Chalamila karibu Dar, jiji hili linataka mtu mtata na mwenye matata kama wewe

Chalamila karibu Dar, jiji hili linataka mtu mtata na mwenye matata kama wewe

Dar haihitaji mkuu wa mkoa, matatizo ya Dar ni ya kitaifa.

Issue kama za wafanyabiashara wa Kariakoo huyo Chalamila atatatuaje?

Dar is a heavyweight.

Tuwe na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Kiongozi Mkuu wa jiji la Dar

Hao wengine ni viongozi katuni.
Aah wapi!
 
Jiji la Dar es Salaam ndilo jiji lenye amsha amsha kuliko jiji lingine lolote. Ndilo jiji lenye bandari kubwa nchini, uwanja wa ndege mkubwa, barabara za kutoka sehemu zote nchini huishia Dar.

Dar ni jiji la maraha na karaha pia. Matapeli, vibaka, majambazi, wezi, na machanguduoa pia.

Mitume na manabii wenye maji ya upako, mafuta, ubuyu wa upako, mafenesi ya upako na chupi zinazosababisha wagumba washike mimba vyote vinapatikana Dar.

Dar kuna panya Road waliokulia katika nyumba za polisi na nyumba za viongozi wa dini.

Dar kila mtu ni afisa wa ikulu, tena bosi. Machinga wa Dar ana Range Rover Sport analia bata mtaani.

Karibu sana Chalamila, hapa ndio nyumbani kabisa kwa kina Tulinawe Kamwela mliyekuwa naye Iringa Tumaini University.

maggid naye kwake Iringa ila mishe ndio zimemleta Dar. Naamini ujio wako Dar ni wa kudumu. Sisi Wazaramo ni wakarimu sana.

Karibu utuhudumie kwa utumishi uliotukuka.
 
Haiondoai uasili mjomba....wenyeji wapo wengi tu ila ni ngumu kujua....na hiyo ndo sifa ya Jiji kubwa....ukiona Jiji bado wenyeji wengi kuliko wageni basi hiko ni Kijiji....
Mueleweshe huyo
 
Back
Top Bottom