LGE2024 Chamwino, Dodoma: Rais Samia apiga kura katika Kitongoji cha Sokoine. Asisitiza amani na majibu kutoka kwenye masanduku

LGE2024 Chamwino, Dodoma: Rais Samia apiga kura katika Kitongoji cha Sokoine. Asisitiza amani na majibu kutoka kwenye masanduku

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye foleni tayari kwa kupiga Kura katika Uchaguzi wa Seikali za Mitaa katika kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino Mkoani Dodoma, leo tarehe 27 Novemba, 2024.

Screenshot_20241127-121408.jpg

Screenshot_20241127-121426.jpg
===

Samia amepiga Kura katika Uchaguzi wa Seikali za Mitaa katika kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino Mkoani Dodoma, leo tarehe 27 Novemba, 2024.

Ametoa rai wa Wananchi wote waliojiandisha na wenye sifa watoke na kupiga kura. Amesema kura hizi ni mtindo wetu wa kidemokrasi na kisiasa, ufanyike kwa usalama na amani bila kuvunja amani na kupiga kura kuwe kwa maelewano.

Amesisitiza “Masanduku yanavyosema ndio hivyo matokeo yatoke”

Aidha, amesema matumaini yake ni kuwa siku hii itaisha vizuri na hadi sasa siku inakwenda vizuri akiamini Wananchi watachagua watu wenye uwezo wa kuwaongoza vizuri
 
Kwa maelezo ya msemaji wa serikali ya Zanzibar (sms) wazanzibari hawahusiki kwenye huu uchaguzi hili limekaeje?
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassana Amesisitiza Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Kuwa Wa Haki Na Kuchagua Viongozi Wenye Ufanisha Na Kuwaunganisha Wananchi.

Rais Dkt. Samia Ameyasema Hayo Wakati Akishiriki Zoezi La Kupiga Kura Katika Kijiji Cha Chamwino Jijini Dodoma

Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Mwaka 2024 Unahusisha Vijiji 12,280 Mitaa 4,264 Pamoja Na Vitongoji 63,886.
 
Hapa napita kimya kimya
Ntarudi badae kusoma comment za wadau
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassana Amesisitiza Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Kuwa Wa Haki Na Kuchagua Viongozi Wenye Ufanisha Na Kuwaunganisha Wananchi.

Rais Dkt. Samia Ameyasema Hayo Wakati Akishiriki Zoezi La Kupiga Kura Katika Kijiji Cha Chamwino Jijini Dodoma

Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Mwaka 2024 Unahusisha Vijiji 12,280 Mitaa 4,264 Pamoja Na Vitongoji 63,886.
View attachment 3163105
Kiongozi madhubuti wa mfano Barani Africa.

Thank you Dr. Samia Suluhu Hassan 🌹
 
Back
Top Bottom