Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Uko sahihi Daby; chakula kinategemea upikwaji wake. Ukila kwa mara ya kwanza chakula kilichopikwa vibaya, hutakaa ule tena chakula hicho ukijua daima ni kibaya.
Ni Kama Mimi nisivyopenda maboga.... Ingawa watu wanayasifia kweli..... Mimi Mara ya kwanza kula boga lilikua bayaaaaaa
 
Mm ile mboga ya majani inaitwa kisamvu, nilikula nikavimba mwili ,hadi leo nikikuta iko mezani mm lazima ninyanyuke,
Nashauri wabadiri hilo jina
 
[emoji1][emoji1][emoji1] Kama nakuona
 
Hivi huu ni ushamba ama ni nyodo za kula?
Tikiti maji linakushindaje?
Wakati nipo chekechea ndiyo niliyajua matikiti, niliyakuta nyumbani siku hiyo. Nilikula, hata sikumaliza kipande nikaanza kutapika.

Hali iliendelea mpaka nikapelekwa hospitali. Hakuna aliyefikiria sababu inaweza kua matikiti, so siku nyingine yakaja tena, ikajirudia tena hali ileile na kutapika kwa nguvu. Baada ya kupona hapa ndiyo hata harufu yake imekua inanishinda.

Hivyo ikawa ishajulikana kwamba kwangu mimi matikiti siyawezi.

Hivyo siyo ushamba wala nyodo ni swala la uhai au ugonjwa.

Hata hivyo juisi yake ikichanganywa na matufaa naweza kuinywa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…