Chalamila: Vibaka wafanywe 'skeleton' za maabara iwe fundisho kwa wengine

Chalamila: Vibaka wafanywe 'skeleton' za maabara iwe fundisho kwa wengine

SKELETON TENA.SIWAPEND WALA SINA HURUMA NAO ILA ADHABU IWE KALI KWA UTARATIBU UNAOFAA
Utathibitishaje kuwa ñi kibaka ? Kusingiziwa ? Vipi wewe siku unakatiza mtaani wakakuungia kisasi etc wakakupiga ni kibaka....unaenda skeleton pia?
 
Wakuu,

Ni Chalamila tena katika matamko yake kama vile amekatwa kichwa! Mchengerwa OR TAMISEMI tunasubiri neno lako hapo, huyu bwana hajui kama kuna sheria za kufuata?

====


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali watu wote wanaojihusisha na uporaji 'vibaka' katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo hususani vibaka wa Daraja la Selenda, ili iwe fundisho kwa wale wote wanaohatarisha amani na usalama jijini.

Chalamila amesema hayo mwishoni mwa juma alipoongoza zoezi la usafi kama maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Daraja la Selenda, Soko la Kimataifa la Salamaki la Feri na maeneo mengine ikiwa ni maandalizi kuelekea Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika 'Mission 300' unaotarajiwa kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Januari 27-28 mwaka huu.

Chalamila amesema, "Sasa, naagiza kibaka takayekamatwa, asipigwe wala kuuliwa, apelekwe maabara awe 'skeleton' mifupa ya kufundishia wengine ambao wataiga mfano kwamba wizi haustahili katika jiji la Dar, kwahiyo hilo ndio agizo langu, wakale kielelezo kizuri kwa watu wengine." amesisitiza RC huyo.
Aulizwe pia mafisafi na wahuni serikalini wafanywaje?

Tuna muuaji mwenye uchu wa nyama za wafu katika madaraka
 
Ndugu yangu walimpiga bisibisi ya tumbo kisa tu wamuibie laptop. Tuliuguza weee mwisho akafariki 🙆‍♂️
Duh polen jamani

Nchi zetu hizi ni shida sana

Viongozi wanajua kuiba tu
 
Hv najiulizaa mtu anaetetea vibaka ni aitha mwanae au ndugu yake nikibaka hv mmeshawah kuonaa kbaka anamtkboa mtu bissbis ya tumboo kisa ampokonye kiswaswaduu.kibaka au mwiz popote alipo nawanao watetea wapgwe mapgo yanayo stahk kutoa nafsi zao 🙏🙏🙏
 
Kuna namna ya kufikisha ujumbe bila kuonesha unahamasisha kuvunja sheria. Mfano yule aliesema POLISI WAWANYANG'ANYE SILAHA MAJAMBAZI. Hapo utajua silaha wananyang'anywa vipi.
Hiyo imenipita nadhani hebu niambie ni nani amesema nikamgoogle saivi
 
Hv najiulizaa mtu anaetetea vibaka ni aitha mwanae au ndugu yake nikibaka hv mmeshawah kuonaa kbaka anamtkboa mtu bissbis ya tumboo kisa ampokonye kiswaswaduu.kibaka au mwiz popote alipo nawanao watetea wapgwe mapgo yanayo stahk kutoa nafsi zao 🙏🙏🙏
Hayo yanatokea haimaanishi ndio nawe uue, ingekua hivi hata mtu anaweza kuwa hajaiba akazushiwa uhai ukapokwa. Sheria zingekua madhubuti wananchi wangewaamini polisi... kujichukulia sheria mkononi ni matokeo ya polisi kufeli
 
Back
Top Bottom