Unachoandika ni tofauti na hoja iliyojengwa awali kuhusu chama kuwa cha Mungu. Mungu ashindwi kitu...
Israel waliikaa utumwani miaka 400 lakini ndio taifa teule la Mungu.
Mungu huwa achelewi wala awahi yeye ujibu kwa wakati.
Moja ya jambo la kimbulula ni hii statement ya Taifa teule! Huu ni uongo.
Itathibitika pasipo shaka, proven beyond reasonable doubt, kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi, scraped from the book of political parties, mara moja na bila huruma yoyote!.
Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifanyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.
Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.
Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa vyama, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.
Niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana "beyond reasonable doubt!" na "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika viongozi wakuu wa CHADEMA waliijua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili Tendwa, atakifuta rasmi Chama cha CHADEMA, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo katiba ya nchi inavyosema!, na yeye ameapa kuilinda katiba hiyo!.
Nikadadisi zaidi, iwapo hayo kwa CHADEMA, yatathibitika kuwa kufanywa na CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Msajili kwanza alisita kidogo na kusema kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa hayo, hakiwezi kufutwa right away kwa sababu huko kutakuwa ni kuvunja serikali iliyopo madarakani, bali atakipeleka Mahakama Kuu ili mahakama itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!. Hii inamaanisha as of now, hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.
My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio mamlaka ya msajili wa vyama, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kusitahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake, watu wakaishia kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki!.
Kwa kumalizia, nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na watu ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa viongozi wa taifa hili!.
Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha.
Najua kuna wenzetu humu, kwa JF ni favorite past time na huja humu wakati hawana kitu kingine cha kufanya!.
Nawaomba mtuhurumie sisi ambao JF ni nyumbani kwetu, ni sebuleni kwetu na chumbani kwetu, tunashinda JF, tunalala JF, tunaamka JF, in short tunaiishi JF, kwetu JF is life we are living for!.
Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.
Mr. Zero, mdomo huumba!, hili la kujiita Mr. Zero, hata kama kiukweli unaakili, kitendo cha kujiita zero, akili zako nazo zinakuwa zero kabisa!, yaani hapo ulipo ni zero!. Rudi kwenye hizo thread zangu pamoja na hii, soma tarehe zilianzishwa lini!.Sasa sina tena shaka Pasco umesajiliwa rasmi Lumumba. Hizi haziwezi kuwa ni hasira tu za Zitto kufukuzwa CDM. Siku zote nilikuwa naamini uko nutural, lakini hizi propaganda ulizoziibua tangu Zitto afukuzwe zimenifanya nidoubt hata uzalendo wako. Siku mbili thread 3 tena zote za propaganda!!! Kama mwandishi huru kama unavyodai nilitegemea uje na analysis ya Tukio badala yake umekuwa too biased kwenye whole issue.
"Bonafide genuine" maana yake ni nini?
Mr. Zero, mdomo huumba!, hili la kujiita Mr. Zero, hata kama kiukweli unaakili, kitendo cha kujiita zero, akili zako nazo zinakuwa zero kabisa!, yaani hapo ulipo ni zero!. Rudi kwenye hizo thread zangu pamoja na hii, soma tarehe zilianzishwa lini!.
Usingekuwa zero, kabla hujachangia ungeona hii thread imeanzishwa tarehe 4 Maya, 2013!.
Nakushauri badili jina, usiendelee kujiita zero, sio unahatari ya kuwa zero humu jf tuu, unaweza kuishia hadi kuwa zero kwenye kila kitu!.
Pasco
Huyu alikuwa John Tendwa, nitamtafuta Jaji Mutungi kabla ya September Mosi, ili kuusikia msimamo wake, ili itakapofika hiyo September mosi, watu wajue huo unaweza kuwa ndio mwanzo wa mwisho wa kilichokuwa kikijulikana kama Chama Cha ....Wanabodi,
Iwapo itathibitika pasipo shaka, (proven beyond reasonable doubt), kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi toka ndani ya daftari la vyama vya siasa, (scraped from the book of political parties), mara moja na bila huruma yoyote!.
Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifyonyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.
Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia mara kwa mara, ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.
Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.
Katika maongezi yetu kuhusu hali ya siasa hali ya siasa nchini, niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana " proved beyond reasonable doubt!" by "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA walihusika kwa kujua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili wa vyama nchini, Jaji John Tendwa, atakuwa hana option nyingine, bali kukifuta rasmi Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini, yaani CHADEMA, toka ndani ya daftari la vyama vilivyosajiliwa, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo sheria ya vyama vya siasa inavyoelekeza kwa mujibu wa katiba ya nchi hii! ambayo yeye ameapa kuilinda.
Kwa kifupi amemaanisha iwapo chama cha siasa kitathibitika kufanya ugaidi, kitafutwa!.
Hata hivyo nikadadisi zaidi, iwapo tuhuma za ugaidi zatathibitika kufanywa na chama tawala CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Baada ya swali hilo, kwanza Msajili alisita kidogo na baadae kusema kuwa kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa ya ugaidi, hatakifuta right away eti kwa sababu ni chama tawala!, kukifuta chama tawala ni kuvunja serikali iliyopo madarakani!, CCM kikifanya ugaidi, hata kivunja, bali atakipeleka mahakamani ili mahakama ndio itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!.
Hii inamaanisha as of now, Tanzania bado hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali iliyopo madarakani nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni serikali dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata chama hicho kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.
My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio ya double standards za mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kustahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake kwa kuvifuta, watu wakaishia kupiga kelele na kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki, waki vyama vingine, vikifanya makosa yale yale, vikiachwa eti kwa sababu ni chama tawala!.
Pia nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na baadhi ya watu ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa serikali na viongozi wa taifa hili!. Nilimwambia hiyo ndia maana halisi ya social forums, watu kujiachia watakavyo!.
Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha kwa watu wote wakiwemo viongozi wa kitaifa!.
Najua kuna wenzetu humu, kwao JF ni favorite past time na huja humu wakati hawana shughuli au kitu kingine cha kufanya!, nawaomba mtuhurumie sisi ambao kwetu JF ni zaidi ya nyumbani kwetu, jf ni sebuleni kwetu, jf ni chumbani kwetu, jf ni kitandani kwetu, tunashinda JF, tunakula jf, tunalala JF, tunaamka JF, in short kwa sisi wengine wetu, jf ndio kila kitu kwetu, tunaiishi JF, yaani kwetu JF is our life that we are living for!.
Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.
Ramli zako zinaendelea,sawa endelea!Huyu alikuwa John Tendwa, nitamtafuta Jaji Mutungi kabla ya September Mosi, ili kuusikia msimamo wake, ili itakapofika hiyo September mosi, watu wajue huo ndio mwanzo wa mwisho wa kilichokuwa kikijulikana kama Chama Cha ....
Pasco
Mkuu Bomihi, Watanzania ni wavivu kusoma, kwa sababu tunapenda mambo rahisi rahisi, hoja nyepesi nyepesi, na maswali rahisi rahisi, bandiko likiwa refu hawawezi kusoma kilichoandikwa ndani, huishia kusoma headlinetuu, amemaliza, na kukoment!.Ramli zako zinaendelea,sawa endelea!
@Pasco,1st sept imepangwa kama siku ya kufanya mikutano nchi nzima!Mikutano ambayo imepewa nguvu na katiba lakini pia na sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu!Lengo la mikutano hiyo limewekwa wazi na hilo wanalipigia kelele kila siku!Mkuu Bomihi, Watanzania ni wavivu kusoma, kwa sababu tunapenda mambo rahisi rahisi, hoja nyepesi nyepesi, na maswali rahisi rahisi, bandiko likiwa refu hawawezi kusoma kilichoandikwa ndani, huishia kusoma headlinetuu, amemaliza, na kukoment!.
Essence ya bandiko hili ni Msajili ana mamlaka ya kukifuta chama chochote akiwa na sababu, lakini hawezi kukifuta CCM hata kifanye nini!. Thank God, JK alikuwa ni mtu mpole akavivumilia sana baadhi ya vyama vinavyohatarisha amani na utulivu wa taifa hili, huyu aliyepo ni namba nyingine, mamlaka ya kisheria, yaliyopo kwa msajili ambayo hayajatumika, yakianza kutumika ipasavyo, tusije kupiga kelele humu kuwa tunaonewa!.
Pasco
Mkuu Bomi, katiba yetu imetoa haki kwa mkono mmoja na kuziondoa haki hizo kwa mkono mwingine!. Haki ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, na sheria ya vyama vya siasa vinaitambua haki hii, sheria ikiishatungwa, hutungiwa kanuni na taratibu za utekelezaji, kwenye kanuni, ili mikutano na maandamano hayo yawe halali kwa mujibu wa sheria, lazima yapate kibali cha OCD wa eneo husika, maadam Amiri Jeshi Mkuu ameishasema hataki maandamano wala mikutano, hivyo hakuna OCD atakayetoa kibali cha mkutano wala cha maandamano!. Kitendo cha Chadema kushikilia msimamo wa mikutano na maandamano kwa kibali au bila kibali, ndio kitisho chenyewe cha amani hiki, yaani Chadema wanataka kupimana ubavu na Magufuli!.@Pasco,1st sept imepangwa kama siku ya kufanya mikutano nchi nzima!Mikutano ambayo imepewa nguvu na katiba lakini pia na sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu!Lengo la mikutano hiyo limewekwa wazi na hilo wanalipigia kelele kila siku!
Hakuna sehemu yeyote inayohamasisha vurugu,sijamsikia kiongozi yeyote akisema watu wapigane au wavamie maeneo ya watu!Isitoshe hili halijawahi kuwa lengo la upinzani hasa CDM!
Sasa hizi Ramli za kusema kitafutiwa usajili ikibainika hivi au vile zinatoka wapi?Hakuna hata element inayoonesha hayo,haki haiombwi bali hudaiwa!
"Angalizo,kama nchi hii wanataka kuona inafika kubaya basi msajili afanye hilo unalopigia ramli litokee"
Ni kweli Haki zilizotolewa kikatiba zimetungiwa kanuni,lakini katiba yenyewe inasema sheria yeyote haitakiwi kukinzana na primary objective yake,yaani yenyewe ni sheria mama!Ndio maana juzi umesikia mahakama imemng'oa meno DPP kwa kuondoa kifungu kinachopingana na katiba!Mkuu Bomi, katiba yetu imetoa haki kwa mkono mmoja na kuziondoa haki hizo kwa mkono mwingine!. Haki ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, na sheria ya vyama vya siasa vinaitambua haki hii, sheria ikiishatungwa, hutungiwa kanuni na taratibu za utekelezaji, kwenye kanuni, ili mikutano na maandamano hayo yawe halali kwa mujibu wa sheria, lazima yapate kibali cha OCD wa eneo husika, maadam Amiri Jeshi Mkuu ameishasema hataki maandamano wala mikutano, hivyo hakuna OCD atakayetoa kibali cha mkutano wala cha maandamano!. Kitendo cha Chadema kushikilia msimamo wa mikutano na maandamano kwa kibali au bila kibali, ndio kitisho chenyewe cha amani hiki, yaani Chadema wanataka kupimana ubavu na Magufuli!.
Msajili wa vyama ana uwezo wa kukifuta chama chochote isipokuwa chama tawala, thread hii ni angalizo tuu Chadema, ikishindana na mwenye nguvu, itaumia!. CCM hata wafanye nini, hawafanywi kitu lakini Chadema au CUF, cha moto watakipata.
Pasco