Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”

Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”

Sio kweli Kila mtu taarifa zake zipo kuanzia za kibayometric Hadi za physical,huwezi Anza kutanga Tanga kushindana na Serikali kisa unafanya siasa za ujinga.

Bora ujinga huo wa Serikali kuliko fedheha.Wafanyabishara wa Kariakoo wasijifanye spesho sana,Nchi hii inaweza enda bila hao wajinga.
Eti nini?
Inchi za jirani zenyewe haziendi bila kariakoo, bwashee kariakoo ni habari ingine kabisa
We subiri tu uone serikali itakavyohangaika
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefika soko la Kariakoo kutokana na Biashara kufungwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kuongea na wafanyabiashara.

Chalamila amesema wafanyabiashara wako wa aina kadhaa ikiwemo walioshiba, kati na wachanga na iwapo wataigana kuna watakaojuta leo, kesho na mwingine baaada ya mwezi mmoja. Chalamila amesema ni kweli wafanyabiashara wanaweza kuwa na changamoto lakini zipo nyingine za kisheria na haiwezaki kuzisuluhisha asubuhi na mapema.


Chalamila amesema duka si sawa na hospitali kwani hospitali zingegoma ingekuwa hatari zaidi na kuomba busara itumike. Mwisho amemaliza na mkwara mzito kwa yeyote atakaempiga mkwara aliyekubali kufungua.

"Aliyekubali kufungua afungue na yule ambae atamletea mkwara mtu yeyote yule aliyekubali kufungua naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonesha shoo nzima. Wewe unakuja unamletea mkwara, mimi nitakuchimba mkwara na hautaamka tena, na hili naomba niwaeleze ndugu zangu wa Kariakoo, utoto ukizidi hatuwezi kufikia hapo"

Pia Chalamila amewashukuru waliofungua maduka na kuwaahidi waliofunga atazilinda biashara zao na hakuna mwizi atakaeiba hata kama itakuwa mwezi. Chalamila amesema biashara sio siasa na leo jioni wataona hasara yake lakini siasa haiwezekani kugundua hasara zake.

Chalamila pia amedai yeye kama mkuu wa mkuu wa mkoa akiumua kwenda kukaa madukani kwao aangalie kiwango kikubwa cha ukwepaji kodi, amehoji kama wataweza kuishi Kariakoo!

Pia, soma=> RC Chalamila: Wafanyabiashara wa Kariakoo wajitafakari, migomo siyo suluhisho

View attachment 3024612
Aggrey Mwanri apewe ukuu wa mkoa wa Darisalamu, hao wafanyabiashara angewachota wote na kuwasukuma ndani
 
Gharama za Bandari
Ndio maana nasema Samia anawachekea si unaona unavyoongea upumbavu hapa harafu uchumi uko paralysede.

Siasa za kindezi kama hizi piga ndani hao wapuuzi wakimbie Nchi.
Samiah anakuchekea wewe labda. Kwangu namuona Kama incapable leader.
 
Sawa. Fuata Sheria za Tanzania bila shuruti
Huu ni msemo usio na maana. Kuna 1) sheria zinazokataza (ni marufuku...), 2) kuna sheria zinazolazimisha (kila mtu ata...), 3) kuna sheria zinazoruhusu (mtu yeyote aweza...). Sasa hiyo ya kutii sheria bila shuruti iko upande gani wakati sheria tayari zina element ya 'coercion' (yaani kufanya jambo lolote au kutofanya kwa jinsi sheria zinavyoelekeza)?
 
Kwani Toka wameanza kunyongwa Wala Rushwa waneisha? Acheni ujinga wa kuhujumu uchumi Kwa siasa nyepesi
Anayekula rushwa Ina maana kajitoa mhanga. Wananyongwa mawaziri sembuse wewe. Nani anahujumu uchumi, kufunga duka au mgomo sio uhujumu uchumi. Hakuna kosa Kama Hilo.
 
Kwani hao wafanyabiashara wameanza kufanya biashara jana paka aanze kuwaeleza hasara na faida za biashara zao.
Mama angewaza kiupana angeanza na kufukuza huyu..... Anaongea kama anaongea na masikini wanaojitafuta.... Tatizo Sana hili...
 
Back
Top Bottom