Wakili
JF-Expert Member
- Jun 19, 2017
- 531
- 657
Habari wapendwa,
Leo napenda tuzungumzie hili suala la ulevi na athari zake na jinsi linavyoumiza familia na jamii kwa ujumla.
Wapendwa ulevi ni tabia mbaya ambayo mtu hujijengea taratibu akizani ya kua yupo sawa kumbe anajimaliza siku hadi siku.
Kwa mfano ulevi wa pombe tuache bangi na sigara hivi pia nitavizungumzia mwishoni,sio siri madhara ni makubwa watu hujidangaya kunywa kwa kujilinda na kujipa matumaini kua mfano bia mbili tatu hazitanidhuru lakini ukweli ni kua unapokua katika utumwa huo jua fika unaharibu mwili wako mpendwa, akili zako utajidanganya kua zitakuwa salama zaidi unavyotumia pombe lakini ukweli wa kisayansi ni kua unapelekea kemikali aina ya dopamain kuzalishwa kwa wingi katika ubongo na kupelekea ubongo kuratibu matendo ya mwili vibaya, yaani kupungukiwa utimamu, huu ndio ukweli na uache ukuingie vizuri na uelewe na kubadilika wewe kama mtumiaji
Achilia mbali hizo athari za ubongo lakini ukweli ambao unauma na wengi hujipa matumaini na hawataki kuusikia ni kwamba mwili hau hitaji kemikali ya alcohol na sivyo Mungu alivyokuumba.
Binafsi nilishawahi kua mtu miaji wa vilevi laini kama bia hadi gin na whisky.Ukweli ni kuwa wakati nimeshatumia mwili ulikua ukipata shida hasa mfumo wa upumuaji, ile hali kuhisi hewa kubanwa puani na kuvuta hewa kwa shida.
Athari nyinginezo ni pamoja na kua mjinga mfano kupoteza concentration na mambo yako binafsi huku ukijali na kupigania muda wa unywaji zaidi.
Athari ni nyingine ni kuponea chupuchupu kupata ajali.Mifano niliyoishihudia kwa macho yangu mawili ni vifo kwa upande wa ndugu,mtu aliyekua akisifika kwa kugida chupa za bapa na pombe laini alifariki dunia mwaka jana mwishoni kwa maradhi mabaya ya ini.
Inasikitisha sana wapendwa kuona jinsi jamii inavyoumia na kupoteza nguvu kazi ya taifa katika ulevi, sasa hivi ulevi umekua ni kitu cha kujivuna na kuongeza status yaani kama wewe sio mlevi basi utaonekana mjinga na mpumbavu katikati ya watu na marafiki.
Mimi binafsi nilikua mlevi wa bangi na sigara kwa miaka sita sasa na pombe karibia miaka mitatu,ukweli ni kua hakuna faida niliyopata au cv niliyojenga kutokana matumizi ya vilevi hivyo zaidi yake ni hasara,kupoteza heshima na uhusiano wangu na familia na jamii kwa ujumla.
Nakusihi mpendwa kama wewe sio mtumiaji mwombe sana Mungu kwa kunia usiingie katika mtego huu ni hatari mno mno na tena mno kwa maisha yako mazuri hadi uzeeni, na kwa wale watumiaji jitahidi uache mara moja maana inawezekana mtu asikudanye kua eti punguza kidogo kidogo huo ni uongo na ni ngumu kuacha kwa namna hiyo,mimi binafsi ni shahidi na niliacha vyote mara moja kirahisi tu.
Nakaribisha maswali.