Na mahusiano bila urafiki hayaendi popote, mwanzo wa mahusiano ni urafiki...
Ila vipi kama unakutana na mtu ambaye yupo serious toka siku ya kwanza mnakutana, na yupo single, na wewe upo serious pia upo single...
Je huyu nae unamchukuliaje anapokuja kukutamkia "nakupenda" siku ya kwanza ama ya pili tangu mfahamiane..??
Tafaadhali usibadilishe gender yanguHahaha we jamaa
Haaa kumbe ke,Tafaadhali usibadilishe gender yangu
Mtu anayenifahamu akinitamkia siwezi kushangaa hata kama hatukuwahi kuwa na ukaribu ila kinachonishangaza ni.mtu kumtamkia mtu unampenda humjui ni mrefu au mweusi, mrefu au mbilikimo n.k. huu si wizi wa mchana kweupe huu
ZitokeeeeSasa SI ndo talaka hizo
Afadhali hao wanaotongoza insta huko sijui twitter. Tabu ipo kwa hawa wanaotongoza Jf jamani mimi wananiacha hoi. Ushimen alishawahi kutoa ushauri wa namna ya kupata mchuchu hapa lakini naona watu walipuuzia na kuona anaongea ujinga ila aliongea ukweli mtupu. Ila ukiona mwanaume anatongoza mwanamke ambae hajawahi kumuona huyo ni bazazi tu kwa sababu anaona hana cha kupoteza
Kwa hilo inategemea ntu na ntu. Lakini bado ni afadhali ukafahamiana na mtu kwa jina urafiki kwanza hata kama mioyo yenu inasema vinginevyo kuliko kumtamkia unampenda hata humjui bali umejitengenezea wewe picha yako unayoipenda ukifika mambo sio kama ulivyofikiria unakula kona matokeo yake ni maumivu na chuki zinaletwa mpaka huku majukwaani.Kwa hilo nakubali...
Lakini je ni kweli mtu anakupa nafasi ya kuwa rafiki hasa humu bila ya kujua lengo lako hasa ni nini...??
Humu na id fake majina fake bado watu wanatongozana na hawafahamiani? Dunia haiishi visa hii.
Mapenzi ni nafsi na sio sura.Kutongoza mitandaoni ni changamoto ila inabidi ukubaliane nazo tu.
Ofcourse walioko mitandaoni ndio hao hao walioko mtaani ila changamoto zake ni kubwa. Juzi nimeona mdau mmoja akilalamika kule twitter kua amepoteza nauli yake mara nne kila akienda mwanamke yuko tofauti na picha zake, kwa sisi wazoefu tunacheka tu kidogo na kutabasamu tunajua kabisa huyu bado mchanga kwenye haya mambo ya online dating.
Kukuta picha tofauti na mtu alivyo ni jambo la kawaida kabisa hata kama sio mwanamke unaeenda kukutana nae. Ila shida inapokuja kua picha aliyokutumia au aliyoweka mtandaoni sio ya kwake kabisa na wala sie yeye, hiyo ni habari nyingine.
Siku hizi wanawake wengi hawaweki picha ambazo sio zao, wachache sana bado wanatumia huo udwanzi wa kizamani. Unajua picha yako mwenyewe inaweza kukuonyesha tofauti kutegemeana na angle ambayo camera man amesimama, mathalani mwanamke mfupi anaweza kupiga picha ange flani ukamuona ni mrefu sana, au anapiga picha kiflat screen chake angle flani ukazani mtu anavuta tela, muone live unaweza kulia.
Siku hizi wanawake wa mutandaoni wanatafta proffessional cameraman wanawapiga picha angle za kitaalam na after photo effects basi mtu anaonekana mtu mwingine kabisa, akikutumia picha mtoto anawaka, makalio sio makalio, kutana nae sasa, unaishia kulia kwa kupoteza muda wako na pesa zako.
Unaweza kushare ni changamoto gani unakutana nazo mitandaoni.
Hii mada inaendelea.
Kwa hilo inategemea ntu na ntu. Lakini bado ni afadhali ukafahamiana na mtu kwa jina urafiki kwanza hata kama mioyo yenu inasema vinginevyo kuliko kumtamkia unampenda hata humjui bali umejitengenezea wewe picha yako unayoipenda ukifika mambo sio kama ulivyofikiria unakula kona matokeo yake ni maumivu na chuki zinaketwa mpaka huku majukwaani.
Haaaaa mkuu we uko vzr,,Well mwaka juzi nilisajili line ya mtandao fulani, sasa nafikiri ni namba iliyokuwa inatumiwa na mtu kabla yangu then ikarudishwa kwenye system. Kuna siku mwanaume akapiga akimuulizia mwenye alikuwa na hiyo namba kabla yangu. Nikamwambia mie ndio mwenye namba na simtambui mtu huyo. Alisisitiza sana kuwa namba anayo kaisave kwa simu yake ila ni kitambo kidogo hajawasiliana nae.
Nilimwelewesha baadae akanielewa na ukawa mwanzo wa mawasiliano. Tukafahamiana majina na mambo mengine, to cut the long stor short baadae tukapanga kuonana. Kwenye picha alionekana mrefu na mwili wa wastani ukijumlisha na bonge la sauti ya kiume nikasema YES.
Sasa siku ya kuonana nae sikuamini nikahisi ni mtu mwingine kaja, jamaa ni kafupiiii, kanenee, kitambi kama gunia. Nilijikaza sikuonyesha kushtuka sana. Alifurahi kweli, tukapiga story,tukala na kunywa then tukaagana kuwa tungeonana siku inayofuata. Mungu anisamehe nilizima simu na sikuitumia tena ile line.
Kwa mtu unayemfahamu huna haja ya kuanzisha urafiki we nenda tu moja kwa moja kwa sababu mwanamke akishakuzoea kumtongoza baadae tena inakuja kuwa changamoto ila kwa huku mtandaoni hapana jitahidi walau uonane na mtu ndio utoe hisia zako, hata picha basiOk, nimekuelewa... Sema idadi kubwa ya wanawake siku hizi hawataki urafiki kwanza, na kama ukiweka urafiki nae basi kuna uwezekano mkubwa akakuona boya... Hii ni changamoto moja wapo kwetu sisi...
Mfano binafsi wadada wanne mtaani kwa nyakati tofauti nimeweka urafiki nao, tena ule ambao wa kumuonyesha kwamba nina jambo zaidi ya urafiki halihitaji kwake, lakini ninapokuja kumueleza nia yangu hasa, naambulia chenga na uongo mwingi, bahati nzuri huwa naelewa mapema na huwa nachukulia poa...
Sasa inafika wakati mtu unasema bora uende useme tu moja kwa moja nia yako, hata kama ni huku mtandaoni..
Ulimtongozea wapi?Haaaaa mkuu we uko vzr,,
Mi nilitongoza dada binamu bilakujua
Wrong namba ilikuwa nomaa aisee, ilibaki kidogo tu tufanye mavituz, daaah ndo tukaja kujuanaUlimtongozea wapi?
Nimekupata vizuri, mwisho kabisa kuna kupata na kukosa...Kwa mtu unayemfahamu huna haja ya kuanzisha urafiki we nenda tu moja kwa moja kwa sababu mwanamke akishakuzoea kumtongoza baadae tena inakuja kuwa changamoto ila kwa huku mtandaoni hapana jitahidi walau uonane na mtu ndio utoe hisia zako, hata picha basi
Yeah. Ata me huwa nachat nao kama cna mtu wa kuchat nae au kama niko bored.Online huwa natongozaga kama michezo siku nikiboeka najisikia kukosa mtu wakuongea naye basi naamua kuwasumbua ila cha ajabu nliobahatika kukutana nao wanakuwaga real kabisa so sijabahatika kukutana na hao wakufake maana mwenye huwa si fake kabisa