Well mwaka juzi nilisajili line ya mtandao fulani, sasa nafikiri ni namba iliyokuwa inatumiwa na mtu kabla yangu then ikarudishwa kwenye system. Kuna siku mwanaume akapiga akimuulizia mwenye alikuwa na hiyo namba kabla yangu. Nikamwambia mie ndio mwenye namba na simtambui mtu huyo. Alisisitiza sana kuwa namba anayo kaisave kwa simu yake ila ni kitambo kidogo hajawasiliana nae.
Nilimwelewesha baadae akanielewa na ukawa mwanzo wa mawasiliano. Tukafahamiana majina na mambo mengine, to cut the long stor short baadae tukapanga kuonana. Kwenye picha alionekana mrefu na mwili wa wastani ukijumlisha na bonge la sauti ya kiume nikasema YES.
Sasa siku ya kuonana nae sikuamini nikahisi ni mtu mwingine kaja, jamaa ni kafupiiii, kanenee, kitambi kama gunia. Nilijikaza sikuonyesha kushtuka sana. Alifurahi kweli, tukapiga story,tukala na kunywa then tukaagana kuwa tungeonana siku inayofuata. Mungu anisamehe nilizima simu na sikuitumia tena ile line.