Chalamila karibu Dar, jiji hili linataka mtu mtata na mwenye matata kama wewe

Jiji la Dar es Salaam ndilo jiji lenye amsha amsha kuliko jiji lingine lolote. Ndilo jiji lenye bandari kubwa nchini, uwanja wa ndege mkubwa, barabara za kutoka sehemu zote nchini huishia Dar.

Dar ni jiji la maraha na karaha pia. Matapeli, vibaka, majambazi, wezi, na machanguduoa pia.

Mitume na manabii wenye maji ya upako, mafuta, ubuyu wa upako, mafenesi ya upako na chupi zinazosababisha wagumba washike mimba vyote vinapatikana Dar.

Dar kuna panya Road waliokulia katika nyumba za polisi na nyumba za viongozi wa dini.

Dar kila mtu ni afisa wa ikulu, tena bosi. Machinga wa Dar ana Range Rover Sport analia bata mtaani.

Karibu sana Chalamila, hapa ndio nyumbani kabisa kwa kina Tulinawe Kamwela mliyekuwa naye Iringa Tumaini University.

maggid naye kwake Iringa ila mishe ndio zimemleta Dar. Naamini ujio wako Dar ni wa kudumu. Sisi Wazaramo ni wakarimu sana.

Karibu utuhudumie kwa utumishi uliotukuka.
Chala hatoboi kwa DAR.subiri utaniambia
Bro
 
Wafanyabiashara wamesema Makala haeleweki anachosema, Mwanza watamuelewa?
 
Wazaramo walishauza Ardhi zao za Dar sasa hivi wengi wapo pembezoni mwa Dar huko Nsangangongele, Mwalusembe na kwengineko
Haiondoai uasili mjomba....wenyeji wapo wengi tu ila ni ngumu kujua....na hiyo ndo sifa ya Jiji kubwa....ukiona Jiji bado wenyeji wengi kuliko wageni basi hiko ni Kijiji....
 
Wenyeji wa Dar sio wazaramo wale wazaramo wenye Dar wapo kando kando uko walishauza maeneo yao kupisha matariji wanaojenga maghorofa, sasa wapo Mwalusembe huko na viunga vyake
 
Wazaramo walishauza Ardhi zao za Dar sasa hivi wengi wapo pembezoni mwa Dar huko Nsangangongele, Mwalusembe na kwengineko
Ni kawaida kwa wenyeji kukaa nnje ya mji,popote pale duniani ipo hivo.. Ukienda London utaona wageni Paris ni hivo Brussels, kwa waliotowa miwani ya Mbao wanalijuwa hili,ila kwako wewe unaona Manzese Magomeni ni sehemu bab kubwa.
 
Sijakupinga Ila wazaramu akifa tu mwenye mji wake wanauza eneo kwa matajiri wanagawana Pesa kisha wanahamia pembezoni huko machakani machakani mji wanawaachia wenye Pesa
 
kapaweza vipi Kagera?

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
Kwa sisi tunaoishi huku tunayaona maendeleo kwa muda mfupi; watu wa huku walizoea kuishi kimazoea, kukumbatia mashamba makubwa muda mrefu kwenye maeneo nyeti pasipo kuyafanyia lolote, Chalamila aliwalazimisha wayajenge ama wayaachie (alimuomba kibali Rais), kitu ambacho matunda yake tumeanza kuyaona, watu wanajenga sahivi. Pia kuna wafanyabiashara walijiona wao ndio wenye mji, wakitokea wawekezaji sehemu tofauti wa kuwachallenge wamekuwa wakipigwa fitna hadi wanaaga mashindano, hawa watabe alifanikiwa kuwadhibiti kwa kiasi kikubwa na sasa tunashuhudia wawekezaji wapya kutoka sehemu tofauti, hawa 'watabe' waliamini hakuna wa kuwababaisha maana wana uongozi pia ndani ya CCM hivyo Chalamila nampongeza kwa kutake risk kupambana nao na kuwashinda. Pia na maendeleo mengine ya kimiundombinu tumeona yakifanyika kwa kasi chini yake, zile doria za Polisi kila ikifika saa5 usiku tumezisahau maana huko nyuma enzi za wakuu wa mikoa wanajeshi tulikuwa tukisumbuliwa ikifika saa tano kasoro inabidi uwahi nyumbani, bila kusahau alikemea sana tabia ya Wahaya kuchelewa kufungua maduka, kitu kinachochangia kupunguza mzunguko wa fedha na kudumaza maendeleo
 
Wenyeji wa Dar sio wazaramo wale wazaramo wenye Dar wapo kando kando uko walishauza maeneo yao kupisha matariji wanaojenga maghorofa, sasa wapo Mwalusembe huko na viunga vyake
Tatizo lako huijui Dar.....unasimuliwa tu....tulia.....naandika kama mkazi na mwenyeji wa Dar.
 
Back
Top Bottom