Abul Aaliyah
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 7,718
- 5,899
P1 haya watangaze huo ushind wa kimbunga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upinzani sio chama, upinzani ni mtazamo Na itikadi!!Ipitishwe sheria
Chama kikisusia Uchaguzi kinafutwa kabisa
Kuna haja gani ya kushiriki uchaguzi wakati CCM wamejipitisha bila kupingwa, wakati mgombea akiteuliwa bila kupingwa ina maana hakuna uchaguzi.
Kuna hivyo vyama vya kipuuzi eti vimesema vinashiriki, wakati havijaweka mgombea hata mmoja, na wala havina hata muwakilishi mmoja bungeni. Ni wapuuzi waliobobea.
Siku za CCM zinahesabika, muda si mrefu wataangukia pua.
1) Ubaguzi/Uonevu/Uadui/Mgawanyiko wa "WANA CCM KWA WANA CCM" ndani ya chama chao (LUMUMBA) haujakwisha bado.
2) Uadui kwa vyama vya upinzani umezidi.
3) Uadui kwa raia umezidi mara 100.
4) Wafanyakazi wa umma toka 2015 - leo hawajaongezewa hata sh100 katika mishahara (licha ya ahadi wanazopewa).
5) Ufsadi wa Sh Trillioni 1.5, na Sh Trillioni 2.0 - Za Prof Assad CAG.
6) Ufisadi wa ununuz wa ndege kwa bei "MARA MBILI".
7) Utekwaji/Kupotea/Kuuliwa kwa raia.
8) Uonevu wa kufunga watu/viongozi wa upinzani gerezani bila sababu.
9) Uminywaji wa wanahabari/vyombo vya habari.
10) Ubakwaji wa demokrasia (RAPE OF DEMOCRACY).
11) Ajira/Biashara kufa kifo cha mende.
12) DPP na TRAFICK POLICE kugeuzwa TRA (Wakusanya mapato).
13) Mauwaji ya kibiti (watu wasiojulikana).
14) Watu wasiojulikana.
15) Uongo uliokithiri kutoka kwa viongozi kwa raia.
16) Figisu kwa CAG (Mtetezi wa kodi za raia)
17) Bunge kua dhaifu.
18) Kupigwa marufuku kwa wapinzani kufanya vikao/kampeni (wakati CCM wamefanya kampeni na vikao kuanzia 2015 mpaka sasa)
19) Kufukuza/Kwaonea/Kuwadhalilisha "WAFANYAKAZI WA UMMA" mbele ya hadhara bila hata kuwapa haki ya kwasikiliza (Kwa kutafuta sifa).
Na mengine mengi. . . . . . .
Msisubiri hata hiyo sheria, vifuteni hata jioni hii, lakini ccm ni chama outdated hakina mvuto tena. Mwanamke mzee hata ajipambe na kuwa na hela, bado vijana watafuata hela zake tu lakini hawawezi kumpenda. Hata mkitangaza chama kimoja cha siasa, bado ccm haitapendwa na wananchi maana watu wameshakinai. Msitumie nguvu kubwa kulazimisha kukaa madarakani, nature hairuhusu ccm kuendelea kupendwa na kizazi cha sasa. Sio kwamba ccm haijafanya kitu wala Magufuli hajafanya kitu, bali nature ndio ilivyo, watu wakichoka wamechoka tu.
Kama umechukia kunywa sumu ACT ndo tayari washajitoaAcha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao
Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama
State agent
Barikiwa sana mkuu, acha ccm ifanye kila inataka, lakini malipo ni hapa hapa dunianiKuna haja gani ya kushiriki uchaguzi wakati CCM wamejipitisha bila kupingwa, wakati mgombea akiteuliwa bila kupingwa ina maana hakuna uchaguzi.
Kuna hivyo vyama vya kipuuzi eti vimesema vinashiriki, wakati havijaweka mgombea hata mmoja, na wala havina hata muwakilishi mmoja bungeni. Ni wapuuzi waliobobea.
Siku za CCM zinahesabika, muda si mrefu wataangukia pua.
1) Ubaguzi/Uonevu/Uadui/Mgawanyiko wa "WANA CCM KWA WANA CCM" ndani ya chama chao (LUMUMBA) haujakwisha bado.
2) Uadui kwa vyama vya upinzani umezidi.
3) Uadui kwa raia umezidi mara 100.
4) Wafanyakazi wa umma toka 2015 - leo hawajaongezewa hata sh100 katika mishahara (licha ya ahadi wanazopewa).
5) Ufsadi wa Sh Trillioni 1.5, na Sh Trillioni 2.0 - Za Prof Assad CAG.
6) Ufisadi wa ununuz wa ndege kwa bei "MARA MBILI".
7) Utekwaji/Kupotea/Kuuliwa kwa raia.
8) Uonevu wa kufunga watu/viongozi wa upinzani gerezani bila sababu.
9) Uminywaji wa wanahabari/vyombo vya habari.
10) Ubakwaji wa demokrasia (RAPE OF DEMOCRACY).
11) Ajira/Biashara kufa kifo cha mende.
12) DPP na TRAFICK POLICE kugeuzwa TRA (Wakusanya mapato).
13) Mauwaji ya kibiti (watu wasiojulikana).
14) Watu wasiojulikana.
15) Uongo uliokithiri kutoka kwa viongozi kwa raia.
16) Figisu kwa CAG (Mtetezi wa kodi za raia)
17) Bunge kua dhaifu.
18) Kupigwa marufuku kwa wapinzani kufanya vikao/kampeni (wakati CCM wamefanya kampeni na vikao kuanzia 2015 mpaka sasa)
19) Kufukuza/Kwaonea/Kuwadhalilisha "WAFANYAKAZI WA UMMA" mbele ya hadhara bila hata kuwapa haki ya kwasikiliza (Kwa kutafuta sifa).
Na mengine mengi. . . . . . .
Mnangoja nini sasa kuweka hiyo sheria ili mtupunguzie gharama za uchaguzi?Ipitishwe sheria
Chama kikisusia Uchaguzi kinafutwa kabisa
Hayo yametangazwa na kiongozi wa chama hicho Mh Zitto Kabwe.
ACT WAZALENDO CHAIFUATA CHADEMA, CHAJITOA KUSHIRIKI UCHAGUZI. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza kuwa chama hicho kimejitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa sababu kuwa wagombea wa chama hicho wengi wameenguliwa.
View attachment 1257821
ACT-WAZALENDO IMEJIONDOA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA:
MILANGO YA DEMOKRASIA IMEFUNGWA: TUSILAUMIANE
MSIMAMO WA ACT WAZALENDO KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI WA NOVEMBA 24, 2019:
Chama cha ACT Wazalendo, kikiwa Chama cha siasa makini chenye usajili wa kudumu nchini, kiliitikia wito wa kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliokuwa ufanyike tarehe 24 Novemba 2019, tukiamini kuwa ni nafasi nyeti ya kuimarisha ushindani wa kisiasa nchini.
Licha ya miaka minne ya changamoto kubwa, na licha ya wananchi wengi kutuonya mapema kuwa hapatakuwa na Uchaguzi wa Haki, bado tuliamua kushiriki kikamilifu tukiamini kuwa taratibu, sheria na Katiba ya nchi itaheshimiwa na wahusika wote wa mchakato huu.
Wanachama wetu 173,593 walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kwa kujaza fomu za uteuzi na kuzirejesha na wengine wengi kwa maelfu walikataliwa kupewa fomu na au ofisi kufungwa kwa wakati wote. Wagombea Uenyekiti wa Mitaa walikuwa 2,481 kati ya Mitaa yote 4,264 nchini, Uenyekiti wa Vijiji walikuwa 8,218 katika ya Vijiji vyote 12,316 nchini, na uenyekiti wa Vitongoji walikuwa 35,457 kati ya Vitongoji vyote 64,384 nchini. Kwa upande wa Wagombea wa nafasi za Ujumbe wa Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mtaa (wajumbe wa kawaida na wajumbe Wanawake) wanaACT 135,675 walijitokeza kuomba nafasi hizo.
Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.
Sababu zote zilizotolewa na Serikali na Chama cha Mapinduzi kuondoa wanachama wetu katika kinyanganyiro cha Uchaguzi hatukubaliani nazo. Kamati ya Uongozi ya Chama taifa iliyoketi leo imeelekeza kuwa wanachama wetu wote waliobakizwa katika Uchaguzi WAJIONDOE katika Uchaguzi huo kwani kushiriki kwao ni kuhalalisha ubakaji wa Demokrasia uliofanywa na Serikali. Kwani kwa uenguaji huu wa wagombea kwa kutumia sababu zisizo na mantiki, si tu wamenyima wagombea wetu haki yao kikatiba, bali wamewanyima Wananchi wote wa Tanzania waliotimiza miaka 18 na zaidi haki yao, iliyopo katika Ibara ya 5 ya Katiba, ya kupiga kura. KWA KUWA CCM IMEONDOA WAGOMBEA WETU asilimia 96%, na sisi TUMEWASAIDIA KUONDOA asilimia 4% ya WALIOBAKIA.
Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa inaona kuwa Dola imeshatuamulia vyama makini vya upinzani tusishiriki kwenye uchaguzi huu. Hawataki ushindani. Wanaogopa ushindani. Wanaogopa sanduku la kura. Wanawaogopa Watanzania. Kwa msingi huo, Kamati ya Uongozi inaona hakuna mantiki ya kushiriki uchafuzi ambao asilimia 96 ya wagombea wetu wameenguliwa. Unashiriki vipi uchaguzi ambao wagombea wako wameondolewa? Kamati ya Uongozi imeamua kuwaachia CCM uchafuzi wao na kwa hivyo ACT - Wazalendo inajiondoa kwenye uchafuzi huo.
Mwaka jana mwishoni, baada ya majadiliano marefu na wenzetu katika Upinzani, tulipitisha na kulitangza Azimio la Zanzibar, ambalo liliutangaza mwaka 2019 kuwa ni “MWAKA WA KUDAI DEMOKRASIA”, mwaka ambao tungepambana kuzidai haki zetu zote tunazonyimwa kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujalitekeleza hilo, kwa matendo ya sasa ya CCM na Serikali, tumepewa nafasi ya kutekeleza Azimio la Zanzibar. ACT-Wazalendo tutakwenda kwa wenzetu wa Upinzani, ili kurudi kutekeleza Azimio la Zanzibar.
TUNAWAPA ARI wanachama na wafuasi wetu, pamoja na wananchi wote kwa ujumla, wakati ni sasa wa kuondoa hofu, kushikamana nasi katika kulinda Demokrasia ya nchi yetu. Hatupaswi kuwa waoga, hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja mmoja na kama KUNDI ZIMA LA KIJAMII.
Tumejitahidi kufuata njia zote za kisheria Lakini CCM na Serikali yake wameamua vinginevyo kwa kutuondoa katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Tumeamua kutafuta njia nyingine za kulinda demokrasia yetu. TUSILAUMIANE.
Mwisho; Kumekuwepo na vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na watendaji wa Serikali kuwabughudhi Wagombea wetu, wanachama na viongozi wetu maeneo mbalimbali nchini. Serikali ya Rais Magufuli isitufikishe kuvuka mstari wa Uvumilivu.
Kabwe Z, Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Dar es Salaam.
Novemba 8, 2019
😆😆😆Wananchama wa CCM hawana ubavu au uvumilivu walio nao Upinzani ,wakibanwa kidogo tu wanaachia Miguu.
Mahakama ipi , hii ya Jaji Mkuu anayelamba miguu ya Jiwe ?Msipokwenda mahakamani kudai haki mtakua wanafiki wa kiwango cha lami
Bado Nccr Mageuzi na pengine CUF Lipumba kama hajapewa pesa.
Vile vyama vingine ni majina tuu kwenye daftari la Msajili
Huu utabaki kuwa uchaguzi wa ndani wa CCMHata hao NCCR wasilazimishwe waachwe waamue wenyewe, lakini wananchi wameshasusia huo uchaguzi, hata wakishiriki hawatakuwa na mtu wa kuwapigia kura. Huwa uchaguzi umeshatiwa najisi, hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu atashiriki huo ushenzi.
November 7, 2019
Dar es Salaam, Tanzania
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba -" Sijawahi kuona uchaguzi wa kihuni ktk nchi hii toka uhuru wa Tanganyika upatikane".
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba -" Sijawahi kuona uchaguzi wa kihuni ktk nchi hii toka uhuru wa Tanganyika upatikane" , Mwisho wa kumnukuu Mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF.
Prof. Lipumba aufananisha uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji unaoratibiwa wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyo chini ya Ofisi ya Rais kuwa kinachoendelea ni uchafuzi wa amani na siyo uchaguzi.
Mwenyekiti wa CUF alisema badala ya kupoteza kuandaa uchaguzi huu batili ni bora serikali ya CCM ingepeleka muswada wa mwendokasi Bungeni ili bunge hilo lenye wingi wa wabunge toka CCM wabadili sheria ya vyama vingi, nchi iwe ya chama kimoja tu kuokoa fedha za walipa kodi kujenga shule na vituo vya afya badala ya kufanya vituko vya namna hii kuviita uchaguzi wa serikali za mitaa Tanganyika.
Source: DARMPYA TV