CHAN Finals: Live from Ivory Coast

CHAN Finals: Live from Ivory Coast

Ukweli ni kwamba hatuma Washambuliaji ,ndio maana magoli yetu mengi yanafungwa na viungo halafu pia karibu wachezaji wetu wote ni wafupi na wana miili midogo

Hilo la umbo la wachezaji niliwahi kuligusia kuwa kwa miili hii yenye umbo la vibaka ,tutashinda lakini si kwa kuchukua kombe, na hao washambuliaji tulio nao hata pakiondolewa kipa basi kufunga itakuwa mbinde. Wana vigugumizi vya miguu.
 
Hilo la umbo la wachezaji niliwahi kuligusia kuwa kwa miili hii yenye umbo la vibaka ,tutashinda lakini si kwa kuchukua kombe, na hao washambuliaji tulio nao hata pakiondolewa kipa basi kufunga itakuwa mbinde. Wana vigugumizi vya miguu.

Mkuu nakuunga mkono hii ishu...
Tunahitaji wafungaji mpaka sasa hatuna wafungaji katika timu ya taifa.
 
michezo hii ni yetu watu wa ukanda huu wa Afrika kwa sababu hakuna timu ya taifa katika ukanda huu wa afrika inakuwa na wachezaji wa kulipwa wanaofikia angalau nusu ya timu. lakini timu za taifa kwa nchi za afrika magharibu ni karibu timu nzima ya wakulipwa, sasa sisi ambao timu zetu za taifa ndio hizi hizi za CHAN tulipaswa kutawala mashindano. angalia wenzetu tunaopakana nao, Zambia na jirani zao Zimbabwe, angalia jirani zetu DR Kongo zote zimeonesha uhai. sasa sisi tatizo ni nini? Maximo aseme kama kazi imemshinda. mimi nilitarajia timu zote za ukanda huu kufuzu maana ndio haswa wenye mashindano haya.
Bora Maximo aachie ngazi hukohuko kama atashindwa kufika nusu fainali.
 
nafikiri kuna umuhimu wa kujaribu kocha mwingine, huyu jamaa amefanya vya kutosha, uwezo wake ndo umeishia hapo, hivyo anatakiwa kulala mbele. sisi tutafute kocha mwingine, kwanini tumng'ang'anie, kwani yeye ni mtz, tulete makocha wengine toka ulaya, na kama hawapo, hata hawahawa wa kwetu bongo wanaweza fanya maajabu. nimechoka kufungwa, nimeshika moyo kuuma hadi mechi inaisha nilifikiri watarudisha,wapi. hiyo ndo vijana wahuni mnasema "duuuu".
 
Wakuu ivi mech ya leo inaanza saa ngapi????,kama vp tujuzane kadiri mchezo unavyoendelea maana wengine twategemea hapa jamvini kupata mwenendo mzima wa hiyo mechi...Kila la kheri stars....be blessed
 
Kocha siyo anayecheza mpira, kuna waalimu wazuri sana wa hesabu lakini angalia mitihani ya form 4, na mpira ndivyo hivyo.

Kaseja hana sifa ya kuchezea timu ya taifa kutokana na kimwili chake, Yanga kwenyewe anasugua bench kwa mechi muhimu.

watu tunasahau alipokuwa anaitwa tanzania one, kila tukionekana hadharani kapu la magori.....
 
Wakuu nijulisheni mechi inaanza saa ngapi kwa saa za kwetu?, leo nataka nishuhudie mwenyewe tunavyowamaliza wenyeji.
 
Jamani someni hii habari, haya kweli yatakuja kutokea timu yetu isipozidi fanya vizuri.

Maximo adaiwa hana uwezo zaidi ya hatua aliyoifikisha Taifa Stars
Na Mwandishi Wetu
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Hussein Sappi amesema tukubali ukomo wa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na staili ya soka anayofundisha timu haiwezi kufika mbali.

Akizungumza katika kipindi cha Kumepambuzuka cha Radio One jana, Sapi alisema makocha wa Brazil wengi hawana rekodi katika ulimwengu wa soka zaidi ya nchi yao.

Alisema Brazil wazuri kwa wao wenyewe lakini hawana rekodi nzuri duniani.
“Mimi nadhani wakati umefika sasa tubadilike, tuangalie Ulaya Mashariki, kule tunaweza kupata makocha wazuri na hata soka yao inajulikana.

“Tunakubali kuwa Brazil wana makocha wazuri lakini kwa faida yao, wapi kuna mafanikio kwa kocha wa Brazil? Tunaona Afrika Kusini inavyoyumba
.


“Kulikuwa na Felipe Scolari, alikuwa Ureno, hakuna kitu, kaondoka akaenda Afrika Kusini, akatoka akaja Chelsea, na sasa hayupo, kuna nini pale. Angalia makocha wa Hispania, Ufaransa, Uholanzi, Russia, Jamhuri ya Czech wapo na naamini tunawamudu...,” alisema.


Akizungumza huku akionyesha kukerwa, alisema: “Isije kufika wakati tukapigana mawe Uwanja wa Taifa pale, mimi hili nalisema kama Mtanzania mwenye haki ya kuzungumza langu na sidhani kama Maximo anatufaa tena,” alisema.

Source: Mwananchi Read News
 
Wakuu ivi mech ya leo inaanza saa ngapi????,kama vp tujuzane kadiri mchezo unavyoendelea maana wengine twategemea hapa jamvini kupata mwenendo mzima wa hiyo mechi...Kila la kheri stars....be blessed

Mkuu Balantanda, kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi inaanza saa 4 usiku kwa saa za TZ.
 
Mkuu Balantanda, kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi inaanza saa 4 usiku kwa saa za TZ.

Ngoja tusubiri ili tujue kama tutaendelea kuwepo kwenye jiji la Abdjan with matumaini ya kutetea maslahi ya Taifa au ndo tusubiri tu kukamilisha ratiba na Zambia!
 
mpira umeisha Zambia 0 - 0 Senegal. Tungoje sisi na wenyeji saa moja kuanzia sasa sijui nayo wataionesha?. Kila la heri TS
 
Ni taarifa ya habari imeanza hapa TBC (06h00 GMT)Not sure kama wataionyesha!
 
jamani leo tunaomba tena msaada, mtandaoni tuangalie kupitia TV gani?, ile ya siku ile (Senegal RTS 1) sasa kuna jamaa sijui anaongea kilugha. Msaada wakuu.
 
wameanza onesha, ile chanel ya Senegal. Mungu isaidie timu yetu japo nasi tusongembele.
 
Ingia RTS 1, ndio wanaonesha. Nimekosea nikaandika RST 1
 
Back
Top Bottom