Chakula cha Mama Ntilie ni kwaajili ya masikini

Chakula cha Mama Ntilie ni kwaajili ya masikini

Masikini kivp Yani Hana hela au anapata huduma isiyo Bora, maana Kuna watu wanaua 3500 kwa sahani moja ya chakula hebu fikiria huyo mtu kwa siku anatumia sh.ngap
 
leo umekosa danga wa kukulisha hotel umeenda mgahawani unaona pa kimasikini...
 
Lakini vinatutoa shavu mkuu Tena unapimiwa mzigo wakutosha Mboga Kama zoote yaani tunafaidi Sana

Ila ukienda kwenye hotel zenye hadhi msosi unapewa Kama umeomba Tena ukute hakijaiva vzr na wananyodo Sana wahudumu wahiyo mihotel
Mnachopewa ni unbalanced diet, ni bora tumbo lijae. Mahoteli makubwa unapewa balanced diet ili kila kona ya mwili wako ifikiwe na necessary nutrients.
 
Hotelini 8000 hushibi
Mboga saba 1500 unashiba na chakula fresh.
Nb wanaokulaga mahotelini wanapatwa na maradhi mbalimbali.
Sisi wa kwamboga saba hutukuti
Nani mjanja,peleka tai yako hotelini
Chakula siyo kushiba mkuu, ndiyo maana watu wanatoka vitambi vya hovyo. Chakula ni balanced diet! Kuhakikisha mwili umepata all ingredients
 
Huu uzi ni ngumu kukubaliana nao kwa 100%. Kwanza inategeme na mama ntilie wa sehemu gani. Mama ntilie wa Moshi ni tofauti kabisa na mama ntilie wa Tandale. Pale Moshi kama unaelekea Dar es salaam Street kuna mama ntilie flani ambao hupika jioni tu kiukweli kwanza wao walivyo tu inaashiria wanafanya kazi benki au ofisi flani ya kiheshima. Msosi wa kutosha na tunda juu. Bei yao ingawa ni ndogo lakini iko kwenye uhalisia kwa hali ya uchumi wa Moshi. Kwahiyo hata mimi nikiwa Moshi huwa naenda hapo kula jioni. Hawa mama ntilie wanaozungumziwa na mleta mada ni hawa wa Tandale ambao chakula cha 3000 anauza buku hadi unashangaa. Uchafu ni sehemu ya mapishi yao halafu unaweza kumnunua na mpishi kabisa. Nimalize kwa kukutaka wewe mtoa mada useme ni mama ntilie gani umemaanisha kwasababu hata Open Kitchen hujiita mama ntilie wa kishua.
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.
Hii misosi ya mama nitilie ni kwaajili ya maskini.
Mabenchi machafu
Viti vimevunjika
Meza chafu, inzi wakutosha
Msosi sometimes unanuka moshi
Wahudumu wachafu
Customer care iko chini.
Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.
Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)
Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.
Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
We hujui utamu wa misosi ya mama ntilie wewe
 
Mnachopewa ni unbalanced diet, ni bora tumbo lijae. Mahoteli makubwa unapewa balanced diet ili kila kona ya mwili wako ifikiwe na necessary nutrients.
Mkuu dalili mojawapo ya mwili kulizika nikutoka shavu sasa hicho unachokiita unbalance diet ndicho kinawatoa shavu
 
Mama Ntilie nao wako na classes zao..mimi kuna baadhi ya mama Ntilie huwezi kunilisha chakula chao asee hasa mama Ntilie wa Dodoma ni wachafu hatari.
Haaaaaa Dada zake Ndugai,
Usimsemee kaka wa mjengoni huwa anakula msosi India
 
Mama ntilie wengine wanauza chakula katika mazingira hatarishi na huwa wanawapa hongo bwana afya na bibi afya ili wasifungiwe.
 
1627193859370.png
 
 
Masikini hana uwezo wa kununua chakula kwa mama ntilie.

Sina mengi wakuu nawasalimu.
Hii misosi ya mama nitilie ni kwaajili ya maskini.
Mabenchi machafu
Viti vimevunjika
Meza chafu, inzi wakutosha
Msosi sometimes unanuka moshi
Wahudumu wachafu
Customer care iko chini.
Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.
Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)
Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.
Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
MAMA NA BABA LISHE NI WATAMU, VYAKULA VYAO NI VITAMU HAKUNA MFANO.
 
Umenikumbusha shule ya msingi. Tulikuwa tunakunywa maziwa ya kununua na mikate wakati wa lunch break. Siku moja class mate akadai kuna sehemu USWAZIBkuba wali Nyama au wali maharage ná kachumbari bomba sana. Akatushawishi twende tukaonje. Kabla ya hapo sikuwahi kula wali maharage na kachumbari. Basi tukaamua kwenda kama Wanafunzi 10 hivi. Cha kushangaza wali maharage na kachumbari ilikuwa very popular kuliko wali Nyama kachumbari lakini umbali sasa. Huu ulichukua muda hata muda wa kucheza na wenzetu ukapotea. Mahali penyewe ilikuwa ni nyumbani kwa mtu USWAZI usafi si haba lakini siku nyingine kulikuwa na wateja wengi. Hivyo mwishowe tuliamua kurudi kwenye maziwa yetu na mikate ili tupate muda wa kucheza ná wenzetu. UTOTO RAHA SANA.

 
Back
Top Bottom