Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akiwemo Ndugai nitaunga mkono fasta. Tunataka chama kitakachoisemea Tanganyika. Sioni mwingine zaidi ya Ndugai.Mbona anatajwa mmoja tuu Maalim seif? Yuko peke yake huyo mwanzilishi wa chama?
Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Kama siasa zikiwa za kistarabu,zisizo za kibabe,fujo na matusi hakuna sababu yeyote kwa nini serikali ya Chama tawala isi relax masharti.Tatizo ni vyama vya upinzani kutokuwa na adabu na kushirikiana na mabeberu kui-sabotage nchi.Nchi hii ni yetu sote,Ni lazima tushirikiane kuijenga,sio kuibomoa.Hujaelewa .
Kwa Hali ilivyo Sasa, vyama haviruhusiwi hata kufanya mikutano ili kujieneza
Na wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa CCM ambao Rais anawaambia wasitangaze mpinzani
Sasa umoja party hata Kama Wana support mazingira yamehodhiwa na Chama tawala
Mnavizia ruzuku tu nyie...Udikteta na ukabila uliuona wewe,sisi wengine hatukuuona.Subiri wananchi wataamua kwenye box la kura 2025.
Mwendazake alikuwa kiongozi muovu. Period.Magufuli anakuja kwa kuwa aliiifanyia nchi yetu mema.Yeye ni symbol ya mema,we cherish what he did,not him.
Endelea kuota wakati kumeshakucha.Ruzuku?
Kama ruzuku ikija itatumika kwa kupanga mikakati ya kuingia madarakani ili kuwaletea Watanzania maendeleo yao,that is all,sio kuganga njaa.
Muovu ulikuwa wewe,ndio maana uli-face his wrath.Kama ni mwizi wa mali ya uma,mkwepa kodi,uli-forge cheti,CIA covert operator na ulikuwa una-sabotage nchi in any way,kwa nini asikushuhulikie.He was right.Mwendazake alikuwa kiongozi muovu. Period.
Hivi kuua ni falsafa eenheChama chochote kinachounga mkono falisafa za JPM, nitakuwa mwanachama wake
Unaua alafu unajisifu falsafa ya magufuliIla hili suala la kuteka na kuua mbona lipo kwenye hii nchi toka enzi za mwalimu, na lipo duniani kote.
Dr Ulimboka ilikua lini anatekwa na kung'olewa kucha kisha kutelekezwa msituni?
Mauaji ya Imran Kombe ilikua lini, na nikizama kutafuta matukio yanayoshabihiana na haya ni mengi..
Jpm alikamata simu za January akimteta, je alimteka, alimuua?
Tatizo hamtaki wanyonge wapewe haki zao. Kwenye suala la huduma za kijamii wanyonge walionewa sana, wafanyakazi wengi waliwaheshimu wananchi wa chini ya JPM.
Mpigaji yeyote yule point yake ni utekaji na uuaji kama ndilo jambo pekee walioliona kwenye uongozi wa JPM, mkiacha mazuri yote na mkaona alichofanya for 5 years ni utekaji na uuaji.
Mh hapo tu kweny falsafa bora kifutwe mazima, mamb ya kutekana, tesa, ua, filisi. NooooUTANGULIZI
TAFADHALI NAOMBA NISIRUSHIWE MADONGO,MIMI NI MJUMBE TU.HATA HIVYO NIKIRI KWAMBA HILI WAZO NIMELIPENDA, INGAWA MIMI NI MWANA CCM.
NIKIRI KWAMBA BAADA YA MIAKA 61 YA UHURU, BADO CCM INATUPIGISHA WATANZANIA MAKIDA MAKIDA.
KWA BAHATI NZURI MAGUFULI ALIBADILI SYSTEM YA UONGOZI TANZANIA, NA KULETA SYSTEM INAYOJALI MAENDELEO YA WATANZANIA.UNFORTUNSTELY WE ARE BACK TO SQUARE ONE.UMOJA PARTY IS MEANT TO REVERSE THIS TREND.
Chama kipya cha kisiasa kimeanzishwa nchini Tanzania, kikiwa na lengo la kuendeleza sera na mtindo wa uongozi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.
Waanzilishi wa Umoja party wanaripotiwa kuwa wanachama na watu maarufu ndani ya chama kinachotawala cha CCM, ambao hawana furaha na uongozi wa sasa kwa kuwa wanaona hauna tija kwa Watanzania walio wengi .
Mwanzilishi wa chama hicho Seif Maalim Seif, ameambia sauti ya Amerika VOA kwamba “Tuliwasilisha maombi ya usajili mwaka jana na tumefikia hatua ya marekebisho kadha wa kadha. Katika Ofisi ya msajili wa vyama kuna katiba na kanuni za chama chetu na vielezo vyote vinavyotakiwa.”
Baadhi ya vigogo wa CCM wanaunda Umoja party?
Kuna ripoti kwamba huenda watu maarufu na wa ngazi ya juu katika chama kinachotawala, ambao wangependelea Tanzania iongozwe namna alivyokuwa anaongoza aliyekuwa rais wa nchi hiyo hayatoi John Pombe Magufuli, ndio wanaosukuma kuundwa kwa chama cha umoja.
“Chama chetu kilifikia hatua ya kuwekwa kwenye gazeti la serikali mwezi Novemba mwaka jana kwa mda wa siku 21 kwa yeyote aliye na pingamizi. Kwa hivyo hiki chama sio kwamba watu wamejikusanya na kuamua kufanya hivi na hivi. Tunachosubiri ni maelekezo ya msajili wa vyama kwa ajili ya kupewa cheti cha usajili.” Amesema Maalim Seif.
Picha za watu ambao wamevalia fulana za chama cha umoja, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Fulana hizo zina picha ya aliyekuwa rais wa Tanzania John Magufuli.
“sisi wa upande wetu hatuna deni lolote la mahitaji ya kisheria ya kutaka kusajiliwa. Ni Afisi tu ya msajili wa vyama kutuambia kiachofuata. Tulishamaliza mwaka mmoja sasa.” Ameongezea Seif Maalim Seif.
Malengo ya umoja party
Misingi ya chama hicho ni kuendeleza falsafa ya aliyekuwa rais John Mgufuli. Waanzilishi wake wanasema kwamba Tanzania sasa ipo katika hali ya sintofahamu, miongoni mwa vyama vya kisiasa huku hali ya maisha kwa watanzania ikiendelea kuwa ngumu, na kwamba ipo haja ya kufuata nyayo za Magufuli kuongoza taifa hilo.
Hata hivyo, Seif Maalim amesita kusema iwapo chama cha mapinduzi kina mapungufu kwa sasa kuendeleza falsafa ya Magufuli akisema kwamba “nadhani falsafa yake, kama chama cha mapinduzi kinaitumia au la, ni jukumu la wananchi wenyewe kuamua.”
Wanachama wengine wa Umoja party hata hivyo bado ni siri ya wenye chama.
“Jamii inaona ukweli ni akina nani wana dhati ya kumuenzi rais Magufuli. Wale ambao wapo tayari kupoteza nyadfa zao, na wale wanaoona kwamba falsafa ya Magufuli haitekelezwi. Siwezi kuwataja majina lakini dhamira zao zinajulikana.” Amesema Maalim Seif, akiongezea kwamba “wimbi la kisiasa ni la kawaida” akiwa anajibu swali iwapo kuundwa kwa umoja Party kutavuruga chama cha CCM ambacho alikipenda John Magufuli.
Mvutano ndani ya chama cha CCM
Mnamo mwezi Januari, mjadala mkali ulitokea Tanzania kuhusu deni la nchi hiyo linaloendelea kuongezeka, baadhi ya viongozi katika chama kinachotawala cha CCM wakisikika hadharani wakimkosoa rais Samia Suluhu Hassan kwa kile walisema ni “kuendelea kukopa kiholela” ili kufadhili miradi ya serikali.
Mjadala huo ulipelekea spika wa buge la taifa Job Ndugai kujiuzulu.
Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa CCM walikosoa uongozi wa rais Samia, ambaye baadaye alifanya mabadiliko serikali na kuwatimua baadhi ya viongozi, siku chache baada ya kusema hadharani kwamba angewatimua wale ambao wanataka kufanya siasa badala ya kutumikia wananchi kuleta maendeleo.
Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC
Labda nikuulize swali.Hivi kama wewe ungekuwa Rais,halafu unahangaika kuwaletea wananchi wako maendeleo.Then watu fulani kwa ujinga tu na uchumia tumbo from nowhere,wanashirikiana na mabeberu ku-sabotage maendeleo ya taifa,wewe kama Rais ungewafanyaje?And you have all the evidence.Naomba unijibu tafadhali.Mh hapo tu kweny falsafa bora kifutwe mazima, mamb ya kutekana, tesa, ua, filisi. Noooo
Usishangae sana, ndio akili za Wanasiasa wa Kibongo..Yaani wanawaza wataingia Ikulu wakati huyo wanayetaka kumtoa madarakani ndio huyo huyo anayesajili hivyo vyama ..How ironic!Unashangilia chama kipya badala ya kupiga Kelele Katiba Mpya ipatikane.
Aliyekuloga kafa.
Kwa hiyo unatuambia kwamba Tanzania hakuna haki?Ndio maana Umoja Party inataka kuingia Ikulu ili irejeshe haki.Usishangae sana, ndio akili za Wanasiasa wa Kibongo..Yaani wanawaza wataingia Ikulu wakati huyo wanayetaka kumtoa madarakani ndio huyo huyo anayesajili hivyo vyama ..How ironic!
Naomba vuta subira kidogo. Kaa hapo hapo usiondoke, narudi na jibu.Kwa hiyo unatuambia kwamba Tanzania hakuna haki?
Udikteta na ukabila uliuona wewe,sisi wengine hatukuuona.Subiri wananchi wataamua kwenye box la kura 2025.
Umoja party ni tawi halisi la ccm, ni chama kilichoko kimkakati kuipa backup çccm ikizidiwa kwenye uchaguzi.Si ajabu ccm imetengeneza tawi, kwa kua wameona mama hafanyi kile ambacho magu alikua anakifanya na kunaweza kupelekea kukosa kura kwa waliokua upande wa magu.
Kwahiyo wameona ni bora waunde copy yao ili kuvuruga na kuzipiga bao idea za vyama vingine kumtumia magu ili kujizolea kura kwa wachache waliomkubali.
Bado sina imani na Umoja party.
Nikweli majizi na waliofoji vyeti ndio waliouona huo udikteta na ukabila.Udikteta na ukabila uliuona wewe,sisi wengine hatukuuona.Subiri wananchi wataamua kwenye box la kura 2025.