Chama cha ACT - Wazalendo chajiondoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Naunga mkono Zitto Kabwe kukiondoa ACT wazalendo kugombea .Hicho Chama kwenye daftari la msajili hakipo.Kilichopo ni Chama Cha ACT.

Hicho chake Cha mdomoni Cha ACT wazalendo hakipo.Hakuna jina Hilo.kwenye Ofisi ya msajili Wala kwenye katiba ya ACT kifungu Cha kwanza Cha katiba ya ACT ya mwaka 2015
 
Umeandika kwa uchungu sana mwanangu
 
Ndomana msemaji.mmoja alisema dawaamul hal minalmuhaal
 
Barikiwa sana mkuu, acha ccm ifanye kila inataka, lakini malipo ni hapa hapa duniani
 
Msipokwenda mahakamani kudai haki mtakua wanafiki wa kiwango cha lami
 
ACT waache utoto. Zitto atutajie jimbo lake la zamani wagombea Wa ACT ni wangapi waliochukua fomu. Watu wamechemka wanasingizia vioja.

Upinzani uache tabia za kuokoteza wagombea kipindi cha kampeni. Ndio mnaingizwa mkenge na wagombea wenu
 
Bado Nccr Mageuzi na pengine CUF Lipumba kama hajapewa pesa.
Vile vyama vingine ni majina tuu kwenye daftari la Msajili

November 7, 2019
Dar es Salaam, Tanzania
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba -" Sijawahi kuona uchaguzi wa kihuni ktk nchi hii toka uhuru wa Tanganyika upatikane".

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba -" Sijawahi kuona uchaguzi wa kihuni ktk nchi hii toka uhuru wa Tanganyika upatikane" , Mwisho wa kumnukuu Mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF.

Prof. Lipumba aufananisha uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji unaoratibiwa wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyo chini ya Ofisi ya Rais kuwa kinachoendelea ni uchafuzi wa amani na siyo uchaguzi.

Mwenyekiti wa CUF alisema badala ya kupoteza kuandaa uchaguzi huu batili ni bora serikali ya CCM ingepeleka muswada wa mwendokasi Bungeni ili bunge hilo lenye wingi wa wabunge toka CCM wabadili sheria ya vyama vingi, nchi iwe ya chama kimoja tu kuokoa fedha za walipa kodi kujenga shule na vituo vya afya badala ya kufanya vituko vya namna hii kuviita uchaguzi wa serikali za mitaa Tanganyika.
Source: DARMPYA TV
 
Hata hao NCCR wasilazimishwe waachwe waamue wenyewe, lakini wananchi wameshasusia huo uchaguzi, hata wakishiriki hawatakuwa na mtu wa kuwapigia kura. Huwa uchaguzi umeshatiwa najisi, hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu atashiriki huo ushenzi.
Huu utabaki kuwa uchaguzi wa ndani wa CCM
 
So na yeye amesusa au?ili tujue moja asije akalia lia halafu akashiriki kwny uchafuzi huo.

 
Kwa kujitoa wapinzani, sasa naazimia rasmi kuwa mpinzani wa kweli. Kilicho kuwa chama changu cha ccm kitatuletea vita.
 
Safi sana... Ngoja tuone...

Hizo fomu inaonekana kama vile, zilikua zinatolewa na vibaraka wa chama tawala...


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…