Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unampata wapi fundi wa uhakika ilihali hujawahi kumiliki Gari?Jitahidi kuwa na fundi wa uhakika..!
Unawashirikisha wadau wenye gari au wanaojuana na mafundi.. Watakupa muongozo mzuri tuu..Unampata wapi fundi wa uhakika ilihali hujawahi kumiliki Gari?
Na huyo Fundi asiwe na tamaa, kama ataweza kuvuka Mtego wa Hela.....Unampata wapi fundi wa uhakika ilihali hujawahi kumiliki Gari?
Be forward wana kipindi maalum Cha offer. Gari ya 6,000 USD unapata kwa 2,500 USDSiku hizi magari yamekuwa bidhaa iliyozagaa kama Madera pale Kariakoo.
Kuna gari yard.. Kuna za minada.. Kuna za mikononi..
Gari za mikononi ni pendwa kutokana na bei yake kupoa kidogo.. Ingawa udalali ni mwingi.. Maneno kama AC unaganda.. Gari ya kufugwa.. Gari ya Mhindi..Namba D hiyo.. Safari popote.. Usitume sms unachelewa.. Jiandae kukutana nayo..!
Changamoto ya hizi gari..
1. Ujanja ujanja mwingi.. Dalali anauza gari ambayo hata yeye haifahamu, hapo lazima aweke chumvi zake.. Atakwambia hii gari service haivuki km 3000 na Castro oil ndio inatumika.. Ukimuuliza mwaka wa gari.. Engine code.. Kilometers.. Lazima akate simu kwanza akavute pumzi..!
2. Gharama ya fundi kwa ukagauzi.. Inabidi nje ya bei ya manunuzi uandae fundi wa kwenda kukagua.. Masega kama yapo au walishayatoa..! Gari ilishapata ajali.. Gari ilisharudiwa rangi.. Uaminifu ni mdogo..!
3. Uwe na smartphone na bando.. Hii ili kukagua madeni ya gari.. Gari za mkononi unakuta ina madeni ya kutosha.. Kuna deni la polisi.. Kuna deni la parking.. Na muuzaji hasemi anajikausha tuu.
4. Gari inaweza kuwa ilitumika kuchukulia mkopo mahali.. Hii hatari zaidi.. Muhimu kukagua kabla hujafanya malipo..! Uone kadi OG ya gari.
Kununua gari ya mkononi hakukupi option ya kuchagua gari zaidi unachofanya ni kukagua.
Tofauti na Be Forward ambapo unaweza ukafumba macho ukapoint gari yoyote. Changamoto ya Be Forward ni jinsi unavyozidi kuscroll down ndio bei inaongezeka..!
Hata Yale ya yard mengi Yana ujanja ujanja tu, pote ni kubahatisha, gari za mikononi kwa watu unaweza ukapata iliosimama mpka ukashangaaa! Nilinunua matako ya nyani kwa mwarabu mmoja hivi kwa 14.5m nikakaa nayo wiki 2 nikaiuza 24m kwa mtu wangu wa karibu sana na iko imara balaa, mpaka sasa ina km 68,000 haina shida yeyote
Kumbe hiyo ndio maana ya "gari ya kulenga"..!Hio ilikuwa gari ya kulenga, gari za hivyo huwa zimenyooka na bei kitonga sababu huwa unaipata kwa mwenyewe na haijapitia mikono mingi.
Ni kipindi gani hicho mkuu?Be forward wana kipindi maalum Cha offer. Gari ya 6,000 USD unapata kwa 2,500 USD
Umasikini unakosesha fursa.Paragraph ya mwisho imenichekesha
Hii hutokea kama bahati tu mfano mie kuna mtu nimemuuzia Allion juzi kati hapo ile gari condition yake ni kama mpya tu maaana gari imekaza kila idara anzia engine mpaka Body!Kumbe hiyo ndio maana ya "gari ya kulenga"..!
Unawezaje kulenga wakati dalali hataki ukutane na mwenyewe..!?
😆😆😆Kuna Mwanangu alienda na Fundi wake kukagua Gari vile anafika kisiri siri Fundi akakamatishwa 150k na Madalali Mkononi, basi Bwana Fundi akaanza kuisifia ile Gari kama yake kumbe Kimeo..... baada ya kununua Jamaa ikaanza kumsumbua hadi alijuta kuinunua