CHARLES2016
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 376
- 435
Tatizo la Chadema ni kushupaza shingo hata mnapoambiwa ukweli, nyie endeleeni na hizo harakati zenu za kudai katiba mpya na haki za binadamu muone Kama zitawafanya mshike Dora.Kwa taarifa yako cdm wanaungwa mkono na wote wanaojitambua, hayo unayosema watu wengi ni propaganda unazobeba huko ccm. Hakuna siku cdm hawakuacha kuzungumzia hizo kero za maji, barabara nk. Na iwapo uchaguzi ungekuwa wa haki ungejua kiwango cdm wanachoungwa mkono na wananchi. Sasa unaposema unataka cdm waungwe mkono na wananchi, halafu kipimo cha kuungwa mkono ambacho ni uchaguzi kinanajisiwa, unataka mpaka machafuko yatokee ndio uelewe?
Kwa mfano ishu za ufisadi ilikuwa ni ajenda mojawapo iliyowapaisha Sana kipindi cha Dr. Slaa, toka mmkaribishe Lowasa mliyemwita fisadi na kumsafisha kuwa hana hatia, neno ufisadi ikawa siyo ajenda yenu tena.
Rejeeni ajenda mlizotumia kipindi cha Dr. Slaa mpate uungwaji mkono nchi nzima, vinginevyo mtaendelea kuwa chama Cha upinzani kwa miaka 50 ijayo.