Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona ulijenga mwaka Juzi mkuu,labda kama ni eneo lingineKumbe tupo wengi....kila mwaka nasafishabkiwanja ila kujenga najenga kwenye mbususu za warembo
Ah wapi sijajenga mie...nasaka huyu fundi anasema 25mil anajenga nyumba ya vyumba viwiliMbona ulijenga mwaka Juzi mkuu,labda kama ni eneo lingine
Mkuu nahisi nimedhulumiaa nifanyaje?Kama hujaanza ujenzi hasa wa nyumba yako ya kwanza ya kuishi jitahidi sana upate elimu ya kutosha kwenye
Ununuzi wa ardhi/kiwanja
Mafundi wa kila idara
Makisio ya vifaa, ufundi
Muda sahihi wa kuanza ujenzi
Nini cha kuanza kufanya nknk
Fanya utafiti wa kutosha.. Pata makisio ya ujenzi kwa kila hatua kwa mafundi tofauti
Ukiachana na changamoto za kuongezewa gharama kwenye vifaa na gharama za ufundi ama kuibiwa kwa vifaa vilivyokwisha nunuliwa kuna hili la kuharibiwa kazi
Na kazi iliyoharibiwa ina changamoto kubwa zaidi za kurekebisha kuliko kazi mpya
Kuna mengi sana ya kuambiana hapa lakini machache makubwa ni haya
1. Usifanye malipo ya ardhi/kiwanja bila kujihakikishia umiliki wake, migogoro, mipaka nk
2. Usifanye malipo bila kujihakikishia serikalini ramani ya mipango miji
3. Usianze ujenzi bila kufanya ibada ya kutakasa ardhi.. Ukishindwa hapo basi ibada ya kuitakasa nyumba
4. Usianze ujenzi bila kujihakikishia sehemu salama ya kuweka vifaa vyote vitakavyohusika kwenye ujenzi
5. Usianze ujenzi kwa kufanya mkupuo wa manunuzi.. Anza na vitakavyohitajika kwa wakati huo tu.. Na kama kina baadhi utavipata mapema kwa bei nzuri kaa navyo mwenyewe
6. Piga kenchi ukiwa umejihakikishia uwepo wa mabati
7. Usifanye wiring kama hakuna mtu anayekaa hapo.. Utajuta
8. Usiiache nyumba tupu/peke yake unapoelekea kumaliza ujenzi wa awali
9. Kumbuka gharama za finishing ndio kaburi la pesa😂 hivyo jiandae
10. Jihadhari na majirani...😀🤔🙇🏿♂.... Wakati wa ujenzi na utakapohamia.. Kuna jirani anaweza kuwa rafiki wakati wa ujenzi lakini akaja kuwa adui mkubwa utakapohamiaView attachment 3234061
Hapana hiyo ni hasara,tafuta milioni hata 15 hiyo vyumba viwili inatosha kabisaAh wapi sijajenga mie...nasaka huyu fundi anasema 25mil anajenga nyumba ya vyumba viwili
Asante. Nipe basi huyo fundi wa mil 15Hapana hiyo ni hasara,tafuta milioni hata 15 hiyo vyumba viwili inatosha kabisa
Mtafute shirima ujenzi boraAsante. Nipe basi huyo fundi wa mil 15
Ndio nani huyo na yupo mkoa ganiMtafute shirima ujenzi bora
Dawa ni kwenda mwenyewe kichwa kichwa kuhemea vifaa na usimshirikishe.Ngumu sana kuwakimbia hapo ,lazima akuingize kwenye 18 zake na ale cha juu ,ukienda kununua kwenye duka unaotaka wewe let say ukakuta bei labda elfu 15 atakwambia twende duka la mbele wanauza 14 ,ukienda tu kwenye hilo duka utakuta bei 14 na utanunua kwa kuona kuna unafuu wa buku ,kumbe hapo yeye ana jero lake hapo.
Sasa hapo ukiwa unakata gogo lazima vuzi litoke jasho 🤣🤣🤣🤣Kuna nyumba niliwahi ingia kuna chumba kina choo ila hakuna dirisha, sijui mwenye nyumba ndio aliamua hivyo au mafundi ndio walivuruga kazi.
😂😂Sasa hapo ukiwa unakata gogo lazima vuzi litoke jasho 🤣🤣🤣🤣
Lakini nimiwa na wale jamaa zako wa kilingeni sii wanaweza nilindia nyaya zangu bila kuwepo mtuNdio zao yani wiring ni majanga kama huna mtu mwaminifu wa kukaa hapo
Hilo waweza kulidhibiti, lakini katika ujenzi kuna wizi wa kila aina usipokuwa makini.Hapo ndiyo dawa yao vinginevyo lazima wapige cha juu.