Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.
Sasa sina tena shaka Pasco umesajiliwa rasmi Lumumba. Hizi haziwezi kuwa ni hasira tu za Zitto kufukuzwa CDM. Siku zote nilikuwa naamini uko nutural, lakini hizi propaganda ulizoziibua tangu Zitto afukuzwe zimenifanya nidoubt hata uzalendo wako. Siku mbili thread 3 tena zote za propaganda!!! Kama mwandishi huru kama unavyodai nilitegemea uje na analysis ya Tukio badala yake umekuwa too biased kwenye whole issue.
 
Last edited by a moderator:
Unachoandika ni tofauti na hoja iliyojengwa awali kuhusu chama kuwa cha Mungu. Mungu ashindwi kitu...

Israel waliikaa utumwani miaka 400 lakini ndio taifa teule la Mungu.
Mungu huwa achelewi wala awahi yeye ujibu kwa wakati.
 
Israel waliikaa utumwani miaka 400 lakini ndio taifa teule la Mungu.
Mungu huwa achelewi wala awahi yeye ujibu kwa wakati.

Moja ya jambo la kimbulula ni hii statement ya Taifa teule! Huu ni uongo.
 

John Tendwa?
 
Mr. Zero, mdomo huumba!, hili la kujiita Mr. Zero, hata kama kiukweli unaakili, kitendo cha kujiita zero, akili zako nazo zinakuwa zero kabisa!, yaani hapo ulipo ni zero!. Rudi kwenye hizo thread zangu pamoja na hii, soma tarehe zilianzishwa lini!.

Usingekuwa zero, kabla hujachangia ungeona hii thread imeanzishwa tarehe 4 Maya, 2013!.

Nakushauri badili jina, usiendelee kujiita zero, sio unahatari ya kuwa zero humu jf tuu, unaweza kuishia hadi kuwa zero kwenye kila kitu!.

Pasco
 
Naona thread za kuleta machafuko zimeanza sawa Pasco wewe na huyo Tendwa mtaleta machafuko mjaribu tu na hii thread yenu ya kutest upepo.
 
Haya yoote ni yakutengenezwa na maccm ili kuendeleza hujuma ila mwenyezi mungu yu pamoja nasi wao Wana dola sisi tuna mungu watashindwa mchana kweuupeee
 

@Pasco, I am not what you think I am, may be in your prayers!!

Hata unishambulie kwa jina langu kiasi gani, the facts will never change. Wewe kama mwandishi huru ni nini umekuja nacho kwenye jukwaa badala ya points za kukuza Udini, Ukabila na Ukanda. Those have been your key words for the past three days. Hiyo thread ya 2013 uliyoiibua inaonyenyesha ni jinsi gani mawazo yako ni yaleyale tangu juzi, jana, leo huenda na kesho. With your shallow thinking you thought it did not pick that because I am Mr. Zero!! I seriously doubt your intellectual capacity especially as a journalist. May be that's why you decided to work independently because no one could hire you!! Povu limekutoka kwa vile nimesema umekuwa hired Lumumba!! Your anger shows how right I was, although it was a guess!!

As an independent journalist (as you it call yourself), I expected you to come up with independent critical analysis in this matter. Unfortunately, you failed!! You have instead taken the side which you are now defending it tooth and nail!! Please stop calling yourself an independent journalist if you are somebody's sympathizer because that makes you not independent anymore!!

As much as you like Zitto, we all knew this will happen to him. The only thing we did not know was when and how.



Just sleep away and keep on dreaming dude!!

I remain Mr. Zero!!
 
Huyu alikuwa John Tendwa, nitamtafuta Jaji Mutungi kabla ya September Mosi, ili kuusikia msimamo wake, ili itakapofika hiyo September mosi, watu wajue huo unaweza kuwa ndio mwanzo wa mwisho wa kilichokuwa kikijulikana kama Chama Cha ....

Pasco
 
Huyu alikuwa John Tendwa, nitamtafuta Jaji Mutungi kabla ya September Mosi, ili kuusikia msimamo wake, ili itakapofika hiyo September mosi, watu wajue huo ndio mwanzo wa mwisho wa kilichokuwa kikijulikana kama Chama Cha ....

Pasco
Ramli zako zinaendelea,sawa endelea!
 
Ramli zako zinaendelea,sawa endelea!
Mkuu Bomihi, Watanzania ni wavivu kusoma, kwa sababu tunapenda mambo rahisi rahisi, hoja nyepesi nyepesi, na maswali rahisi rahisi, bandiko likiwa refu hawawezi kusoma kilichoandikwa ndani, huishia kusoma headlinetuu, amemaliza, na kukoment!.

Essence ya bandiko hili ni Msajili ana mamlaka ya kukifuta chama chochote akiwa na sababu, lakini hawezi kukifuta CCM hata kifanye nini!. Thank God, JK alikuwa ni mtu mpole akavivumilia sana baadhi ya vyama vinavyohatarisha amani na utulivu wa taifa hili, huyu aliyepo ni namba nyingine, mamlaka ya kisheria, yaliyopo kwa msajili ambayo hayajatumika, yakianza kutumika ipasavyo, tusije kupiga kelele humu kuwa tunaonewa!.

Pasco
 
@Pasco,1st sept imepangwa kama siku ya kufanya mikutano nchi nzima!Mikutano ambayo imepewa nguvu na katiba lakini pia na sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu!Lengo la mikutano hiyo limewekwa wazi na hilo wanalipigia kelele kila siku!
Hakuna sehemu yeyote inayohamasisha vurugu,sijamsikia kiongozi yeyote akisema watu wapigane au wavamie maeneo ya watu!Isitoshe hili halijawahi kuwa lengo la upinzani hasa CDM!
Sasa hizi Ramli za kusema kitafutiwa usajili ikibainika hivi au vile zinatoka wapi?Hakuna hata element inayoonesha hayo,haki haiombwi bali hudaiwa!
"Angalizo,kama nchi hii wanataka kuona inafika kubaya basi msajili afanye hilo unalopigia ramli litokee"
 
Mkuu Bomi, katiba yetu imetoa haki kwa mkono mmoja na kuziondoa haki hizo kwa mkono mwingine!. Haki ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, na sheria ya vyama vya siasa vinaitambua haki hii, sheria ikiishatungwa, hutungiwa kanuni na taratibu za utekelezaji, kwenye kanuni, ili mikutano na maandamano hayo yawe halali kwa mujibu wa sheria, lazima yapate kibali cha OCD wa eneo husika, maadam Amiri Jeshi Mkuu ameishasema hataki maandamano wala mikutano, hivyo hakuna OCD atakayetoa kibali cha mkutano wala cha maandamano!. Kitendo cha Chadema kushikilia msimamo wa mikutano na maandamano kwa kibali au bila kibali, ndio kitisho chenyewe cha amani hiki, yaani Chadema wanataka kupimana ubavu na Magufuli!.

Msajili wa vyama ana uwezo wa kukifuta chama chochote isipokuwa chama tawala, thread hii ni angalizo tuu Chadema, ikishindana na mwenye nguvu, itaumia!. CCM hata wafanye nini, hawafanywi kitu lakini Chadema au CUF, cha moto watakipata.

Pasco
 
Ni kweli Haki zilizotolewa kikatiba zimetungiwa kanuni,lakini katiba yenyewe inasema sheria yeyote haitakiwi kukinzana na primary objective yake,yaani yenyewe ni sheria mama!Ndio maana juzi umesikia mahakama imemng'oa meno DPP kwa kuondoa kifungu kinachopingana na katiba!
Pasco katiba hiyo hiyo ndio imemweka Rais madarakani,na ndio hiyo hiyo imetambua vikosi vya ulinzi na usalama!Ni sawa wao kuisigina katiba kwa kutumia sheria vibaya lakini si sawa kwa vyama vya siasa Kutumia haki waliyopokwa!
Tuvute subira,tuone hiyo tarehe moja kitatokea nini!Mwenye mpini ni serikali nakubali lakini siku zote dhulma haijawahi kuishinda haki,wanaweza fanya wakaona wameshinda kwa muda tu ila kumbe ndio wamejiwekea bomu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…