Chagua CHADEMA upate Demokrasia na maendeleo Mtaani kwako

Chama ambacho kimeoza, kinaongozwa ki-ukoo ukoo zaidi, Tanzania hatuwezi kukubali kuendelea kwenye ubaguzi wa kikanda au kikabila, mwenye macho haambiwi tazama.
 
Sasa mbona Huyo sky anasema watu waichague cdm wakati wengine mnasema hakuna atakaejitokeza kushiriki uchaguzi.
Mbona Hamna kauli moja inayofanana.
 
Watu makini, wanapojikwaa na kuanguka, hawaishii tuu kuamka, kujikunguta kujifuta vumbi, kuangalia walipoangukia, na kuendelea na safari yao, watu makini hawaangalii walipoangukia, bali hugeuka nyuma kuangalia walipojikwaa.

Angalia tarehe ya bandiko hili, kisha some kwenye bandiko nilisema nini kuhusu CCM, kisha nikasema nini kuhusu Chadema, halafu angalia CCM walifanya nini na Chadema walifanya nini.






CCM pia sikuwaacha





P
 
Sasa mbona Huyo sky anasema watu waichague cdm wakati wengine mnasema hakuna atakaejitokeza kushiriki uchaguzi.
Mbona Hamna kauli moja inayofanana.
Hii inaitwa inconsistency. Ukiwaambia wanakasirika.
P
 
Chama ambacho kimeoza, kinaongozwa ki-ukoo ukoo zaidi, Tanzania hatuwezi kukubali kuendelea kwenye ubaguzi wa kikanda au kikabila, mwenye macho haambiwi tazama.

Ni mawazo mgando kujua upinzani Ni chadema pekee wapo Cuf, AcT, Na wengine..

Figisu za huu uchaguzi mdogo Ni fundisho kwa vyama ivyo vya upinzani kuelekea ktk uchaguzi mkuu..

Kushindwa kujiandikisha/ au kususia sio sababu ya wapinzani kutetereka, muda bado upo. Inatakiwa kuwepo Uhuru wa mikutano, majukwaa na midahalo ya kisiasa ambayo italeta changamoto na hoja za maendeleo, ushauri, na mawazo mbadala hiyo ndio demokrasia ya kweli...

Upinzani wa kisiasa sio dhambi.
 

Ndio chama kikubwa pinzani vingine yama vya mfukoni au kwenye flash. Je, unataka na hivyo tuviite vyama kweli? yaani unakuta Agenda yao kubwa kuandika issues zinazopelekea Tanzania kuwa koloni la mataifa makubwa. Tusiwe na uhuru wa kujiamualia mambo yetu kama taifa.
 

Mkuu. Huwa sielewi nia yako Wakati mwingine. Unasema mshindi tayari ok. Naweza kukubaliana na wewe. Why. Huyu Unayemsifia ndo wale wapinga watu kujiandikisha. Leo anaomba kura. Nani apige kura hiyo. Kuna vichwa mpaka nashindwa elewa huko Tz taarabu itaisha lini na kazi zitaanza lini.
 
Kwa kiasi kikubwa uko sahihi, lakini vigezo vya free and fair election viko Vingi hivi kama kutoa tu fomu watendaji wanafunga ofisi, uchaguzi unakuwaje free and fair?
 
Sasa mbona Huyo sky anasema watu waichague cdm wakati wengine mnasema hakuna atakaejitokeza kushiriki uchaguzi.
Mbona Hamna kauli moja inayofanana.

Sisi sio timu useme tuna msemaji wetu, hili ni jukwaa huru kila mtu anaweza kuchangia apendacho, sisi tulioamua kwamba hatutapiga kura ni mpaka hapo itakapopatikana tume huru, ama mazingira ya kuridhisha kupiga kura msimamo wetu uko pale pale. Kuoana mawazo na mitazamo kwenye baadhi ya mambo haimaanishi tunakubaliana kwenye kila jambo au tunalazimika kukubaliana kwa kila jambo. Yeye kama anaamini kwenye box la kura aendelee kuamini hiyo ni haki yake, lakini sisi wengine hilo ni zoezi haramu kama haramu nyingine na hatuyumbi kwenye hilo. Hata aseme kiongozi yoyote wa cdm, ccm, dini nk, bado msimamo mwetu ni dhabiti kwa kutoshiriki ushenzi unaoitwa uchaguzi kwenye awamu hii ya tano hilo halitawezekana.
 
Hii inaitwa inconsistency. Ukiwaambia wanakasirika.
P

Labda mwenye hiyo incosistancy iko kwenye huyo mleta uzi, sisi wengine hatubadiliki kwenye msimamo wetu maana tuna sababu za msingi wa kutoshiriki huo ushenzi. Tena nimemshamngaa mleta uzi kama nilivyomshangaa Mbowe kusema atashiriki uchaguzi huu, huku akiwa amegoma kushiriki chaguzi nyingi na wakati bado mazingira ni yale yale.

Ni bora viongozi wa upinzani kwa sasa wakajikita kwenye kuhamisisha tume huru ya uchaguzi na sio kuendelea kuzipa uhalali chaguzi hizi za uhuni wa kitoto.Hapo ndio madai yangu ya kwamba muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umekwisha, ni vyema akampisha mtu mwingine kiroho safi aendelee na matakwa ya umma.

Nilipendekeza viongozi wa upinzani kususia uchaguzi huu na kutangaza kutoshiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa, mpaka ipatikane tume huru ya uchaguzi, na ikifika mwaka kesho kuanzia mwezi machi watangaze maandamano ya amani kila mwanzo wa mwezi au mwisho, kwa kuanzia maandamano hayo yafamywe na viongozi tu, baadae wakashirikisha wananchi. Iwapo hakutakuwa na muafaka, ifikapo wiki ya mwisho ya uchaguzi kuwe na maandamano wiki nzima wangalau masaa 6 kila siku. Faida za maandamano haya itakuwa ni kutoa uhalali wa madai yao, uchaguzi utakuwa na picha mbaya kimataifa, na viongozi watakaopatikana watakuwa wamepatikana kwa mchakato haramu, na hawatakuwa na confidence kwani watakuwa wanatawala watu wasio na imani na madaraka yao. Kubwa kuliko yote, joto hilo halitampa Magufuli nguvu ya kujiongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi, kwani atakuwa ameingia madarakani kwa kipindi cha mwisho kwa uchaguzi uliosusiwa na watu wengi. Hali hiyo itaaicha Tanzania na picha mbaya kimataifa na itajikuta na wakati mgumu huku tukiwa na jamii iliyogawika.
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya dola kutawala.
 
Alafu utaanzisha uzi mmeibiwa kura..dah, mbowe anawainjoi sana.
 
Siku hizi ukiwa mpinzani unaonekana wewe ni zaidi ya shetani huku mitaani, ndio maana hata kuvaa magwanda watu wanaona aibu
 
Alafu utaanzisha uzi mmeibiwa kura..dah, mbowe anawainjoi sana.

Yaani ni mpaka tungoje uchaguzi ndio tuanzishe uzi wa wizi wa kura? Hiyo tu kupika idadi ya wapiga kura na huu uhuni wa kipuuzi unaoendelea hivi sasa ni jibu tosha la wizi huo.
 
Paskali mwanzo wa jamii forums ulikuwa kijana smart kilichokukumba nini njaa ama nini maanake afadhali ya le mutuz ana nafuu peleka njaa zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…