1.KAHAWA
kuna jamaa zangu wengi hupenda kweli kahawa,namimi ki ukweli napenda sana ile harufu yake tena nikiona na zile kashata huwa natamani kweli,siku 1 namimi nikasema haiwezekan kila siku nile harufu,Akapta muuza kahawa "nikamuita" kwa kujiamini kama vile member kbsa, akaja nkamwambia "weka kahawa hapa bwana mkubwa" Akanimiminia.
akanipa na kashata zake nikachukua 1,nikatia mdomoni mdomoni "bwana weeee" ilikua chungu hiyooooo haimezeki yani bahati yangu ilivyokua mbaya nilikaa sehemu ambayo hamna hata pakutemea.kote kulikua na tyrese tena nyeupee,asee nilijitahd kunywa ile kahawa ila sikuweza pga hata pafu lingine,muda huo nakunywa kashata yangu mkononi "nishaimaliza mudaaa" ila kakikombe ka kahawa kamejaa full,wenzangu washaongeza round mbili mi npo tu.
nikawa natafuta namna ya kutoka pale nisogee pembeni nikaimwage ie kahawa,ikabd nitege Alarm ya dk 3 nikakaa simu ikaita nikajifanya nimepokea nkainuka nikasogea kwenye mchanga nkamwagilia mbali kahawa lao.