Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Ili kujenga mahusiano mazuri kwanza hakikisha wewe ni mwaminifu. Ukitaka kuwa na mahusiano mazuri hakikisha uliyenaye ni mwaminifu. Kwetu wanaume kitu cha kwanza muhimu ni mwanamke mwaminifu.
Uaminifu unajumuisha; kusema ukweli, kuwa na mtu mmoja (kuto saliti), kumuamini mwenzako, kuhifadhi siri za ndani, na kufanya kinachotakiwa kufanywa/ulichosema unakifanya.
Hakikisha kwanza wewe una uwezo wa kuwa mwaminifu, kisha ndio umjaji mwanamke wako. Lakini kama mwanamke uliyenaye hana sifa za kufanya vitu hivyo, inabidi ujiulize tena kama upo na mtu sahihi.
Kosa linalofanywa na wengi ni kuamini kuwa ukiwa naye utaweza kumbadilisha. Sio kweli, hakuna mtu anayeweza kumbadili mwingine. Mtu anabadilika anapotaka mwenyewe. Watu wengine ni wa kumsaidia tu ili abadilike.
Usizame mazima kwa mwanamke. Anza kwa kujuana naye kwanza. Ukiona mambo ambayo huwezi vumilia ni heri uachane na huyo mwanamke mapema. Kabla hujawekeza hisia sana kwake. Ikifikia hatua umeshazama mazima, ni ngumu kuachana naye.
Utajikuta unajipa moyo “Ah, ipo siku atabadilika, nitamfundisha atabadilika,” sio kweli. Mtu akikuonesha jinsi alivyo, mwamini. Hauna haja ya kujidanganya. Usije ukaishia kusalitiwa, kuumia na kuona wanawake wengine wote ni wabaya.
Share Na Wengine Wapate Kujifunza.