CHAN Finals: Live from Ivory Coast

CHAN Finals: Live from Ivory Coast

Angalau leo ni raha kamili.
Kipenga hicho pee...
Tumeshinda!.
Mungu ameibariki Tanzania.
Amen.
 
upumbavu huu........... ndo maana hatutaweza cheza ulaya namna hiiiiiii. refa mpuuzi
 
Ahsanteni wadau wote kwa kutupa hizo habari nzuri ambazo zitaendana na uzinginzi mnono, ahsante taifa stars na benchi la ufundi ila kazi bado ipo tukaze buti!
 
Dah,

Walau nimefurahiiii. Hata wife naona hakulala mpaka aone final results. Full uzalendo

Kweli huo ni uzalendo Mkuu Max, nasi sasa tunafuraha angalau tunanyoa watu, hatu kichwa cha mwendawazimu tena. Hongera vijana wetu na kocha pia.
 
Mpira umekwisha lkn duuh tumecheza chini ya kiwango haswa dk.za mwisho... Cha muhimu ni kujiandaa kwa Team ya Zambia...
 
Huyu Refa ni mpuuzi sana inapaswa Stars walalamike ni hujuma tosha huwezi chezesha mpira Dk 99.
 
Hongera stars. Sasa gemu lifuatalo ni dhidi ya Zambia. Kazi ipo.
 
Sio refa wadau hata huduma ya tv yao wametunyima wadau, lakino tumewangoa
 
Mpira umekwisha lkn duuh tumecheza chini ya kiwango haswa dk.za mwisho... Cha muhimu ni kujiandaa kwa Team ya Zambia...


Hiyo ni kawaida.
Mara nyingi timu inayoongoza dakika za mwisho huwa inashambuliwa zaidi,maana wapinzani wanakuja kasi kusawazisha na washindi wanajitahidi kulinda gori.
 
saafi sana,Tumshukuru Mungu. Ila Refa amekuaje kazidisha muda hivyo? Alikua anafidia time au ni vipi sasa
 
sare ya zambia na senegal ni ahueni, now we stan almost equal chances....... twahitaji ushindi dhidi ya zambia
 
Wana JF na Watanzania wenzangu,

Nawapeni hongera kwa ushindi wa timu yetu leo. Nimeshindwa kuendelea kuangalia mpira wa UEFA nikabaki kwenye JF kuangalia matokeo. Bahati mbaya hapa nilipo sikuweza kuifutatilia mechi live.

Tuwatie moyo wachezaji wetu wafanye vizuri zaidi. Hongera wachezaji, Hongera team ya ufundi.

Leo nitapata usingizi mzuri.

Cheers na usiku mwema

Tiba
 
Vijana angalau sasa watakuwa na Morali ya kimchezo, nadhani Zambia wahesabu siku za kuondoka. Sijui mechi za siku hiyo zitachezwaje, zinatakiwa zichezwe muda sawa ili kuondoa kukatisha tamaa wachezaji, manake mpaka sasa Zambia na Senegal wameshinda mechi moja na kudroo moja, wakati waTZ tumefungwa moja na kushinda moja. Hivyo nafasi yetu bado ngumu, manake Ivory Coast wao ni wa mwisho, naona mchezo waona Senegal wanaweza wawe wamekata tamaa.

Ila kwakuwa wana upinzani na Senegal, uko uwezekano Senagal wakawafunga ili kuwatoa kabisa. Nasi tukishinda kwa Zambia hapo tutasonga, ila tukitoa droo ama kufungwa tumekwisha.
 
Watu wanadai hata Drogba angekuwepo leo angefanywa mwali na carnavaro....
 
Nawatakia heri, viongozi wa TFF na wachezaji wote wa timu ya Taifa mwaka 2009 uwe wa mafanikio.

Nawatakia heri, viongozi wa FAT na wachezaji wote wa timu ya Taifa mwaka 72 uwe wa mafanikio. Kibaden oyeee oyeee kwa uchezaji bora kitwana oyeoyee. Wachezaji wote wa enzi hizo walitajwa katika wimbo huu. Nadhani baadhi yenu mtaukumbuka huu wimbo ulikuwa maarufu sana mwaka 72. Kuna haja ya kutunga mwingine kwa wachezaji wa sasa
 
klhnsiren.gif

KLHN News Alert:

Hatimaye refarii aliweza kukipata kipenga chake na kupuliza kwa uvivu kuashiria mpambano wa timu ya Taifa ya Tanzania na ile ya Ivory Coast ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani kufikia tamati.

kwa ushindi huo wa Taifa Stars inaonekan kibarua cha kocha wa timu ya Taifa ya Ivory Coast kinaelekea kuota nyasi baada ya timu kamambe ya Taifa Stars ya Tanzania kuibanjua timu yake bao moja bila katika michuano ya kwanza ya timu za Taifa za wachezaji wa ndani (CHAN) inayofanyika huko Ivory Coast. Bao hilo la Tanzania lilifungwa kwa gonga moja ya kichwa ya mshambuliaji machachari Mrisho Ngassa. Timu ya Tanzania ikicheza kwa kujiamini chini ya kocha wake Mbrazili Maximo iliweza vyema kulinda bao hilo liliopatikana dakika ya 38 ya mchezo huo. Kwa ushindi huo timu hiyo ya Tanzania imejiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mashindano hayo.

Mechi hiyo ambayo dakika za mwisho zilitafsiriwa na mashabiki wa Tanzania kama jitihada za refarii kuibeba Ivory Coast ilikuwa ni ya kusisimua na yenye mvuto wa aina pekee ambapo timu hiyo changa ya Tanzania imezidi kujijengea jina katika eneo la Afrika ya Magharibi na bila ya shaka katika chati za kandanda duniani.
 
Last edited:
Nawatakia heri, viongozi wa TFF na wachezaji wote wa timu ya Taifa mwaka 2009 uwe wa mafanikio.

Nawatakia heri, viongozi wa FAT na wachezaji wote wa timu ya Taifa mwaka 72 uwe wa mafanikio. Kibaden oyeee oyeee kwa uchezaji bora kitwana oyeoyee. Wachezaji wote wa enzi hizo walitajwa katika wimbo huu. Nadhani baadhi yenu mtaukumbuka huu wimbo ulikuwa maarufu sana mwaka 72. Kuna haja ya kutunga mwingine kwa wachezaji wa sasa

Bubu kama unao tutumie link yake tujipongeze. Siujui huo, manake enzi hizo Mfumwa alikuwa hayuko.
 
Back
Top Bottom