Vijana angalau sasa watakuwa na Morali ya kimchezo, nadhani Zambia wahesabu siku za kuondoka. Sijui mechi za siku hiyo zitachezwaje, zinatakiwa zichezwe muda sawa ili kuondoa kukatisha tamaa wachezaji, manake mpaka sasa Zambia na Senegal wameshinda mechi moja na kudroo moja, wakati waTZ tumefungwa moja na kushinda moja. Hivyo nafasi yetu bado ngumu, manake Ivory Coast wao ni wa mwisho, naona mchezo waona Senegal wanaweza wawe wamekata tamaa.
Ila kwakuwa wana upinzani na Senegal, uko uwezekano Senagal wakawafunga ili kuwatoa kabisa. Nasi tukishinda kwa Zambia hapo tutasonga, ila tukitoa droo ama kufungwa tumekwisha.