Changamoto katika ujenzi: Mafundi uchwara wanavyoharibu kazi

Changamoto katika ujenzi: Mafundi uchwara wanavyoharibu kazi

Anayehitaji nyumba yake kusimamiwa ujenzi nipo hapa jamani sina kazi ila abc za ujenzi ninazo
Je njia gani nzuri y malipo kwa fundi kujenga kwa Day au kwa tofali?
1.Day bei gani?
2.Tofali bei gani?
KAZI ni kipimo cha utu
 
Mkuu, unapoanza ujenzi jitoe hasa kusimamia mwenyewe, usitume mtu kusimamia kwa niaba yako, hata mkeo hapana maana kuna ujanja mwingi sana wa wizi na upotoshaji wa manunuzi.
Ukimuweka msimamizi ,mafundi watamtuma kwenda dukani kununua maji huku wao wakijifanya wapo busy ,ukitoka tu mifuko ya cement inafaulishwa au inafukiwa kwenye mchanga.
 
Kama hujaanza ujenzi hasa wa nyumba yako ya kwanza ya kuishi jitahidi sana upate elimu ya kutosha kwenye
Ununuzi wa ardhi/kiwanja
Mafundi wa kila idara
Makisio ya vifaa, ufundi
Muda sahihi wa kuanza ujenzi
Nini cha kuanza kufanya nknk
Fanya utafiti wa kutosha.. Pata makisio ya ujenzi kwa kila hatua kwa mafundi tofauti
Ukiachana na changamoto za kuongezewa gharama kwenye vifaa na gharama za ufundi ama kuibiwa kwa vifaa vilivyokwisha nunuliwa kuna hili la kuharibiwa kazi
Na kazi iliyoharibiwa ina changamoto kubwa zaidi za kurekebisha kuliko kazi mpya
Kuna mengi sana ya kuambiana hapa lakini machache makubwa ni haya
1. Usifanye malipo ya ardhi/kiwanja bila kujihakikishia umiliki wake, migogoro, mipaka nk
2. Usifanye malipo bila kujihakikishia serikalini ramani ya mipango miji
3. Usianze ujenzi bila kufanya ibada ya kutakasa ardhi.. Ukishindwa hapo basi ibada ya kuitakasa nyumba
4. Usianze ujenzi bila kujihakikishia sehemu salama ya kuweka vifaa vyote vitakavyohusika kwenye ujenzi
5. Usianze ujenzi kwa kufanya mkupuo wa manunuzi.. Anza na vitakavyohitajika kwa wakati huo tu.. Na kama kina baadhi utavipata mapema kwa bei nzuri kaa navyo mwenyewe
6. Piga kenchi ukiwa umejihakikishia uwepo wa mabati
7. Usifanye wiring kama hakuna mtu anayekaa hapo.. Utajuta
8. Usiiache nyumba tupu/peke yake unapoelekea kumaliza ujenzi wa awali
9. Kumbuka gharama za finishing ndio kaburi la pesa😂 hivyo jiandae
10. Jihadhari na majirani...😀🤔🙇🏿‍♂.... Wakati wa ujenzi na utakapohamia.. Kuna jirani anaweza kuwa rafiki wakati wa ujenzi lakini akaja kuwa adui mkubwa utakapohamiaView attachment 3234061
Siku hizi siingii sana JF, kwa sababu ya majukumu. Ila hii nimekutana nayo mida hii imenilipua kicheko, yaani fundi kaweka mtego wa umeme kwenye chanzo cha maji...🤣🤣🤣
 
FB_IMG_1739639014854.jpg
 
Back
Top Bottom