Changamoto wanazopitia vijana wetu mpaka wanakuja na kampeni za kataa ndoa

Kwa sababu mwaka au manara kaachana na mke wake na wewe unakataa ndoa unashindwa kuelewa tayari hao jamaa wana vizazi vyao hapa duniani na unakuta mtu anasema kataa ndoa maskini hana hata mtoto mmoja
 
Ni aibu Mwanaume mwenye akili timamu kukataa ndoa kwani ndoa ni ibada, mtu akisema anajipanga kwanza aoe hapo tutaelewa au akisema muda ukifika ataoa hapo sawa lakini wanaokataa ndoa hawana hoja kabisa,
Pinga haki sawa, waarabu wamegoma haki sawa ndio maana ndoa imekuwa ibadan kwao.
 
Hii mada ya kataa ndoa inabidi ijibiwe kwa hoja, hawa vijana wanaoikataa ndoa ukute wana mantiki kubwa sana, inaitaji umakini mkubwa sana kuwaelewa na kuweza kujibu hoja yao ya msingi.

Kwa mimi binafsi nadhani kuna utofauti kubwa kati ya kuoa na kufunga ndoa.

1. Naanza na kuoa.

Wazee wetu wa zamani walikuwa wanaoa siyo kufunga ndoa. Ndiyo maana familia zao ziliweza kuishi kwa amani kubwa sana na kuheshimiana tofauti na sasa. Mwanamke alikuwa ana adabu kubwa na anamtii mme wake. Hakukuwa na tamaa za mali ambazo kwa asilimia kubwa zinavunja familia. Mwanamke alijua anatoka kwao anaenda kuolewa na kuanzisha familia na siyo kuchuma mali.

2. Ndoa
Ni upgrade ya kuoa ikiwa na maana hii ifuatayo.
Tafsiri ya ndoa za kipindi hiki ni kama ajira ama taasisi ya biashara yaani startup ambayo founders wawili kila mmoja ana share ya 50% ya ownership. Ambapo anytime founder yeyote anaweza kuharibu hiyo taasisi iliyoanzishwa na kuondoka na 50% yake. Na hii imetengenezwa kwa ajili ya favour ya mwanamke, power ya mwanamme ni kama haipo kwenye ndoa. Ndoa imeegemea upande mmoja na wanawake wanatumia iyo weakness vibaya sana. Hakuna mwanamme anayeweza vumilia kukaa na mwanamke malaya, mjeuri, mwenye kiburi, asiyemsikivu e.t.c eti kisa kafunga naye ndoa.

Maoni yangu ni kwamba turudi kwenye utaratibu wa zamani yaani tuoe na tuzae ila tusifunge ndoa. Ndoa zimekuwa za kitapeli.
 
Mkuu una akili mingi mno , kuoa na kufunga ndoa ni vitu viwili tofauti , usingetakiwa ukomenti tu huku , ungefungua uzi kabisa mkali.
 
Umeweka hoja nyepesi sana zisizokidhi wala kuakisi kile nilichokiandika.. Ngoja nimalizie mada kwanza nitakurudia
Hizo sio hoja wewe ndio umeweka hoja kwamba vijana hawataki kuoa. Ukaweka na sababu ambazo wewe unahisi ndio zinafanya vijana hawataki kuoa.

Unfortunately Sababu ulizoorodhesha hazikua na mashiko ndio mimi nikaja kuzipinga na kukuonyesha kwamba sio hivyo. Huwezi kujisifu kwamba nyie mlikua mnatembea kilometa 20 halafu useme eti sisi hata 1km tunapanda boda.
Nikuulize

Hizo km 30 mlizokua mnatembea mlizitembea mkiwa mnapenda au kwasababu usafiri ulikua ni shida.? Wazee kama nyie ndio mnaonaga kiteseka kwa watoto ni sifa eti kwakua nyie mlilalia mkeka basi na watoto walalie mkeka. Kila era na mambo yake.

Point nilizonukuu kwako pale juu hazina mashiko kabisa.
 

Asante kumajibu huyo mzee,atambue kila zama na watu wake na maisha yao,huwa na shangaa sana hata wanao amini histori za wazeee wazamani waliokufa na kusahaurika kupitia vitabu vya dini,watu ambao hawajua hata gari wala smartphone zinafafanaje,eti tuishi maisha waloishi wao huo ni upuuzi,natamani hata dini zije mpya zinazoendana na maisha ya sasa.
 
Kwa sababu yesu alipanda punda na mtume ngamia , wachungaji na mashee wapande punda na ngamia?
 
Ni aibu Mwanaume mwenye akili timamu kukataa ndoa kwani ndoa ni ibada, mtu akisema anajipanga kwanza aoe hapo tutaelewa au akisema muda ukifika ataoa hapo sawa lakini wanaokataa ndoa hawana hoja kabisa,
Ndoa ni ibada kwenu. Usilazimishe wote tuamini unachoamini wewe.
 
fugaku nimezisoma hoja za vijana ni nyepesi mno na kwakweli hazina mantiki na kuna vitu hawavielewi

1. Wanakataa ndoa kwa tafsiri ya kuwa na vyeti vya ndoa .. Kwamba wako tayari kuishi na mwanamke lakini sio kufunga naye ndoa[emoji38]
sheria inasema ukiishi pamoja na mwanamke kwa miezi mitatu kisheria hiyo ni ndoa tayari.. Hili hawalijui

2. Hawataki/wanapinga sheria ya kugawana mali nusu kwa nusu . . huu nao ni woga wa kijinga kabisa na kukosa kujiamini.. Hivi unafunga ndoa ili muachane? Kwahiyo ndoa inakufa hata kabla hamjaanza kuishi pamoja kwakuwa badala ya kujenga familia mnawaza kugawana mali mkiachana

3. Kiburi cha wan awake
Ndoa sio kitu cha kukimbilia wengi wanakutana na mabinti huku mijini na kabla hawajafahamiana vema ndoa hii hapa! Ukiingia huko ndani ndio unakutana na mengine mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…