Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefika soko la Kariakoo kutokana na Biashara kufungwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kuongea na wafanyabiashara.

Chalamila amesema wafanyabiashara wako wa aina kadhaa ikiwemo walioshiba, kati na wachanga na iwapo wataigana kuna watakaojuta leo, kesho na mwingine baaada ya mwezi mmoja. Chalamila amesema ni kweli wafanyabiashara wanaweza kuwa na changamoto lakini zipo nyingine za kisheria na haiwezaki kuzisuluhisha asubuhi na mapema.

Chalamila amesema duka si sawa na hospitali kwani hospitali zingegoma ingekuwa hatari zaidi na kuomba busara itumike. Mwisho amemaliza na mkwara mzito kwa yeyote atakaempiga mkwara aliyekubali kufungua.

"Aliyekubali kufungua afungue na yule ambae atamletea mkwara mtu yeyote yule aliyekubali kufungua naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonesha shoo nzima. Wewe unakuja unamletea mkwara, mimi nitakuchimba mkwara na hautaamka tena, na hili naomba niwaeleze ndugu zangu wa Kariakoo, utoto ukizidi hatuwezi kufikia hapo"

Pia Chalamila amewashukuru waliofungua maduka na kuwaahidi waliofunga atazilinda biashara zao na hakuna mwizi atakaeiba hata kama itakuwa mwezi. Chalamila amesema biashara sio siasa na leo jioni wataona hasara yake lakini siasa haiwezekani kugundua hasara zake.

Chalamila pia amedai yeye kama mkuu wa mkuu wa mkoa akiumua kwenda kukaa madukani kwao aangalie kiwango kikubwa cha ukwepaji kodi, amehoji kama wataweza kuishi Kariakoo!

View attachment 3024459
View attachment 3024461

Hivi Serikali ikiamua kuwafutia leseni wafanyabiashara wote waliogoma ikizingatiwa tin namba zinasoma na wapigwe marufuku kokote kufanya biashara Kwa sababu za uhujumu uchumi kwani watafanya nini?
 
wanatumia ID za watu wengine ambao hawako kwenye mifumo ya kulipoa kodi. Kufikia hapo serikali inakuwa imefanya ujinga.
 
Sasa Waziri wa Biashara kakubali kuongea nao na kuwasililiza malalamiko yao. Wewe chawa mwenye roho mbaya umebaki kuropoka. Yani mnajifanya mna hasira kuliko Waziri mwenyewe. Pole sana.
Bando la bure anafanya chochote tu hata cha kijinga tu
 
wanatumia ID za watu wengine ambao hawako kwenye mifumo ya kulipoa kodi. Kufikia hapo serikali inakuwa imefanya ujinga.
Sio kweli Kila mtu taarifa zake zipo kuanzia za kibayometric Hadi za physical,huwezi Anza kutanga Tanga kushindana na Serikali kisa unafanya siasa za ujinga.

Bora ujinga huo wa Serikali kuliko fedheha.Wafanyabishara wa Kariakoo wasijifanye spesho sana,Nchi hii inaweza enda bila hao wajinga.
 
Unaleta hoja dhaifu sana, ungekuwa hata na genge ungeelewa
Hakuna Cha genge,Mimi nauza dawa la bidhaa za Kilimo,Kodi nalipa na maisha yanaenda,kwamba nyie pimbi wa Kariakoo ndio mna malalamiko sana kuliko sisi wa Mikoani au?

Serikali iwashughulikie tuone itapata hasara zipi.
 
Hivi Serikali ikiamua kuwafutia leseni wafanyabiashara wote waliogoma ikizingatiwa tin namba zinasoma na wapigwe marufuku kokote kufanya biashara Kwa sababu za uhujumu uchumi kwani watafanya nini?
Kasome sheria ya leseni ya biashara, kwanza katika adhabu hakuna kufungiwa biashara Bali fine au kufunguliwa kesi mahakamani. Muwe mnasoma kwanza kabla ya kuropoka.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefika soko la Kariakoo kutokana na Biashara kufungwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kuongea na wafanyabiashara.

Chalamila amesema wafanyabiashara wako wa aina kadhaa ikiwemo walioshiba, kati na wachanga na iwapo wataigana kuna watakaojuta leo, kesho na mwingine baaada ya mwezi mmoja. Chalamila amesema ni kweli wafanyabiashara wanaweza kuwa na changamoto lakini zipo nyingine za kisheria na haiwezaki kuzisuluhisha asubuhi na mapema.

Chalamila amesema duka si sawa na hospitali kwani hospitali zingegoma ingekuwa hatari zaidi na kuomba busara itumike. Mwisho amemaliza na mkwara mzito kwa yeyote atakaempiga mkwara aliyekubali kufungua.

"Aliyekubali kufungua afungue na yule ambae atamletea mkwara mtu yeyote yule aliyekubali kufungua naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonesha shoo nzima. Wewe unakuja unamletea mkwara, mimi nitakuchimba mkwara na hautaamka tena, na hili naomba niwaeleze ndugu zangu wa Kariakoo, utoto ukizidi hatuwezi kufikia hapo"

Pia Chalamila amewashukuru waliofungua maduka na kuwaahidi waliofunga atazilinda biashara zao na hakuna mwizi atakaeiba hata kama itakuwa mwezi. Chalamila amesema biashara sio siasa na leo jioni wataona hasara yake lakini siasa haiwezekani kugundua hasara zake.

Chalamila pia amedai yeye kama mkuu wa mkuu wa mkoa akiumua kwenda kukaa madukani kwao aangalie kiwango kikubwa cha ukwepaji kodi, amehoji kama wataweza kuishi Kariakoo!

Pia, soma=> RC Chalamila: Wafanyabiashara wa Kariakoo wajitafakari, migomo siyo suluhisho
Kwetu kuna msemo "buli kuundi buli kumbali" (kama siyo shida yako, iko pembeni/siyo shida yako). Hawa wafanyabiashara ni wao wanaojua mambo wanayoyapitia. Ni wao wanaopata hasara kama wakifunga maduka, lakini kama wameona heri wapate hasara kuliko faida wanayoipata inayoambatana na kero wanazozilalamikia, pengine zinazo wapa pia hasara na kushindwa kulipa kodi wanayotakiwa walipe, halafu hatua waliyoichukua ili kero hizo ziweze kufanyiwa kazi, wewe usiyepata hizo kero/hasara uone ni utoto, naona ni ukosefu wa consideration na kwa kiongozi ni lack of good judgement.
 
Hakuna Cha genge,Mimi nauza dawa la bidhaa za Kilimo,Kodi nalipa na maisha yanaenda,kwamba nyie pimbi wa Kariakoo ndio mna malalamiko sana kuliko sisi wa Mikoani au?

Serikali iwashughulikie tuone itapata hasara zipi.
Ulisema u mkulima, Leo unadai unauza bidhaa za KILIMO!!

KAZI Yako ni uchawa, huna unachofanya zaidi.
 
Back
Top Bottom