CHADEMA yawasha moto Arusha. Mbowe azindua Mkakati mpya

CHADEMA yawasha moto Arusha. Mbowe azindua Mkakati mpya

Kwa taarifa yako cdm wanaungwa mkono na wote wanaojitambua, hayo unayosema watu wengi ni propaganda unazobeba huko ccm. Hakuna siku cdm hawakuacha kuzungumzia hizo kero za maji, barabara nk. Na iwapo uchaguzi ungekuwa wa haki ungejua kiwango cdm wanachoungwa mkono na wananchi. Sasa unaposema unataka cdm waungwe mkono na wananchi, halafu kipimo cha kuungwa mkono ambacho ni uchaguzi kinanajisiwa, unataka mpaka machafuko yatokee ndio uelewe?
Tatizo la Chadema ni kushupaza shingo hata mnapoambiwa ukweli, nyie endeleeni na hizo harakati zenu za kudai katiba mpya na haki za binadamu muone Kama zitawafanya mshike Dora.

Kwa mfano ishu za ufisadi ilikuwa ni ajenda mojawapo iliyowapaisha Sana kipindi cha Dr. Slaa, toka mmkaribishe Lowasa mliyemwita fisadi na kumsafisha kuwa hana hatia, neno ufisadi ikawa siyo ajenda yenu tena.

Rejeeni ajenda mlizotumia kipindi cha Dr. Slaa mpate uungwaji mkono nchi nzima, vinginevyo mtaendelea kuwa chama Cha upinzani kwa miaka 50 ijayo.
 
Mguu sawa! makamanda songeni mbele na msikate tamaa. Mlifanyiwa dhambi mbaya sana ktk chaguzi zote za awamu ya 5. ILA mshahara wa dhambi ni mauti
 
Uko na marking scheme?

mnakwamaga wapi kujibu maswali madogo, we ukiwa maskini usianze toa visingizio wakati wengne wameweza bana au mpaka lissu awe prezida ndo utatoka kimaisha 😂
 
Tatizo la Chadema ni kushupaza shingo hata mnapoambiwa ukweli, nyie endeleeni na hizo harakati zenu za kudai katiba mpya na haki za binadamu muone Kama zitawafanya mshike Dora.

Kwa mfano ishu za ufisadi ilikuwa ni ajenda mojawapo iliyowapaisha Sana kipindi cha Dr. Slaa, toka mmkaribishe Lowasa mliyemwita fisadi na kumsafisha kuwa hana hatia, neno ufisadi ikawa siyo ajenda yenu tena.

Rejeeni ajenda mlizotumia kipindi cha Dr. Slaa mpate uungwaji mkono nchi nzima, vinginevyo mtaendelea kuwa chama Cha upinzani kwa miaka 50 ijayo.

Sioni hata kama unajua unachokiongea. Kwanza ufisadi sio ajenda, labda urudi kwanza shule ujifunze ajenda ni nini. Na isitoshe wapiga kura wengi wa Tanzania hupiga kura kwa hamasa, ushabiki, rushwa, hofu na sababu nyingine kabisa nje ya hizo unazosema ni ajenda, na sehemu kubwa udhaifu wa tume ya uchaguzi ndio huamua mshindi na sio wapiga kura. Kama neno ufisadi lilikuwa tatizo na Lowassa ndio alikuwa fisadi Mkuu, asingepata kura 6m+ huku rais aliyemshinda kwa utata akiwa na 8m+. Ww ni bendera fuata upepo na wala lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani.

Kama hujui umuhimu wa katiba mpya kuleta mabadiliko kwenye hayo mambo ya maji, umeme nk, basi utakuwa hujui lolote kwenye unalotetea ama kutoa ushauri hapa.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , leo kimeanza kupanga mipango mipya ya kukisogeza karibu zaidi na Wananchi , ambapo Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe ameanza kwa kufungua kikao cha Kamati ya Utendaji Mjini Arusha

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, tarehe 27 Mei 2021 siku ya Alhamisi, anatarajiwa kuzindua ‘Operesheni Haki,‘ ambayo itafanyika nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021 na Chadema, kupitia ukurasa wake wa Twitter, kampeni hiyo itazinduliwa jijini Arusha.

Taarifa ya Chadema imesema kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, pamoja na uimarishwaji misingi ya haki nchini.

Sambamba na hilo, taarifa ya Chadema imesema, Mbowe ameendesha kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho, katika Kanda ya Kaskazini, kilichofanyika leo jijini Arusha.

“Leo Mei 25, 2021, Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe, ameendesha Kikao cha Kamati Tendaji ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha,” imesema taarifa ya Chadema.
Watamkumbuka Ole Sabaya.
 
mnakwamaga wapi kujibu maswali madogo, we ukiwa maskini usianze toa visingizio wakati wengne wameweza bana au mpaka lissu awe prezida ndo utatoka kimaisha 😂

Yes, ni mpaka Lisu awe rais ndio nitoke kimaisha kama Sabaya, Makonda, Bashiru, Polepole nk.
 
Sioni hata kama unajua unachokiongea. Kwanza ufisadi sio ajenda, labda urudi kwanza shule ujifunze ajenda ni nini. Na isitoshe wapiga kura wengi wa Tanzania hupiga kura kwa hamasa, ushabiki, rushwa, hofu na sababu nyingine kabisa nje ya hizo unazosema ni ajenda, na sehemu kubwa udhaifu wa tume ya uchaguzi ndio huamua mshindi na sio wapiga kura. Kama neno ufisadi lilikuwa tatizo na Lowassa ndio alikuwa fisadi Mkuu, asingepata kura 6m+ huku rais aliyemshinda kwa utata akiwa na 8m+. Ww ni bendera fuata upepo na wala lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani.

Kama hujui umuhimu wa katiba mpya kuleta mabadiliko kwenye hayo mambo ya maji, umeme nk, basi utakuwa hujui lolote kwenye unalotetea ama kutoa ushauri hapa.
[emoji23][emoji23][emoji23] Chadema mnachekesha kweli kusema ufisadi siyo Ajenda? Hivi umesahau ile LIST OF SHAME ya Mwembe yanga iliyomuhusisha Lowasa? Hivi unadhani ni kitu gani kilimtoa Dr. Slaa Chadema Kama siyo ujio wa Lowasa aliyemnadi kuwa fisadi papa baadae akapokelewa Kama mgombea wa urais?

Chadema kipindi cha Dr. Slaa mliibua ufisadi mkubwa Kama EPA, Richmond, ESCROW n.k na hiyo iliwapaisha Sana na kuwa na uungwaji mkono nchi nzima. Leo utasemaje ufisadi haikuwa Ajenda yenu?

Mabadiliko ya katiba sikatai kwamba yana umuhimu, lakini ni lazima mtambue wananchi walio wengi hawana uelewa Mpana wa hiyo katiba. Kwa hiyo hamuwezi kueleweka kirahis msiposhabihisha katiba na changamoto zao za maisha ya kila siku Kama nilivyozitaja.
 
Kwa taarifa yako hilo suala la katiba mpya linaeleweka vizuri sana, na ni hitaji la wananchi wengi japo sio wote. Kwa hiyo unataka watu wasubiri kudai katiba mpya mpaka watu wote waelewe? Wengi wa bendera fuata upepo kama ww ndio ndio mnasema watu hawahitaji katiba mpya, na sababu kubwa ya kuigomea katiba mpya ni kwakuwa mnadhani lengo la katiba ni kuitoa ccm madarakani.

Hilo la Lowassa kwenda cdm sio kila mtu anayeikubali cdm aliunga mkono, mimi hapa nikiwa mmojawapo, na ushahidi ni post zangu humu ndani, since day one alipoingia cdm.

Hiyo unayolazimisha cdm za enzi za Dr. Slaa inaonyesha huna hoja, bali hoja ulizokariri, hivyo kwa sasa unazitapika tu hapa jukwaani, na huyo Dr.Slaa angeendelea kuwa cdm enzi za Magufuli kwa hizo hoja zake, leo hii angekuwa marehemu, jela, ama na kilema cha maisha. Usitake kufananisha mambo ambayo hayaendani kutokana na nyakati.

Ufisadi sio ajenda, kama unadhani ufisadi ni ajenda, basi ingia kwenye kitabu cha itikadi ya cdm uone kama ufisadi ni ajenda, na kitabu hicho kiwe ni cha kabla ya 2015. Ufisadi ulikuwa ni hamasa na sio ajenda. Ajenda ni kama kuwa na serikali za majimbo, serikali tatu, elimu bure chekechea mpaka university nk, hizo ndio ajenda boss.
 
Back
Top Bottom