Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Unafahamu kuna watu wametelekezwa na mimba na hata kula yao ya siku ni mtihani?
 
Hawa ndo Watanganyika
Magufuli aliwaita wanyonge wanashangilia eti anawapenda

Mimba yako
Mtoto wako
Hata kuchangia elfu 50 unasema unanyanyaswa
 
Jibu swali kwa jibu sio kwa swali.
Kwani Tz hamna ustawi wa jamii na mashirika mengine ya wakina mama wenye matatizo?
Nakuuliza sababu unajenga hoja kama mgeni ama mtu mwenye uelewa finyu wa mazingira ya Kitanzania.

Miezi michache iliyopita kuna mtu alifariki kwa kugongwa na nyoka kwa sababu alikosa fedha.

Kuna wagonjwa huko Tunduru wanasafirishwa kwenye matenga.
Na kama umewahi kutembea ama kuishi mikoani utashuhudia maelfu ya Watanzania wanaishi kama wanyama kutokana na umasikini.

Asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi hand-to-mouth hawana hata akiba.

Mnazungumzia habari ya ku-save elfu hamsini kama kwamba ni buku.

Tembeeni mjionee diversity. Msishinde Kariakoo mkaishi mnaifahamu Tanzania.
 
Acha kutafuta huruma na kukwepa wajibu
Huyo mama alimpigia mkuu wa mkoa simu.
Simu ni bei gani? Vocha?
Anakosaje elfu 50 mwaka mzima.
Kuna watu wana maisha magumu sawa nadhani hao serikali ingeona jinsi ya kuwasaidia
 

Kweli Kabisa
Elimu bure
Afya bure.

Wapo watu wakupewa bure Kabisa hasa Wazee waliokuwa wanalipa Kodi, watoto yatima,
 
Acha kutafuta huruma na kukwepa wajibu
Huyo mama alimpigia mkuu wa mkoa simu.
Simu ni bei gani? Vocha?
Anakosaje elfu 50 mwaka mzima.
Kuna watu wana maisha magumu sawa nadhani hao serikali ingeona jinsi ya kuwasaidia
Umeuliza maswali ambayo majibu yako ndani ya jibu lako.
Kama unakiri kuna watu wana maisha magumu na wanahitaji kusaidiwa, kwa nini huyo mama asingesaidiwa?
Unaulizia habari za vocha na simu, kwani hawezi kuazima kwa mtu?
___
Mimi sitafuti huruma, ila ninachohitaji ni lugha za staha kutoka kwa kiongozi ambaye anaongoza watu wenye maisha yanayotofautiana.
Pia, ninahitaji kuona rasilimali za nchi zinatumika ili kuwasaidia wananchi wake. Nchi hii na rasilimali zake, ni aibu kukosa gloves kwenye hospitali zake.

Zindukeni ninyi.
 
Mkuu mbona kama unakwepa kujibu swali kwa kuleta hoja zingine. Hiyo habari ya wagonjwa kusafirishwa kwenye matenga hapo nailaumu serikali moja kwa moja ila hapa tunaongelea mama mjamzito. Mkuu hata kama uwe masikini vipi ukikaza unaweza kupata 50,000 ndani ya miezi tisa hata kwa kuombakuomba kwa majirani la sivyo utabaki unailaumu serikali kwa vitu vidogovidogo.
 
Kabla ya kuangalia rasimali zetu kama zinatufaidisha au la
Tuangalie hizi akili za kutungisha mimba siku ya kujifungua hata Elfu 50 huna
Haya tuchukulie mtoto amezaliwa anataka nepi, chandarua, maziwa lishe, vyakula vya mama mzazi, blanket
Unataka na Serikali ikupe Bure eti kwakuwa unalipa kodi
 

Wewe utakubali kumpeleka Mkeo au binti yako mjamzito Akiwa Hana vifaa vya kujifungulia au Hana pesa?

Ikiwa jibu ni Ndio Basi wewe ni shetani mwenye cheo cha juu Kabisa.

Kwa nini mnapenda kutafutia watu ubaya?
 
Wacha uzoba wewe. Kwani hakukuwa na namna nyingine ya kuelezea hiyo hali bila kusema maneno ya kijinga kuwa arudi nyumbani mume wake akasaidie kujifungua? Haya mambo kiongozi yoyote mwenye busara anaweza kuyaelezea kwa kutumia hekima na siyo kiburi. Au wewe huko kwenu mlikuzwa kwenye mazingira ya kutotumia busara wakati unaongea kwenye kadamnasi?
 
Wewe utakubali kumpeleka Mkeo au binti yako mjamzito Akiwa Hana vifaa vya kujifungulia au Hana pesa?

Ikiwa jibu ni Ndio Basi wewe ni shetani mwenye cheo cha juu Kabisa.

Kwa nini mnapenda kutafutia watu ubaya?
Kulikuwa hakuna namna nyingine ya huyu mjinga kuelezea na wananchi wakamwelewa? Kiburi na ulevi wa madaraka unazidi kuwaandama waafrika ndiyo maana hatuendelei
 
Kama unajua yotee haya na unajijua wewe masikini KWANINI UBEBE MIMBA?

Unabeba mimba ukimtafutia nani shida sasa??

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Najaribu kukupa mifano walau kupanua ufahamu wako lakini kwa kuwa una kichwa kigumu unaona nikwepa jibu.

Je, huyu aliyeombaomba na kupata hamsini, endapo akipata dharura kabla ya muda wa kujifungua akatumia hiyo fedha, atarudi tena kuomba?

Watu hawana vipato vya uhakika. Kula kwenyewe wanabahatisha. Hawajawahi kuwa na akiba maisha yao yote kwa sababu wanachokipata chote kinaishia tumboni.

Labda nikuulize, masikini wa mwisho kabisa uliyewahi kumwona kwa macho yako, alikuwa anafananaje?
 

Watanzania wengi hupendelea kupewa Maneno ya busara ili kukimbia wajibu wao.

Busara zina wakati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…