Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo kwenye ushoga sio sababu. kweli hajajibu hoja na mimi naomba kumuuliza kuwa ushoga umeanza mwaka huu?Kataa ndoa [emoji23] hujajibu hoja zao, kichaka unachotumia cha ushoga hakina mashiko, kwa sababu watu hawapingi kuoa, bali wanakataa ndoa! Wapo watu wameoa na hawafungi ndoa [emoji23]
Kataa haki sawa kwnza ndo uje ukubali ndoaNiliona clip moja kule ulaya wanawake wanatembea kwa kuandamana uchi barabarani wakitaka wanaume wawaowe nikajuwa hawa wazungu wamechanganyikiwa,lakini kwa mwendo huu na hizi kampeni za vijana kataa ndoa soon tutashuhudia haya mambo na huku kwetu...
Well said madame. Ukatae ndoa halafu unataka iweje?Nawaona hawa kataa Ndoa na wale wa TikTok wa kujificha kwenye haki sawa kwa wote hawana tofauti
Pinga haki sawa, waarabu wamegoma haki sawa ndio maana ndoa imekuwa ibadan kwao.Ni aibu Mwanaume mwenye akili timamu kukataa ndoa kwani ndoa ni ibada, mtu akisema anajipanga kwanza aoe hapo tutaelewa au akisema muda ukifika ataoa hapo sawa lakini wanaokataa ndoa hawana hoja kabisa,
Hii mada ya kataa ndoa inabidi ijibiwe kwa hoja, hawa vijana wanaoikataa ndoa ukute wana mantiki kubwa sana, inaitaji umakini mkubwa sana kuwaelewa na kuweza kujibu hoja yao ya msingi.Sehemu ya pili
2.MALEZI kwenye makuzi
Kutokana na utandawazi maendeleo ya tech na harakati za maisha siku hizi wazazi hawana muda wa kukaa na vijana wao na kuwapa ABC za maisha ukikuta familia imekaa pamoja basi kama sio wakati wa chakula basi ni kuangalia tv nk
Maisha ya sasa pia hayatoi nafasi kwa vijana kushiriki shughuli za kujijenga kimwili na kiakili, uwajibikaji nk.. Wazazi, watoto wote wako busy kutafuta maisha na muda kidogo unaopatikina basi unaishia kwenye starehe na mambo yasiyojenga uwajibikaji wala ukomavu wa akili, maono na mitazamo
3. Uchumba wa muda mfupi, ndoa katika umri mdogo, ndoa bila kujiandaa
Kampeni kubwa ya kataa ndoa mifano yake inasababishwa pamoja na mengineyo lakini na hayo hapo juu
Ndoa si kitu cha kukimbilia ni jambo la kuleta muunganiko wa kudumu wa kihisia maono na mapenzi.. Hivyo uchaguzi wa mwenza sahihi sio jambo la dharura
Japo kuna mengine yatagundulika mbele ya safari, lakini walau kaa na mtu si chini ya miaka mitatu, ukichukua muda wa kutosha kumchunguza kwenye kila kitu
Hisia zake kwako
Mapenzi yake kwako
Utayari wake kwako
Maono yake
Kiwango chake cha akili, maarifa na ufahamu
Hamu zake
Tamaa zake
Madhaifu yake nknk
Unaenda mbele zaidi kwa kuangalia background yake hasa kupitia familia yake, ndugu zake jamaa na marafiki
Haya mambo yote yanakuhitaji muda wako wa kutosha tuu.. Usiamini kwa asilimia mia yote anayokuambia kuhusu yeye! Mchunguze mood yake ukiwa huna, ukiwa na stress ukiwa unazo ukiwa na furaha nknk
Vijana wengi hukimbilia ndoa katika umri mdogo.. Ndoa katika umri mdogo nyingi huvunjika baada ya muda mfupi
Ndoa inataka maandalizi hasa na kutambua baadhi ya mambo ya msingi
Unaoa binadamu na sio mnyama wa kufuga ama mdoli..
Uchumba ni tofauti kabisa na ndoa
Mtashare sasa chumba kimoja, kitanda kimoja, nyumba moja kila siku.. Mtaonana kila usiku mnataka hamtaki
Passion of love ikiisha mnabaki na hisia zenyu halisi na hapo sasa ndio ndoa inaanza rasmi
Unaanza kuyaona mapungufu ya mwenzako
Unaanza kumchoka
Unaanza kujilaumu nknk.. Wengi hushindiwa hapa na kukimbilia mitandaoni kulaumu na kuomba ushauri kwa wasio wana ndoa ama walioshindwa kwenye ndoa zao
Ndoa ni ya wawili tuu wa tatu ni Mungu wa nne ni shetani.. Ndani ya hiyo cycle wengine wooote hawahusiki kabisa na kama wakihusika wana mipaka yao
Mwisho wa sehemu ya pili.. Nitaendelea sehemu ya tatu
Mkuu una akili mingi mno , kuoa na kufunga ndoa ni vitu viwili tofauti , usingetakiwa ukomenti tu huku , ungefungua uzi kabisa mkali.Hii mada ya kataa ndoa inabidi ijibiwe kwa hoja, hawa vijana wanaoikataa ndoa ukute wana mantiki kubwa sana, inaitaji umakini mkubwa sana kuwaelewa na kuweza kujibu hoja yao ya msingi.
Kwa mimi binafsi nadhani kuna utofauti kubwa kati ya kuoa na kufunga ndoa.
1. Naanza na kuoa.
Wazee wetu wa zamani walikuwa wanaoa siyo kufunga ndoa. Ndiyo maana familia zao ziliweza kuishi kwa amani kubwa sana na kuheshimiana tofauti na sasa. Mwanamke alikuwa ana adabu kubwa na anamtii mme wake. Hakukuwa na tamaa za mali ambazo kwa asilimia kubwa zinavunja familia. Mwanamke alijua anatoka kwao anaenda kuolewa na kuanzisha familia na siyo kuchuma mali.
2. Ndoa
Ni upgrade ya kuoa ikiwa na maana hii ifuatayo.
Tafsiri ya ndoa za kipindi hiki ni kama ajira ama taasisi ya biashara yaani startup ambayo founders wawili kila mmoja ana share ya 50% ya ownership. Ambapo anytime founder yeyote anaweza kuharibu hiyo taasisi iliyoanzishwa na kuondoka na 50% yake. Na hii imetengenezwa kwa ajili ya favour ya mwanamke, power ya mwanamme ni kama haipo kwenye ndoa. Ndoa imeegemea upande mmoja na wanawake wanatumia iyo weakness vibaya sana. Hakuna mwanamme anayeweza vumilia kukaa na mwanamke malaya, mjeuri, mwenye kiburi, asiyemsikivu e.t.c eti kisa kafunga naye ndoa.
Maoni yangu ni kwamba turudi kwenye utaratibu wa zamani yaani tuoe na tuzae ila tusifunge ndoa. Ndoa zimekuwa za kitapeli.
Hizo sio hoja wewe ndio umeweka hoja kwamba vijana hawataki kuoa. Ukaweka na sababu ambazo wewe unahisi ndio zinafanya vijana hawataki kuoa.Umeweka hoja nyepesi sana zisizokidhi wala kuakisi kile nilichokiandika.. Ngoja nimalizie mada kwanza nitakurudia
Ila wazee wa zamani mna mambo nyie...Mentality yenu ipo stagnant kama Policies za French kutawala afrika. Let me break it down for you.
Zamani mlilima hivyo kwakua trekta na plau zilikua chache. Sasa hivi trekta zimejaa tele kwanini tulime kwa jembe la mkono. Teknolojia ya mwaka 10000 BC
Mlitembea hivyo sio kwa kupenda usafiri ulikua shida...kama bodaboda zingekuwepo hata nyie msingetembea umbali huo
Ni uamuzi wa mtu... Organic drink n food zipo. Hata nyie kama Mo energy zingekuwepo mngekunywa. Enzi hizo mlikua mnasafiri kwemda huko ili tu mpate soda.
Tutafanyaje kazi za jasho wakati maisha ya sasa ni tech based kila shughuli zipo ipo computerized. Hata nyie hamkupenda kuzifanya. Sema hamkua na options
Wala hizo sio sababu za kukataa ndoa kabisa. Maisha is about to chabge and adapt. Nyie wazee mnataka tuishi kama tupo karne ya 20.zamani chakula kiliwatosha coz mlikua watu wachache nchini ndo maana kuku wa kienyeji mliweza kusubiri ikae miezi 6. Sasa hivi tuko 60+ unategemea hao kuku watatutosha??? Lazima broiler na GMOs food zihusike.
Acheni kutufosi tuishi maisha yenu nyie wazee hata nyie mliyaishi bila kupenda
Ps. Mimi sipingi ndoa... tena kwa caliber yangu siwezi ishi bila partner so Sikupingi hoja yako ila nakupinga point ulizoweka kutetea hoja yako.
#Ndoa muhimu #Kubali ndoa
kaka mshana naona unatumia nguvu kubwa sana kwenye hili suala, mtu kama hataki kuoa unamuacha, kasi waliyokuja nayo ndio kasi watakayoondoka nayo, maji yapatayo moto haraka hupoa haraka
Kwa sababu yesu alipanda punda na mtume ngamia , wachungaji na mashee wapande punda na ngamia?Hizo sio hoja wewe ndio umeweka hoja kwamba vijana hawataki kuoa. Ukaweka na sababu ambazo wewe unahisi ndio zinafanya vijana hawataki kuoa.
Unfortunately Sababu ulizoorodhesha hazikua na mashiko ndio mimi nikaja kuzipinga na kukuonyesha kwamba sio hivyo. Huwezi kujisifu kwamba nyie mlikua mnatembea kilometa 20 halafu useme eti sisi hata 1km tunapanda boda.
Nikuulize
Hizo km 30 mlizokua mnatembea mlizitembea mkiwa mnapenda au kwasababu usafiri ulikua ni shida.? Wazee kama nyie ndio mnaonaga kiteseka kwa watoto ni sifa eti kwakua nyie mlilalia mkeka basi na watoto walalie mkeka. Kila era na mambo yake.
Point nilizonukuu kwako pale juu hazina mashiko kabisa.
Ndoa ni ibada kwenu. Usilazimishe wote tuamini unachoamini wewe.Ni aibu Mwanaume mwenye akili timamu kukataa ndoa kwani ndoa ni ibada, mtu akisema anajipanga kwanza aoe hapo tutaelewa au akisema muda ukifika ataoa hapo sawa lakini wanaokataa ndoa hawana hoja kabisa,
fugaku nimezisoma hoja za vijana ni nyepesi mno na kwakweli hazina mantiki na kuna vitu hawavielewiHii mada ya kataa ndoa inabidi ijibiwe kwa hoja, hawa vijana wanaoikataa ndoa ukute wana mantiki kubwa sana, inaitaji umakini mkubwa sana kuwaelewa na kuweza kujibu hoja yao ya msingi.
Kwa mimi binafsi nadhani kuna utofauti kubwa kati ya kuoa na kufunga ndoa.
1. Naanza na kuoa.
Wazee wetu wa zamani walikuwa wanaoa siyo kufunga ndoa. Ndiyo maana familia zao ziliweza kuishi kwa amani kubwa sana na kuheshimiana tofauti na sasa. Mwanamke alikuwa ana adabu kubwa na anamtii mme wake. Hakukuwa na tamaa za mali ambazo kwa asilimia kubwa zinavunja familia. Mwanamke alijua anatoka kwao anaenda kuolewa na kuanzisha familia na siyo kuchuma mali.
2. Ndoa
Ni upgrade ya kuoa ikiwa na maana hii ifuatayo.
Tafsiri ya ndoa za kipindi hiki ni kama ajira ama taasisi ya biashara yaani startup ambayo founders wawili kila mmoja ana share ya 50% ya ownership. Ambapo anytime founder yeyote anaweza kuharibu hiyo taasisi iliyoanzishwa na kuondoka na 50% yake. Na hii imetengenezwa kwa ajili ya favour ya mwanamke, power ya mwanamme ni kama haipo kwenye ndoa. Ndoa imeegemea upande mmoja na wanawake wanatumia iyo weakness vibaya sana. Hakuna mwanamme anayeweza vumilia kukaa na mwanamke malaya, mjeuri, mwenye kiburi, asiyemsikivu e.t.c eti kisa kafunga naye ndoa.
Maoni yangu ni kwamba turudi kwenye utaratibu wa zamani yaani tuoe na tuzae ila tusifunge ndoa. Ndoa zimekuwa za kitapeli.