Chama cha Walimu wajifunze kutoka TLS

Chama cha Walimu wajifunze kutoka TLS

Uchaguzi wa Chama cha Walimu huwa ni Aibu tupu, hebu wajifunze kutoka TLS. HONGERA TLS
Hongera Mwabukusi
Walimu wa nchi hii hawana misimamo, CWT ni ccm wing, they have no idea why wapo hapo , they have no idea kama wanapigania haki za walimu au chama tawala

Ndio maana heshima yao kwenye jamii imeporomoka sana
 
Waalimu waoga sana,kuna mradi tulikuwa tunafanya na Waalimu,daah wananidhamu ya uoga sana,sijui kwanini
 
Ni rahisi na ngumu pia. Ila wale jamaa wanaotuletea saccos kwenye TLS ndio wanataka tujekuwa kama ndugu zetu walimu.

CWT wapo hivyo walivyo moja ya sababu ikiwa ni kubadili malengo ya msingi kwa kuweka malengo ya kiuchumi.

Watu hawajui kuwa uchumi wa mtu binafsi haujengwi na hivi vyama na kuipenyeza hiyo ajenda ni kujimaliza wenyewe.
 
Hawa ni wanasheria na wasomi kwa jina lao wanajitambua sana tofauti na walimu.
 
Mnataka tu kuwaonea walimu, kuitaka CWT ijifunze kwa TLS ni kutaka toroli liige kwa V8.Haiwezekani
 
Kitendo cha kuchanganya walimu wa shule ya msingi na secondary CWT basi kila kitu kilishaharibika.Walimu wa shule ya msingi huwambii chochote kuhusu CWT
 
Uchaguzi wa Chama cha Walimu huwa ni Aibu tupu, hebu wajifunze kutoka TLS. HONGERA TLS
Hongera Mwabukusi

Sasa wale makada wa chama cha kijani watafanyaje mambo tofauti na "magodifaza" wao...
 
Back
Top Bottom