CHADEMA yawasha moto Arusha. Mbowe azindua Mkakati mpya

makamanda kila la kheri tupo nyuma yenu
 
JPM angeua chama. Tushukuru Mungu. Shukrani kwa SSH kukomboa vyama vyote nchini
chaguzi zote zote ccm imepata zaid ya aslimia 80 unasema angeua chama. subiri uine 2025 uone kama watapata hizo kura
 
Mwamba kama Mwamba yaani
 
Huyu jamaa unampa ushauri na kukuomba ni mwanamke aumwanaume isije kuwa ni Kimara sasa life imechange haletewi matumizi
 
Aje na huku kanda ya ziwa tunamhitaji sana Kamanda,yuko kimya sana
 
Huyu jamaa unampa ushauri na kukuomba ni mwanamke aumwanaume isije kuwa ni Kimara sasa life imechange haletewi matumizi
Tuendelee kumuombea yeye na wa aina yake wapone.
Pia wale wenzetu waliyoshiriki kwa nguvu zote kuifukuza corona kwa maombi, wangeongeza uzalendo wao katika hili.
 
Chadema Kama chama cha upinzani mmesahau kuwasemea wananchi na kero zao mbalimbali Kama maji, ardhi, elimu, miundo mbinu, umeme, ajira, rushwa na ufisadi badala yake mmejikita kudai Mambo ambayo wananchi hawaoni Kama ni changamoto kubwa kwao.

Katiba, haki za binadamu na Uhuru wa habari siyo kero kubwa kwa watanzania waliyo wengi, hizo ni kero kwa watu wachache (wanasiasa, waandishi wa habari, wanasheria na NGOs zinazohusika na haki za binadamu).

Wananchi wa vijijini kwa mfano kero zao kubwa ni maji, barabara, umeme, pembejeo za kilimo, masoko ya mazao yao, huduma za Afya, miundo mbinu ya elimu n. K

Kama kweli mna nia ya kurejesha ushawishi kwa wananchi walio wengi, mikutano yenu ijikite kuongelea kero zinazowagusa wananchi walio wengi. Tatizo la Chadema ni kwamba mmejikita zaidi mtandaoni (Twitter na Jamii forum) ambako mnahisi uungwaji mkono mnaopata kule ndiyo picha halisi ya nchi nzima, mnasahau watumiaji wa mitandao hiyo hawazidi hata robo ya wapiga kura wote nchini, na wapiga kura wengi wapo vijijini.

Rudisheni Chadema ya kipindi cha Dr. Wilbroad Slaa iliyokuwa na mvuto kwa watanzania wa rika zote, Chadema iliyochallenge serikali katika maswala yanawagusa wananchi direct.
 

Kwa taarifa yako cdm wanaungwa mkono na wote wanaojitambua, hayo unayosema watu wengi ni propaganda unazobeba huko ccm. Hakuna siku cdm hawakuacha kuzungumzia hizo kero za maji, barabara nk. Na iwapo uchaguzi ungekuwa wa haki ungejua kiwango cdm wanachoungwa mkono na wananchi. Sasa unaposema unataka cdm waungwe mkono na wananchi, halafu kipimo cha kuungwa mkono ambacho ni uchaguzi kinanajisiwa, unataka mpaka machafuko yatokee ndio uelewe?
 
Washeni moto Uchagani, kwa nini munakimbilia Arusha??? Mukitoka huko munajidai kanda ya ziwa, mukigawa madaraka munarudi Moshi. NO!
 
Kuna mtoto mmoja alikuwa analilia pipi huku akitia huruma, na watu walimuonea huruma. Kuna wakati hunyamaza na kucheka na kupiga story, welevu walijiuliza maswali kwa mini hulia sana na ghafla wakati mwingine hunyamaza? Baadaye wakagundua kwamba kumbe wale wenye pipi wanaposikia kilio kimezidi hudondosha pipi na yeye akiokota hunyamaza. Na wala hawaambii waliomhurumia kwamba huwa anaokota pipi zilizodondoshwa. Kwa hiyo akajikuta akikosa thamani polepole.
UTAKUWA NA THAMANI TU UKISIMAMIA UNACHOKIAMINI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…