Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.
Itathibitika pasipo shaka, proven beyond reasonable doubt, kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi, scraped from the book of political parties, mara moja na bila huruma yoyote!.

Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifanyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.

Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa vyama, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.

Niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana "beyond reasonable doubt!" na "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika viongozi wakuu wa CHADEMA waliijua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili Tendwa, atakifuta rasmi Chama cha CHADEMA, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo katiba ya nchi inavyosema!, na yeye ameapa kuilinda katiba hiyo!.

Nikadadisi zaidi, iwapo hayo kwa CHADEMA, yatathibitika kuwa kufanywa na CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Msajili kwanza alisita kidogo na kusema kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa hayo, hakiwezi kufutwa right away kwa sababu huko kutakuwa ni kuvunja serikali iliyopo madarakani, bali atakipeleka Mahakama Kuu ili mahakama itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!. Hii inamaanisha as of now, hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.

My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio mamlaka ya msajili wa vyama, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kusitahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake, watu wakaishia kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki!.

Kwa kumalizia, nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na watu ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa viongozi wa taifa hili!.

Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha.

Najua kuna wenzetu humu, kwa JF ni favorite past time na huja humu wakati hawana kitu kingine cha kufanya!.
Nawaomba mtuhurumie sisi ambao JF ni nyumbani kwetu, ni sebuleni kwetu na chumbani kwetu, tunashinda JF, tunalala JF, tunaamka JF, in short tunaiishi JF, kwetu JF is life we are living for!.

Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.

Duuuh! Ikithibitika mahakamani, hao CDM wafutwe tu.
 
Kumbuka vizuri, Ninavyokumbuka alisema ili sisiem ishinde ni lazima wagombea waanze na majina ya C otherwise haitoshinda. Na kama ataingia mwingine mwenye majina yasiyoanza na C basi anaondoka yeye.

hiyo labda alikwambia wewe, lakini the common one was "...yeyote atakayempinga Kikwete kwenye uchaguzi mkuu 2010 mauti yangemfika" msikilize hata Roma Mkatoliki anaikumbuka vizuri hii!
 
Hata hivyo ni tafsiri potofu ya sheria - kwani sheria ya usajiri na kufutwa kwa usajiri inahusu vyama vya siasa bila kujali ni chama tawala au cha upinzania. Hakuna sheria exclusive pale. Kama kufutwa kwa chama kutamaanisha ni kufutwa kwa serikali iliyopo madarakani hilo ni jambo lingine lisilo mhusu yeye kama msajiri wa vyama vya kisiasa. Hilo litakuwa ni jambo la mgogolo wa kikatiba. Mahakama ya Katiba ambayo haipo isipokuwa likitokea jambo kama hilo basi ndo kazi yake. Sheria ya usajiri wa vyama vya siasa haina upekee wa chama tawala - vyote ni vya siasa na mwongozo wake ni mmoja tu.

Mahengela umemaliza kabisa mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Pasco, msajili wa vyama vya siasa yupo hapo kuitumikia serikali ya CCM. Hivyo basi kuifuta CCM itamaanisha kuwa msajili wa vyama anayeishi kiujanja ujanja kwa huruma ya CCM maisha yake pia yatakosa muelekeo. Hivyo, yupo tayari kuifuta chadema ili mradi ujira wake unalindwa na CCM. Kama ulivyotanabaisha kuhusu 'mgogoro wa kikatiba', mgogoro ni mkubwa sana hasa kwenye mamlaka ya raisi kuteua watendaji wakuu wa baadhi ya vyombo vinavyopaswa kuwa huru ili kujenga demokrasia. Walau bunge lipewe mamlaka ya ama kuthibitisha ama kutengua teuzi za raisi, hapo tunaweza kupata akina Tendwa wenye uthubutu wa kukiwajibisha chama tawala.
 
Pasco,
uvivu wako wakusoma nakukubali cheap answers utakupa tabu sana ktk maisha siku sheria zipo wazi msajili hana
ubavu wa kufuta chama na kama angekuwa nao angeshafanya hivyo siku nyingi hana ubavu huo. msajili inambidi aende mahakamani kabla alivyozungumzia kwy issue ya CCM kuishawishi mahakama kuhusiana na hayo anayowashutumu nao na mahakama ikubaliane nae kitu amabacho hana ubavu nacho ndio maana unamuona amekuwa kama junk dog kupiga kelele tu na mara nyingine kudhalilishwa na tume ya uchaguzi kwa kuingilia kazi zisizo za kwake.
kwa ufupi ofisi yake ingebidi ifutwe kwani ina limit uhuru wa watu kujumuika kwa namna wanavyotaka wenyewe.

Politiki,

Nakuunga mkono.

Mimi narudia maneno yangu yaleyale kwamba kwa sasa CCM wameshazidiwa nguvu na CHADEMA pamoja na kwamba CCM ndiyo wako madarakani. Watanzania walio makini wameshajua na wanajua kuwa CCM kwa sasa wanatafuta kila upenyo au opportunity yoyote iwe nzuri au mbaya ya kuweza kuihusisha CHADEMA na UGAIDI ili iwe na sifa ya kuwa scrapped from the list of Political parties in Tz!

Ukiona mtu anashabikia kufutwa kwa Chama kama CHADEMA basi ujue huyo ni sehemu ya mikakati hiyo miovu inayopangwa ucku na mchana na viongozi wa CCM ili kuhakikisha CHADEMA kinafutwa haraka iwezekanavo kabla ya GE-2015.Hili jambo liko wazi kwa kila Mtanzania na CCM wanajua hilo!!!

Bwana Pasco ni sehemu ya mtandao huo muovu wa kuiangamiza CHADEMA. Watu wa aina ya kina Pasco ni hatari sana katika nchi hii. Hawa ni watu walionunuliwa na CCM ili kuhakikisha wanailinda,kuitetea na kuinusuru CCM ising'olewe madarakani.

Alichokiandika Bwana Pasco hapa ni katika mbinu zilezile za kujaribu kucheza na akili za Watanzania ili waendelee kuamini kwamba CHADEMA ni chama cha Kigaidi. Inachekesha na kusikitisha iwapo kweli Bwana Pasco alikutana na huyo Msajili wa Vyama Bwana John Tendwa, wakazungumzia swala la kuifuata CHADEMA na kukubaliana iwapo itathibitika beyond resoanable doubt kuwa CHADEMA wanahusika na UGAIDI watafutiliwa mbali toka Daftari la msajili wa Vyama!!!!Hayo ni maneno mazito sana kuyatamka hivihivi!

Wakati tunatafakari maneno haya ya Bwana Pasco na John Tendwa, Watanzania na mimi mwenyewe binafsi ningependa kuwauliza Bwana Pasco na Tendwa swali hili: Walikuwa wakirejea(reference)ya KESI GANI iliyoko Mahakamani ambayo itathibitika kuwa CHADEMA wanahusika na Ugaidi ili wafutwe????Maana tayari Mahakama Kuu juzi imetupilia mbali mashtka yote matatu yaliyokuwa yameelekezwa kwa Lwakatare kuwa ni ya Kigaidi kufuatia ile Video ya kina Mwigulu Nchemba na Nnepi Nauye!!!Je, kuna kesi nyingine inayotengenezwa kuihusisha CHADEMA na ugaidi???? Naomba Bwana Pasco awaeleze Watanzania au Tendwa mwenyewe maana tumeambiwa na huyu rafiki yake kuwa naye huwa anapitiapitia humu jamvini!!!

Tayari kuna tetesi kwamba Bomu la Olasiti kule kanisani linaweza likaunganishwa na Ugaidi wa CHADEMA!!!!!!!!!Watanzania hatutashangaa kwasababu huu ni mpango mkakati wa kuimaliza CDM. Kwa vile CCM inaweweseka inaweza kufanya vituko ambavyo Dunia nzima itabaki ikiduwaa. Mfano live ni lile tuukio la juzi pale Chuo cha Uhasibu Arusha. Kwamba mwanachuo ameuawa na majambazi,vibaka au bifu na vitu namna hiyo lakini BADALA YA MKUU WA MKOA KUAGIZA POLISI WAKAWASAKE WALIOSABABISHA MAUAJI YA MWANACHUO, YEYE ALIAGIZA MBUNGE LEMA ASAKWE NA KKAMATWA KANA KWAMBA YEYE NDO MUUAJI NA TAYARI KUNA KESI MAHAKAMANI!!!!

Kwa hiyo hatutashangaa kusikia kuwa waliolipua Bomu pale kanisani Olasiti ni CHADEMA kwa vile hiki chama ni cha magaidi!!!Lakini CCM wanatakiwa kutafakari na kupima huu ujinga,upumbavu na uhuni wanaotaka kuupandikiza na kuwaaminisha Watz mwisho au hatima yake ni nini kwa mstakabali wa Taifa letu.

Watu tusije tukashangaa tutakapoona Video nyingine ya Lwakatare na Ludovick au Dr.Slaa na Lema,au Mbowe na Tundu Lissu hapa Mtandaoni wakipanga njama za kwenda kulipua Kanisa la RC kule Olasiti-Arusha.Binafsi sitashangaa kwa sababu ni vitu ambavyo vinajionyesha wazi kabisa kuwa vinaandaliwa na CCM kwa maksudi!!

Tusubirini vioja bado vinakuja!
 
HIVI KUMUONDOA CHEYO NA MREMA kuna tofauti gani na kuwaondoa SLAA na MBOWE? Si hao ndiyo CDM yenyewe? Ukiwaondoa kuana CHADEMA Tena? Lema, Sugu, Nasari, ABWAO NA wengine si kazi yao ni kulamba miguu wa hao mabosi wao tu na wakiondoka huwezi kuwasikia tena.

Kwa hiyo ukimwondoa kikwete CCM kwisha. na kwa msingi huo CCM bye bye 2015. Hongera mzee wa musoma.
 
Loo sikuzote sikio la kufa halisikii dawa.Kwanza huyu bwana Tendwa muda wake wa kazi umeisha au hujui hilo anaendelea kufanya kazi kwa sababu analindwa na CCM na kwakuwa anafanya kazi ya CCM lakini anachezea pabaya sana CHADEMA ni kitu kingine kuliko mnavyofikilia.Tatizo lenu mnajifungia ndani mnadhani hali kwa watu ni shwari ndugu yangu watu wanawalaani nyie CCM kwa vitendo mnavyo fanya kwa watu.Watu hawasemi lakini pita mitaani hata yule hasiye na akili yaani ndondocha anawacheka.Mambo yakujidanganya mkidhani bado watu wanafikra kama za zamani za kidumu chama cha mapinduzi zitawaponza.Matatizo yanayotokana na uzembe wenu wa kufikiri ni mengi sana na ndo yanayoligharimu taifa.Ww jaribu kuangalia matatizo kama yanayotokea mtwara na lindi watawala wanajidanganya wakidhani hali ni shwari kumbe kume kujwa manzee ni hatari kupikia petroli kwenye jiko la mchina.Alafu ww uliyeleta mada hii mbovu hata hujui kujieleza na utashangaa ww ni mkuu wa wilaya kwa kweli taifa linaumwa ugonjwa usio na kinga,tiba wala kupunguzwa makali kama ukimwi wa utawala wa CCM.Nawaambia laana za watanzania zitawaandama akina mwigulu na ww unayeshabikia upuuzi huu wa kuumiza watanzania ili kulinda maslai yenu binafsi.WW jiulize toka Mwangosi ameuawa unadhani wanatafuta ushaidi gani kutoa adhabu au unadhani kitendo cha waziri wa mambo ya ndani kumsifikia KAMUANDA ni akili hiyo?Ulimboka,Kibanda,Lwakatare wote wanateseka kwa sababu ya tamaa za maCCM.Mwisho naomba ushangae nguvu kubwa anayoitumia Mwigulu na msaidizi wake Nape juu ya Lwakatare wakati viongozi wengine wamekaa kimya huoni ni ujinga na uzuzu mkubwa?HATA CHADEMA IZIMWE IPOTEZWE TUTAIPINGA CCM KWA NGUVU ZOTE KWA MAOVU YOTE WANAYOTUTENDEA WATANZANIA.
 
Pasco kuna kitu unakijua husemi
Mkuu The "B" Boss, ninachokijua nni kitu kimoja tuu!, "Bonafide Genuine!".
Wengi humu wanazunghumzia tuu "actus reaus" ya ile "bonafide genuine!"
None anazungumzia "mens rea" ya hiyo "bonafide genuine!" ambayo huwezi kuipata bila kujua "the motive behind!" na "the underlying facts!". Saa hizi wengi wanafikiri its just a joke!. When that joke turns into reality!, msije kulalamika humu kuwa "its unfair!" wakati mlisha ambiwea kila kitu like "buyer be ware!".
Pasco
 
Itathibitika pasipo shaka, proven beyond reasonable doubt, kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi, scraped from the book of political parties, mara moja na bila huruma yoyote!.

Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifanyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.

Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa vyama, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.

Niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana "beyond reasonable doubt!" na "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika viongozi wakuu wa CHADEMA waliijua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili Tendwa, atakifuta rasmi Chama cha CHADEMA, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo katiba ya nchi inavyosema!, na yeye ameapa kuilinda katiba hiyo!.

Nikadadisi zaidi, iwapo hayo kwa CHADEMA, yatathibitika kuwa kufanywa na CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Msajili kwanza alisita kidogo na kusema kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa hayo, hakiwezi kufutwa right away kwa sababu huko kutakuwa ni kuvunja serikali iliyopo madarakani, bali atakipeleka Mahakama Kuu ili mahakama itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!. Hii inamaanisha as of now, hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.

My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio mamlaka ya msajili wa vyama, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kusitahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake, watu wakaishia kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki!.

Kwa kumalizia, nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na watu ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa viongozi wa taifa hili!.

Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha.

Najua kuna wenzetu humu, kwa JF ni favorite past time na huja humu wakati hawana kitu kingine cha kufanya!.
Nawaomba mtuhurumie sisi ambao JF ni nyumbani kwetu, ni sebuleni kwetu na chumbani kwetu, tunashinda JF, tunalala JF, tunaamka JF, in short tunaiishi JF, kwetu JF is life we are living for!.

Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.
Tendwa is such an incompetent lawyer that can not stand before any learned friend with such idiot sort of decisions. He is partial, slippery, unobjective and unfocussed. Must have got an LLB through the party supremacy era!!
 
Mkuu The "B" Boss, ninachokijua nni kitu kimoja tuu!, "Bonafide Genuine!".
Wengi humu wanazunghumzia tuu "actus reaus" ya ile "bonafide genuine!"
None anazungumzia "mens rea" ya hiyo "bonafide genuine!" ambayo huwezi kuipata bila kujua "the motive behind!" na "the underlying facts!". Saa hizi wengi wanafikiri its just a joke!. When that joke turns into reality!, msije kulalamika humu kuwa "its unfair!" wakati mlisha ambiwea kila kitu like "buyer be ware!".
Pasco

tatizo ule mstari wa madudu ya ccm na madudu ya chadema haupo kwa baadhi ya watu
so reaction sijui zitakuwaje..

kwa wengine chadema ni clean 100 percent na ccm ni chafu 100 percent...hapo ndo tabu ilipo
 
Haya ni ya leo, kuhusu somo hili!.

attachment.php


​

Aliyekuwa mlinzi binafsi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi ndani ya chama hicho.

Akizungumza kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari leo, amesema kuwa kilichotokea hakijui ila anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza na halina ukweli wowote ule.

attachment.php


​

Amesema kutokuelewana kwake na Katibu Mkuu wa chama hicho kulianza pale alipoanza kupishana kwa maneno kati yake na mke wa Dk. Slaa ambapo Slaa alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa hakuwa na ugomvi na mke wa Dk. Slaa na hakuweza kufanya hivyo.

Amesema kuwa siku ya Jumamosi aliitwa Makao Makuu ya chama kwa mualiko kuwa kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa chumbani ambapo aliwakuta vijana watano wa chama hicho ambao amewataja kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke, kumtesa, kumvua nguo, kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu na viongozi wa chama cha CCM ili amuue katibu mkuu dk. Slaa.

attachment.php


​

"Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu na wanataka kunichafua kwa jamii, tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea."

"Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa Slaa kwa muda wa miaka mingi sana, tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki" amesema Kagenzi

Katika Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefichua mipango ya kitesaji na kigaidi inayofanya na CHADEMA huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.

"Jamani hiki chama ambacho kina ndoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia? Maana wameniteka na kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu na kuweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote, eti wakinishinikiza mimi nitaje wanaonituma, jamani nawaambia mimi hanitumi mtu" ameedelea kusema Kagenzi.

Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .

Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa mwezi lakini anasema kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.

Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa

Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawahi kupokea pesa hizo.

Hatua atakazochukua



Kagenzi amesema hatua iliyobaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubiri kesi mahakamani ili kukishtaki chama hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai ni vya kiuaji.

Haya yakithibitika kuwa ni kweli yametendeka!, then....

Itakuwaje?!.

Pasco
 
tatizo ule mstari wa madudu ya ccm na madudu ya chadema haupo kwa baadhi ya watu
so reaction sijui zitakuwaje..

kwa wengine chadema ni clean 100 percent na ccm ni chafu 100 percent...hapo ndo tabu ilipo
Haya ni maneno makali sana!.

Pasco
 
KOMAA maana naamini yako mengi mtaibua,,,endeleeni kulia mkidhani kwa staili mtapata huruma ya umma!,,, niwashauri k2,,......chukueni ha2a .....kama hamuwezi PISHA.,2MECHOSHWA NA PROPANDA ZENU.
 
KOMAA maana naamini yako mengi mtaibua,,,endeleeni kulia mkidhani kwa staili mtapata huruma ya umma!,,, niwashauri k2,,......chukueni ha2a .....kama hamuwezi PISHA.,2MECHOSHWA NA PROPANDA ZENU.

Maccm mapumbavu sana tamemtuma aje avue shati kwa wanahabar.ni ushenz wa hal ya juu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom