana kwa pesa zetu sisi wenyewe."
Huo ndio ujinga ninaokwambia watu wanauopokea bila ya kuhoji!
Usione kwa vile wewe unao uelewa wa kutosha na kupambanua mambo, ukadhani hali iko hivyo kwa wengine. Hii ni kazi mnayotakiwa kuifanya, kuwaondolea 'ujinga' watu.
 
Hapa, hizi sio 'politics' kwa aina yoyote ile. Huu ni uonevu, na siasa sio kuoneana kwa kutumia vyombo vinavyotakiwa kusimamia haki kwa yeyote bila kujali 'politics' anayoiamini.
Kwa hiyo, mkuu 'ROBERTO', unatumia kisingizio cha 'politics' kufumbia macho unachosema hukitaki.

Just be honest with yourself.
Kiufupi ndani ya siasa hasa za vyama kuna mengi.... Mazuri na mabaya....mabaya ndo hayo kama uliyoyasema..... Ndo siasa za Africa....
 
Bendera zina madhara gani? Hawa wateule wanamuaibisha Rais.
rais yupi? usimpakazie rais kipenzi cha wanyongwa. wangapi wameachiwa siku ya uhuru? Peter, kumbuka kunyamaza humaanisha kukubali. Beatrice sio anabeat rice. utaona kali yake mwakani. madiwani wote mbele kwa mbele. Boniface Jacob atapata ruhusu kwenda SA kurudi ni baada ya uchaguzi mkuu. akijidai kurudi mapema anapewa repatriation kama Miguna wa Miguna! usisahau kuwa Kabundi atalitafsiri jina lake kibiblia, yakobo=tapeli. if you want to kill a dog, give it a bad name.
 
Tatizo siyo yeye nadhani Ni uwezo wa kufikiri.

Nina uhakika wamelipia ukumbi na kupewa risti na Nina uhakika sehemu ya ukumbi lazima kupambwa ndani na maeneo ya nje .

Nina hakika huyu Mama atakuwa ameharibu biashara za watu kwa kuingilia mkutano na kuuvuruga.

Tunahitaji viongozi went uthubutu was kufikiri kabla ya kutenda na kufikiri japo kidogo kabla ya kuzungumza.

Poleni watanzania wenzangu mlio kerwa na hichi kitendo na nawaomba tumsamehe,maana najua Ni hofu juu ya kuachia ofisi .
 
Hivi kuna sheria yoyote ile inayohusu utaratibu wa kuweka bendera, mabango na matangazo? Kama ipo je, imefuatwa?

Niliuliza tangu jana kama kuna sheria yoyote, hili ndio tatizo kubwa Tanzania wengi wanapenda kufanya mambo kienyeji. Ningekuwa Chadema ningesema kwamba hakuna hiyo sheria au sheria iliyopo haihusiani na swala hili. Kilichobaki inatumika nguvu ya hoja wakati uwezo wa nguvu haupo.
 
HATUMFURAHISHI RAIS BALI TUNAMWARIBIA

Na Thadei Ole Mushi

Hebu Fikiria, Mahali ambapo Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa nchi amekaa na kamati kuu ya CCM Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri anaweza kutoa agizo la Bendera za Chama ziondolewe? Definitely hilo haliwezekani lakini kwa Chadema mahali ambapo Chama kikuu cha Upinzani kinakutana na kamati yake kuu na baraza kuu kwa ajili ya mkutano wake mkuu anatokea mtu tu anaamuru zitolewe.

Yeye anafikiri amekisaidia sana Chama Chetu CCM, anafikiri kwa kufanya Hivyo kamfurahisha sana Rais wetu. Hili ni kosa la kimkakati kabisa.

Katika kipindi kama hiki ambacho Chadema inafuatiliwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa katika uchaguzi wake tunawapa political mileage, tunawapa agenda, tunawapa justification ya wao kuonewa je hivi ndivyo tunavyoijenga CCM?

Katika kipindi kama hiki taifa linapotaka maridhiano ya Kisiasa vijana wa ngazi za chini bila kutumwa na mtu yeyote anaamua kupanda mbigiri Mpya kwa taifa letu. Anaamua kuleta mitafaruku isiyokuwa ya Lazima kwa taifa letu.

Wakati binti Akwilina akipigwa Risasi kabla yalitoka maamuzi ya kipuuzi na yasiyo na weledi kama Haya kuwa chelewesheni Barua za mawakala. Zile barua zingewahi Chadema wasingeandamana na CCM bado ingelishinda. Tumekaa mahali na familia zetu tunajiandaa kwa Xmass wakati Binti asiyekuwa na Kosa akiwa Kaburini anaendelea Kuoza. Tunajifariji kila upande kuwa Hatujui aliyerusha ile Risasi lakini tunajidanganya kwa kuwa Mungu anajua kila kitu.

Wakati Spring Revolution inaanzia Kule Tunisia na kusambaa maeneo Mengine ya North Afrika Tunisia ilikuwa kimya na Tulivu kabisa. Ben Ali alikuwa zake Ikulu na mambo yalikuwa yakienda kama kawaida Kosa la Askari wawili tu kumpiga vibao kijana Bouaziz kilitosha kuleta machafuko Makubwa na kusambaa hadi nchi nyingine. Hawa Askari hawakutumwa na Ben Ali walijiamulia tu kwa kufikiri wanamfurahisha Rais.

Umoja, Mshikamano hauletwi na Maamuzi ya aina hii.

Niwaambieni tu CCM kuwa Upinzani na hatari kubwa ya Chama chetu haupo njee ya CCM Bali upo ndani ya CCM. Chama changu hakijafikia kuogopa hadi Bendera.

Anyway Ngoja nirudi jalalani....

Ole Mushi.
0712702602
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama changu hakijafikia kuogopa hadi Bendera.

Anyway Ngoja nirudi jalalani

😂😂😂😂😂
Lazima muogope hadi bendera, chezea kukataliwa wewe. Kukataliwa kubaya sana.
CCM ya Magufuli imekataliwa Tanganyika na Zanzibar, mbinguni na duniani.
 
Niliuliza tangu jana kama kuna sheria yoyote, hili ndio tatizo kubwa Tanzania wengi wanapenda kufanya mambo kienyeji. Ningekuwa Chadema ningesema kwamba hakuna hiyo sheria au sheria iliyopo haihusiani na swala hili. Kilichobaki inatumika nguvu ya hoja wakati uwezo wa nguvu haupo.
Wangekujibu sheria ipo au haipo wewe ingekusaidia nini?

Hapana, sio wewe tu, hata wao ingewasaidia kitu gani?

Unauliza swali ambalo jibu lake tayari unalo, hapo unatafuta majibu ya kihuni kama hili.

Samahani sana lakini...
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Wangekujibu sheria ipo au haipo wewe ingekusaidia nini?

Hapana, sio wewe tu, hata wao ingewasaidia kitu gani?

Unauliza swali ambalo jibu lake tayari unalo, hapo unatafuta majibu ya kihuni kama hili.

Samahani sana lakini...

Mkuu mimi sipo Tanzania nilikuwa nataka kufahamu kama sheria ipo au hakuna. Anyway kwa sababu umefanya judgement tayari na inaonekana hakuna anayefahamu kama kuna sheria au la. Hatari sana. Shukrani kwa kunifahamisha. (Utawala wa Sheria)

BTW UK ukitaka kuweka tangazo kwenye nguzo za umeme barabarani au kwenye nguzo zako lazima upate kibali na unalipia kiasi flani cha pesa na muda matangazo yako yatakapokuwa barabarani. Hata ukitaka kupeperusha bendera nk Fees zipo categorised kufuatana na sheria zao.
 
Back
Top Bottom